Sex is no more an issue, know how to handle your man

Mr George Francis

Senior Member
Jun 27, 2022
186
212
SEX IS NO MORE AN ISSUE, KNOW HOW TO HANDLE YOUR MAN.

Leo katika pitapita zangu nimekutana na wadada fulani hivi wanapiga story. Mmoja nilisoma nae sekondari lakini hatukuwahi kuonana tangu siku tumehitimu kidato.

Sikuwa na uhakika kama ni yeye, nilisimama kwa muda kiasi nikiwatazama huku nikitegea sikio story zao.
Mdada mmoja akasema,
"Mwenzangu wee!! Wanaume wa siku hizi yani sijui wapoje!!? Mtu ukishampa penzi lako tu anatafuta njia ya kuondokea."

Yule mwingine niliyewahi kusoma nae, akadakia,
"Mh!! Shoga yangu!! Me naona usipompa ndio wanakukimbia kwasababu anaona kama vile humpendi."

Wakamalizia na kicheko cha pamoja,
"Heheheheee!! Paaaambee!!!"

Wakageuka upande niliposimama mimi, macho yetu yakakutana na hapo ndipo nikapata uhakika kuwa kweli ni yeye yule ninayemfahamu.

Nikasogea karibu yao, tukasalimiana kisha nikawa na jambo hili la kuzungumza nao.

🪐Tendo la ndoa (sex) haiwezi kuwa sababu ya mwanaume kuachana na mpenzi wake au kuendelea kudumu nae. Elewa kuwa kuna tofauti kati ya upendo na tamaa za mwili. Upendo wa kweli hausukumwi na tamaa za mwili.

🪐Mwanaume anayekupenda, ataendelea kukupenda hatakama hamtashiriki tendo la ndoa kabla ya kuoana.

🪐Na pia kama anakupenda, ataendelea kukupenda hatakama mtashiriki tendo la ndoa marakwamara kabla ya kuoana.

🕸️Lakini issue ni kwamba, tukiondoa swala la tendo la ndoa kwenye mahusiano yenu ni kitu gani kingine cha ziada unachoweza kushare na mpenzi wako ili kuboresha mahusiano yenu!?

🕸️Ni kipi hasa mnachozungumza pale mnapopata nafasi ya kuzungumza ?

🕸️Unamsaidiaje mpenzi wako katika kukua kiroho na kiimani?

🕸️Unamsaidiaje mpenzi wako katika kukua kiakili na kupata mawazo mazuri ya maendeleo?

🕸️Unamsaidiaje mpenzi wako katika kukua kiuchumi kwaajili ya kesho yenu iliyo bora?

🕳️Au wewe ni yule ambaye unatamani zaidi pesa au vijisenti vyake?

🕳️Au wewe ni yule ambaye unaona kumchuna mpenzi wako ndio ujanja wa mjini?

🕳️Au ni wewe yule ambaye unapenda zaidi kupewa kuliko na wewe kutoa?

🕳️Au wewe ni yule ambaye kila siku ni kuomba vocha arafu ukitaka kuongea nae unatuma tafadhali nipigie?

🕳️Au wewe ni yule ambaye badala ya kujenga maisha unapenda outs na kufanya matumizi yasiyo ya lazima?

Maisha ya mwanadamu yametawaliwa na kitu kinachoitwa "KARMA"
yaani waluguru wanasema
"what comes around, goes around."
Kwa lugha rahisi tunasema
"Nipe nikupe." au
waebrania wanasema "mkono unaotoa ndio unaopokea."

Mtendee mpenzi wako vile ambavyo hata wewe ungependa kutendewa, usimtendee kile ambacho hata wewe usingependa kutendewa.

Ili kumteka mpenzi asikukimbie kwa namna yoyote, jitahidi sana kuwa yule mwanamke ambaye mpenzi wako atajihisi furaha kuwa na wewe siku zote za maisha yake na hasitamani kukupoteza kirahisi.

Mapenzi yanatengenezwa na mpenzi bora anatengenezwa pia. Tambua thamani yake na mfanye atambue thamani yako pia katika maisha yake.

Muhimu kabla ya yote ni kutambua lengo hasa la mahusiano hayo kabla ya kuyaanzisha. You're just dating au mna malengo ya kuishi pamoja milele.

Kujua lengo kutakupa mwongozo wa kufahamu mipaka yenu katika mahusiano husika. Nimalizie kwa kusema kwamba
"Sex is no more an issue, know how to handle your man."

#No_learnig_No_earning
So We Have To Learn

NAME: Mr George Francis
📩 mr.georgefrancis21@gmail.com
e7178145d1a14055b39f0e4fc7405827.jpg
 
Mbona hilo wanawake tulio wengi tunalijua?

Issue ni kwamba inategemea wewe ni mwanaume wa aina gani pia, ukiwa muhuni na mshenzi na sisi tunaenda na flow.

Ukiwa mstaarabu na unaonekana kabisa unafaa kuwa mume, vya ziada muhimu. Tunakuwa mpenzi, mshauri, mfariji, mshkaji na hata msaidizi.
 
Back
Top Bottom