Next Level
JF-Expert Member
- Nov 17, 2008
- 3,153
- 176
Nasikitika kuwajulisha kuwa Ndugu Gervas Mkili hatunaye tena. Mkili alifariki jana Jumapili pale Hospital ya Muhimbili wakati akipatiwa matibabu ya Moyo, tatizo lililogundulika siku moja kabla ya kifo chake.
Kwa wale waliopitia UDSM, bila shaka hawazi kumsahau kijana huyu machachari pale mlimani miaka ya 2000 mpaka 2004 hivi.....! Kama mtakumbuka kijana huyu aliwekwa mahabusi pamoja na vijana wengine kwa sababu ya kuongoza harakati za kudai haki za wanafunzi pale mlimani, ikiwa ni pamoja na BUMU kuongezeka. Na mtakumbuka kutokana na juhudi zake, tuliweza kuongezewa bumu kutoka Tshs 2000 hadi 2500....na kutokana na hili, kuna mgomo uliandaliwa ili kuhakikisha Mkili anatoka SERO, na hili lilifanikiwa baada ya Mzee Luhanga mwenyewe kwenda kumtoa kijana huyu na kutuletea pale Nkrumah na ndip mgomo ukasitishwa!
Mkili mpaka anafariki alikuwa Principal wa shule za Green Acres na alikuwa na mke na mtoto mmoja!
Mwili wa marehemu unatajiwa kusafirishwa leo kuelekea Shinyanga kwa mazishi, kwa walio Dar es Salaam msiba upo nyumbani kwake Mbezi Beach na sasahivi maandalizi ya safari yanafanyika Muhimbili Hospital!
Pole sana dada Deodatha (mjane), pole sana Mama Deo, pole sana Eddie, pole sana Mranda, pole sana Josephine, pole sana Baba Carol, pole sana David (Daz Mwalimu)!
Rest in peace man MKILI......I will indeed miss you!
There is no way out to escape such a divine gift, we loved you brother but God has loved you the most! Umetangulia sisi nasi tutakinywa kikombe hicho. Jina la bwana lihimidiwe milele na milele. Amen