Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,547
- 41,059
Ukiutazama mkataba wa bandari kati ya DP na Tanzania, ni vigumu sana kuamini kuwa waliouandaa na kuusaini walikosa uelewa wa mapungufu yote yaliyo dhahiri kiasi ambacho hata asiye na uelewa mkubwa angeyaona.
Sasa tujiulize, hivi kweli ilikuwa ni kutokana na kukosa uelewa wa waliohusika, au kuna dhamira iliyojificha nyuma yake ambayo imetafutiwa pakuanzia? Je, yawezekana imetafutwa njia ya kuvunja Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar au kuufanyia marekebisho makubwa Muungano wetu? Kuna mambo tunayotakiwa kujiuliza:
1) kuwaondoa watu wote wa Tanganyika kwenye kukamilisha uporaji huu wa bandari ilikuwa ni kwa bahati mbaya au mpango uliokuwa umesukwa? Mpango ulianzia kwa kuwaondoa Watanganyika kwenye nafasi zote ambazo wangeshiriki kwenye maamuzi: mkurugenzi wa bandari, Katibu Mkuu wa wizara na Waziri; na Mwanasheria mkuu akawekwa pembeni.
2) vikawekwa vipengere vya mkataba, kama vile DP kuwa na mamlaka ya kutaja eneo lolote la ardhi analolitaka, na serikali kulazimika kuwaondoa watu na kuwalipa fidia, kisha kuipa DP ardhi hiyo bure. Ni kama imetafutwa njia ya kuamsha hasira ya Watanganyika dhidi ya waliofanya maamuzi ambao wote ni Wazanzibari.
3) kuziondoa bandari za Zanzibar, wakati suala la bandari ni la Muungano. Hii nayo huenda imefanywa makusudi ili kuonesha wazi kuwa mkataba ni wenye dhamira mbaya. Na kwamba Watanganyika wafure, na kisha wajenge chuki dhidi ya Zanzibar.
4) Katikati ya mjadala wa bandari, makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar anatamka kuwa katika nchi hii hakuna mkataba wa hovyo kama mkataba wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar. Ubaya wa mkataba wa bandari una uhusiano gani na ubaya wa mkataba wa Muungano?
Je, mkataba huu wa hovyo wa DP umefanywa makusudi ili Watanganyika waone umuhimu wa kuupitia upya mkataba wa Muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika?
Je jambo hili huenda limefanyika makusudi ili kufanyia marekebisho makubwa ya mkataba wa Muungano au hata kuuvunja kabisa? Kama ndivyo hivyo, waliolipanga hili wamepanga chuki ifikie kiwango gani ili lengo lao litimie?