Gesi Mtwara: Bibi wa Msimbati, nimeamini maneno yako

Gesi Mtwara: Bibi wa Msimbati, nimeamini maneno yako

kama imefika kinyerezi mgao wa nini??
Unaonaje ukifanya utafiti kidogo kuhusu sababu za mgao kwa sasa. Nimekusaidia kukujulisha kuwa gesi ya Mtwara siyo tatizo imeshafika Kinyerezi tena kwa pressure zaidi ya iliyotarajiwa.
 
Damu ya watanzania iliyo mwagwa mtwara kisa gesi itawalilia milele,kilio chao ndo kinafanya gesi inakua kitendawili tena kwenye kuzalisha umeme,rudini muwaombe msamaha
 
Ukawa mpapiga kura DW kwenye utafiti wao wa wagombea urais?
 
Aliwambia waki2mia nguvu 2 bac ges haitofka dsm hayo mabomba yatatoa maj.
 
Bibi wa Msimbati alishasema gesi haitoki, CCM na Serikali yake wakaenda kupiga na kuua wananchi wa Mtwara wasio na hatia. Juzi kwa mbwembwe na madaha tumeambiwa mitambo ya kuzalisha Umeme wa gas umewashwa na mgao itakuwa ni jambo lililobaki Kwenye Vitabu Vya historia.

Wakati Simba Chawene alijinasibu kwa madaha mbele ya umma kuwa tatizo la umeme litakua historia, leo gazeti la Mwananchi limeandika Eng. Mramba wa TANESCO anasema mgao wa umeme haukwepeki kwani uzalishaj wa umeme umeshuka toka 561 megawatts mpaka 105 megawatts kutokana na ukame ulioikumba nchi...

Swali la kujiuliza; Gas iliwashwa au ilikua changa la macho?

Maneno ya Bibi wa Msimbati ndio ukweli mtupu, Gesi HAITOKI!

Tangazo , Tangazo, Tangazo ukiona maeneo unayoishi umeme wa Tanesco umewaka zaidi ya wiki bila kukatika tafadhali utoe taarifa kituo cha Tanesco kilichopo karibu na eneo unaloishi itakuwa kuna tatizo la hitilafu ya umeme.
 
Aliwambia waki2mia nguvu 2 bac ges haitofka dsm hayo mabomba yatatoa maj.

ha ha ha kuna kisa cha mfereji wa maya kule same uliopangwa kupeleka maji sehemu.ya Igoma ili watu wa milimani washushwe tambarare kulima pamba wazee wa kipare wamwambia DC wa kiingereza hautafikisha maji Igoma kwa kuwa hawako tayari kushuka tambarare kuumwa na mbu. kweli mkoloni mwingereza aliuchimba miaka bila mafanikio baada ya uhuru miaka ya 70 serikali ya nyerere iliuchimba kwa miaka kadhaa nayo ikashindwa. ajabu maya iko milimani na igoma iko bondeni lkn maji hayaendi
 
Bibi wa Msimbati alishasema gesi haitoki, CCM na Serikali yake wakaenda kupiga na kuua wananchi wa Mtwara wasio na hatia. Juzi kwa mbwembwe na madaha tumeambiwa mitambo ya kuzalisha Umeme wa gas umewashwa na mgao itakuwa ni jambo lililobaki Kwenye Vitabu Vya historia.

Wakati Simba Chawene alijinasibu kwa madaha mbele ya umma kuwa tatizo la umeme litakua historia, leo gazeti la Mwananchi limeandika Eng. Mramba wa TANESCO anasema mgao wa umeme haukwepeki kwani uzalishaj wa umeme umeshuka toka 561 megawatts mpaka 105 megawatts kutokana na ukame ulioikumba nchi...

Swali la kujiuliza; Gas iliwashwa au ilikua changa la macho?

Maneno ya Bibi wa Msimbati ndio ukweli mtupu, Gesi HAITOKI!
Rejea hapo juu kwenye redi.Tanesii Iko ni sawa na serikali ya CCM suala limabadilika kutoka kuwa historia hadi kuwa Sayansi.Nawaambia msitegemee chochote kutoka wenye kampuni yenyekuendeshwa na CCM.Maana Taa Nee Siko na taasisi yao.
 
naomba nimfahamu huyo bibi.
hili linanikumbusha Iramba kuna mahali maji yanatolewa na kusambazwa mjini,
wale wazee wa pale wakaomba na wao wapatiwe maji ya bomba wahusika wakakataa,
wale wazee wakasema mtakunywa hayo mabomba na maji hamtayaona
watu hawakuamini yaani ilikua wakifunga tu mtambo unaharibika na maji miezi kadhaa hakuna,
mpaka wenye mamlaka walipokwenda kuongea na wazee.

ndicho kilichotokea kwa huyu bibi, ingawa serikali inajifanya haiamini sana mila (uchawi) lakini cha moto wanakiona. kuna wakati mawe ya huku yaliaza kwisha eti kuifukia bahari ili mitambo iwe salama..looh.
 
NDo sisi Malofa tunapga kura chama cha Nyerere fyuuuuuuus
 
Labda tatizo.la mgao limegeuka kua jiografia au sayansi ndio maana hauishi
 
Mgao utaisha tutakapo pata kiongozi mchapa kazi, naamini ni Magufuli pekee atatutoa kwenye mtihani huu

Kwanza nakuomba ukiri kuwa JK amefeli katika mtihani huo na kisha utueleze (JK) amefeli wapi katika mtihani huo?

Vinginevyo usemalo nalo ni changa la macho.
 
Kwa mfano....
Unaanzaje azanje kuipenda ccm hasa ukute ni mkazi wa dar
1 Foleni

2 Shida ya maji kwa majimbo yote ya dar

3 Kiza,mgao wa umeme,,,,,,
 
Gathering satellite field stations?
Huyo jamaa ni mtaalam lakini ni muongo.
Tatizo watanzania tukiona maelezo mengi na kiingereza huko ndani hatutaki kufuatilia details!
Na ndio tunavyoibiwa!!
Sehemu nyingine kama hujui kusoma hata picha basi uelewe, sasa satellite inatokea wapi kwenye gas?

Toa wewe basi maelezo au hizo process kumkosoa uyo jamaa sio unaandika pumba tu. Unakosoa na kuweka right process na kuanisha wapi yuko wrong by the way amesema kaambiwa. Unapinga halafu una altenrnative ya uchambuzi upuuzi kabisa. Una shaka na satelite? Hivi unaelewa maana ya satelite? una shinda mtandaoni halafu hauelewi maana ya satelite na inatumikaje, au ndio nyinyi mnaoshinda mtandaoni na kutafuta skendo za wahamasishaji ngono na pombe kwenye jamii. Bila shaka utakuwa ninyiemu wewe, maana huko ndio waliojaa wenye fikra za namna hiyo.
 
Ila nilisikia kwamba Pombe Magufuli alisema gesi wamepewa wachina...sasa isijekuwa sisi tunaona na kushangilia bomba lisilo na kitu. mwisho wa siku bomba hilo tutapitishia maji yatokayo mto Rufiji na Ruvuma ili wakazi wa Dar waondokane na adha ya ukosefu wa maji. Angalau.

Kwa hiyo kuna mirija iendayo china kwa raha zao au ikoje!! Au wadhungu wamejikokia kwenye manowari zao kwa raha zao!! TZ utaipenda kwa vituko vya wasanii viongozi!
 
Back
Top Bottom