Gharama ya kujenga darasa kutokana na fedha za COVID-19

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
TAMISEMI imetoa maelekezo kuwa gharama ya kujenga darasa moja kwa fedha za msaada wa Covid-19 ni Tshs.20,000,000. Kama majengo haya yatajengwa na Wakandarasi waliosajiliwa naona haya hayakutiliwa maanani:-

(1) Mkandarasi aliyesajiliwa anapolipwa lazima akatwe withholding tax ambayo ni 10% ya gharama ya mradi.
(2) Lazima alipe insurance kwa jengo analojenga
(3) Kama ikibidi atatengeneza samani kwa fedha hiyo
(4) Nchi nzima gharama ni 20M bila kujali umbali na maeneo ya nchi. Mfano bei ya saruji kwa Wilaya ya Tunduru, Nkasi, Kyerwa, Rorya, Kigoma Vijijini, Uvinza, Nachingea n.k siyo sawa na Ilala, Morogoro, Tanga.

Mbona vitu kama hivi havikutiliwa maanani na Tamisemi? Kwa gharama zilizotolewa na Tamisemi itamlazimu Mkandarasi ajishauri sana kabla ya kuomba kandarasi hii.
 
Darasa la ukubwa gani kwanza, kwa mfano 10×6 m² kwa nini zisitoshe .Sina uhakika kama samani zimejumuishwa kwenye gharama za ujenzi.
Hoja ya jamaa hapo ni gharama kuwa sawa bila kujali mahali
Ni kweli bei ya saruji Kigoma ni 25000,wakati kwa dar ni 16000
Hivyohivyo kwa Bei ya nondo na materials mengine
 
Hoja ya jamaa hapo ni gharama kuwa sawa bila kujali mahali
Ni kweli bei ya saruji Kigoma ni 25000,wakati kwa dar ni 16000
Hivyohivyo kwa Bei ya nondo na materials mengine
Unachosema ni sahihi kabisa. Lakini usisahau kwamba bei ya mchanga, kokoto, mawe, mbao na labour charge Kigoma nI rahisi kuliko Dar kwa hiyo kuna namna fulani gharama zina balance japo siyo lazima ziwe sawa 100%.
 
Pesa zimeingizwa kwenye account za shule, maana yake hiyo ni "force account".

Mkandarasi hawezi jenga darasa kwa million 20 pamoja na kuweka samani madarasani hiyo pesa haitoshi kabisa.

Hata hii force account Kuna hatihati isikamilike.
 
TAMISEMI imetoa maelekezo kuwa gharama ya kujenga darasa moja kwa fedha za msaada wa Covid-19 ni Tshs.20,000,000. Kama majengo haya yatajengwa na Wakandarasi waliosajiliwa naona haya hayakutiliwa maanani:-

(1) Mkandarasi aliyesajiliwa anapolipwa lazima akatwe withholding tax ambayo ni 10% ya gharama ya mradi.
(2) Lazima alipe insurance kwa jengo analojenga
(3) Kama ikibidi atatengeneza samani kwa fedha hiyo
(4) Nchi nzima gharama ni 20M bila kujali umbali na maeneo ya nchi. Mfano bei ya saruji kwa Wilaya ya Tunduru, Nkasi, Kyerwa, Rorya, Kigoma Vijijini, Uvinza, Nachingea n.k siyo sawa na Ilala, Morogoro, Tanga.

Mbona vitu kama hivi havikutiliwa maanani na Tamisemi? Kwa gharama zilizotolewa na Tamisemi itamlazimu Mkandarasi ajishauri sana kabla ya kuomba kandarasi hii.
Hapa jiran mtaa ninaokaa ilijengwa shule ya msing kwa sh milion 400 kipind cha maguful mwezi wa 12 mwaka jana na shule ikaisha ndan ya mwezi ina madarasa 14 ofice za walimu 2 na nyumba ya walimu kubwa tuu ilijengwa na kandarasi wa kike ndan ya mwez mu1 na ikakamilika kwaiyo iyo 20 n nying sana inatosha hata na madawati nanukuu " tuseme ukwel ndugu zangu milion 20 n nyingi sana na inatosheleza kwa darasa 1 kamili full na shelf la ndan kabisa la kuwekea vitabu na madaftar ata madarasa ya private sidhan kama huwa yanazid M 20 kwa kila moja
 
Kama mkandarasi atapewa kazi ya ujenzi binafsi millioni 20 hazitoshi kutokana na gharama zifuatazo:- (1) Kukatwa witholding tax ya 20% (2) Kukatwa service levy ya Halmashauri (3) Bei ya vifaa vya ujenzi kama nondo, mabati gauge 28, misumari, mbao nk kwa maeneo ya pembezoni na bado usumbufu wa Wahe. Madiwani.
 
Back
Top Bottom