Ghalama za power tiler toka nje

Vitalis Msungwite

JF-Expert Member
May 11, 2014
3,283
7,834
Wakuuu,nimejaribu kupitia nyuzi mbalimbali zinazohusu power tiler lakini nyingi ni 2012 kurudi nyuma. Pia watu wengi wameshamaliza mizigo hiyo. Sio kwamba hazipo mtaani,zipo ila bei si rafiki sana,nimejaribu kuangalia mitandaoni nimeona kuna uafadhari iwapo itaagizwa moja kwa moja.

Kupitia alibaba bei zina range US$80-150 kwa used, na 500-1200 kwa mpya kwa seti moja. Kilichofanya nije hapa ni kubadilishana mawazo juu ya njia bora ya kununua hizi mashine.
Mtaani bei ni Tsh 3.5mil-11mil,ukiangalia hizi bei ni km Mara tatu ya zile za mtandaoni.TUSAIDIANE KATIKA

GHALAMA NA TARATIBU ZA USAFIRISHAJI

Watu wanaoagiza magari anaweza kuagiza moja na akaletewa,je kwa upande wangu naweza kuagiza seti moja tu! Na nikaletewa?. Pia nimeangalia mizigo mikubwa huwa kwenye makontena,lakini powertiler set moja ni box moja tu la mbao,je kunauwezekano wa kusafirishwa katika hali hiyo?

Pia ghalama za bandalini zipoje kwa upande wa powertiler au hupigwa hesabu kwa kontena zima?
Tusaidiane maana isije kuwa ghalama ni kubwa kuliko za mitaani au nikalizwa tu mitandaoni

af7a4b04d56768de5cc6e462e563258e.jpg

UPDATES: NIMEPATA POWER TILLER MPYA

Nawashukuru wadau wote kwa michango ya mawazo na wengine mliokuja PM kunipa muongozo n.k. nilipoona mipango imeyumba niliipeleka hela kwenye kilimo. Mwaka huu nimepata 8mil na katika pita pita mtaani nikapata taarifa juu ya power tiller zinazoizwa na mbunge wa mbarali kwa bei ya 2 mil ikiwa full kila kitu eg disc plough, Rotavator, iron/Cage wheels+trailer.

Mwezi may 27 2018 Nimechukua hiyo na mpaka sasa inapiga kazi za kusomba mchanga,tofari na mazao nimerudisha kwa hiyohiyo.

Nimenunua Amec 18 HP

Nawashukuruni sana kwa michango yenu ya mawazo , kama nawe utahitaji nitakusaidia uipate

Picha zinagoma kupanda
 
Last edited:
kama umeona mtandaoni jaribu kuwasiliana na kampuni inayo uza kama wanaweza kukuuzia 1 set.kuhusu utumaji wake unaweza ukawapa address wakutumie TZ ,kisha ikifika utalipia ushuru.ama wakutumie kwenye kampuni za kusafirisha mizigo toka china kwenda Tz.ukitumia njia ya pili nadhani ni rahisi kwani utoaji wa bandarin watatoa wao.wewe ni utafata ware house kwao mzgo ukisha fika.
kila la kheri mkuu
 
Kuwa makini na mashine za kichina mkuu especially hizi za bei chee. Kuharibika mara kwa mara, upatikanaji wa spare ni shida unless unaenda kulimia kwenye shamba lako mwenyewe na sio kukodisha.

Manufacturer /supplier atakupa bei ya pamoja na gharama za usafirishaji ila hakikisha inafanyiwa inspection huko wakutumie na certificate yake ya kapeleka tbs.

Power tiller unalipia vat tu ambayo ni 18% ya thamani ya mzigo wako shipping cost included pamoja na gharama nyingine za bandari. Agency fee 250 elf na pia inspection kule China inaweza cost dola mpaka 300.
 
Ok sawa ngoja nijipange
 
Ghalama = gharama

Tiler = tiller

Na ndiyo sijaisoma post yote.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Sasa wewe ki power tiller kimoja unataka ukanunuwe nje ya Tanzania?

VipoTanzania tena bei nzuri, unapewa na mtaalam wa kukufundisha kukitumia na unakuwa na guarantee ya muda fulani. Jamani.

Nje agiza container zima, siyo ki power tiller kimoja.

Watu kama wewe ndiyo mnachapwa visenti vyenu mtandaoni.
 
Najua kukitumia na najua vipo vingi nchini,kilichofanya niangalie mtandaoni ni bei bibi yangu. Huko ni US$ 1000 maximum = 2.3 mil,pamoja na cost zote approximately 3.5 mil wakati madukani ni 8-11 mil. Nikishindwa bora niache tu lakini lazima nithubutu
 
Ghalama = gharama

Tiler = tiller

Na ndiyo sijaisoma post yote.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?[/QUOTE
ni janga la kitaifa kwa sasa, cha ajabu hata waandishi wa habari wamo kwenye hilo janga. utasikia wakisema, " ahabari zilizotufikia hivi punde" baadala ya habari zilitu......" hayupo, eti ayupo" alama eti halama", sijui ndo sifa.
 
Sasa wewe ki power tiller kimoja unataka ukanunuwe nje ya Tanzania?

VipoTanzania tena bei nzuri, unapewa na mtaalam wa kukufundisha kukitumia na unakuwa na guarantee ya muda fulani. Jamani.

Nje agiza container zima, siyo ki power tiller kimoja.

Watu kama wewe ndiyo mnachapwa visenti vyenu mtandaoni.
Dah!kuna watu wengine sijui wameumbwaje,mtu anaomba muongozo badala ya kumsaidia unaingiza dharau eti "ki power tiller kimoja"?
 
Dah!kuna watu wengine sijui wameumbwaje,mtu anaomba muongozo badala ya kumsaidia unaingiza dharau eti "ki power tiller kimoja"?

Sasa ki power tiller kimoja ukiagize kutoka nje ya nchi wakati hapa vimejaa tena bei poa, kama si upunguani huo ni nini?

Huo niliompa ni muongozo tosha kabisa na msaada mkubwa kwa wenye kufikiri.

Wewe unamuongoza aagize nje, siyo?
 
Maana yangu ni kwamba km unajua wanavyouza na bei yake kwa hapa nyumbani na nje ya nchi mpe ili aamue mwenyewe kusuka au kunyoa.
 
Back
Top Bottom