Ukweli ni kwamba Gerson Msigwa ameshushwa Cheo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,789
218,426
Kuna Wakati mambo ya Nchi hii yanashangaza sana !

Pamoja na kwamba sifahamu vigezo vya Mtu kuteuliwa kuwa msemaji wa serikali , Lakini natambua kwamba kuwa Msemaji wa serikali ni dhamana kubwa mno , na kwa kadiri ninavyomfahamu Msigwa hakustahili kuwa Msemaji wa Serikali yetu ya Tanzania , Msemaji wa Serikali hawezi kuwa kama Msemaji wa Yanga , Haji Manara , au yule wa Clouds Mbwiga Mbwiguke , haikubaliki kuropoka ropoka tu , ni lazima Msemaji wa serikali ayajue mambo ya nchi yake na awajue viongozi wake , hata kama anatumwa , he/she must understand the mood of the people , body language yake ni lazima ifuate mawimbi ya anaowaeleza jambo .

Kwa kadri ya Kumbukumbu zangu , Msigwa ndiye Msemaji wa serikali Duni kabisa kuwahi kuwepo tangu Tanzania ianzishwe . Alishindwa kabisa kuitetea serikali yake hata kwenye mambo mepesi , hajui kabisa kipengere muhimu cha Propaganda , Msemaji wa serikali unapotetea serikali hata kama ni kwenye jambo linaloumiza Wananchi , Yaani wananchi wakikusikiliza japo wanalia lakini wawe wanatabasamu .

Nawashukuru waliopendekeza kwamba ashushwe cheo na kutupwa kwenye Ukatibu wa Wizara , Japo nimedokezwa kwamba hiyo ni njia ya kuondokea .
 
Nieleke tu kwamba Uzi huu umetayarishwa,umehaririwa na kupitiwa na mmoja wa think tank wa Chama kikuu Cha upinzani katika nchi ijulikanayo kama kisiwa Cha amani.

Ama kweli acha serikali elimu ya katiba na nionavyo miaka mitatu michache sana ilitakiwa kuwa elimu isiyo na kikomo
 
Nieleweke tu kwamba Uzi huu umetayarishwa,umehaririwa na kupitiwa na mmoja wa think tank wa Chama kikuu Cha upinzani katika nchi ijulikanayo kama kisiwa Cha amani.

Ama kweli acha serikali elimu ya katiba na nionavyo miaka mitatu michache sana ilitakiwa kuwa elimu isiyo na kikomo
 
Magufuli...
Samia asingekua Mwanamke....Makamo alikua ni Mwinyi.

Ndo mjue Samia yuko hapo Kwa sababu ya Uanamke wake ,sio Uwezo.,Uwezo alikua Mwinyi.


View: https://youtube.com/shorts/t0I3p8Lls5M?si=tMLB4Ko3gBZYeRFA

Kwa hiyo unaona kabisa 2025 ukichukua fomu ya Urais na hata kura zikihesabiwa uwanja wa Taifa unaweza kushindana na Rais Samia na ukashinda? Ikumbukwe Anayewaza hivi hajawahi hata kugombe uenyekiti wa mtaa na hata akigombea anaweza asishinde
 
Ukiwa Mtumishi wa serikali kuhamishwa ni Jambo la kawaida.Uteuzi huu nimeupongeza,wizara hiyo imepata mtu sahihi...Kongole Comrade GMsigwa
 
Tunasuka upya serikali kuelekea 2025! Tunapanga kikosi kipya baada ya cha sasa kufanya kazi kwa MUDA MREFU na wapinzani kukizoea!


Mabadiliko kwenye vitengo ni sehem ya mkakati mpya!

Elewa ndugu mlipa kodi!!
 
Tunasuka upya serikali kuelekea 2025! Tunapanga kikosi kipya baada ya cha sasa kufanya kazi kwa MUDA MREFU na wapinzani kukizoea!


Mabadiliko kwenye vitengo ni sehem ya mkakati mpya!

Elewa ndugu mlipa kodi!!
Nimefurahishwa na hapo mwisho uliposema "ndugu mlipa kodi" nimekuelewa sana !
 
Presidential appointees wanavigezo vinavyoendana na maokoto yale yale. Cha msingi ingia kwenye system huwezi lala njaa.
 
Sema Honestly Speaking nilichokuwa namkubali mshkaji hakuwa na maringo wala kujikweza na ni versatile ananyumbulika kuendana na mazingira. Ushawahi waza ikiwa ulifanya kazi na Magu na ukawa unakubali falsafa zake. Ghafla bin...... Anaingia huyu mmama ambaye hana hata vision na wewe inatakiwa umsapoti na kupromote mitazamo ya serikali yake... Kuna wakati ukivaa viatu vya hawa jamaa walioko serikalini unaona ni pagumu kiasi gani
 
Nieleweke tu kwamba Uzi huu umetayarishwa,umehaririwa na kupitiwa na mmoja wa think tank wa Chama kikuu Cha upinzani katika nchi ijulikanayo kama kisiwa Cha amani.

Ama kweli acha serikali elimu ya katiba na nionavyo miaka mitatu michache sana ilitakiwa kuwa elimu isiyo na kikomo
Ulitaka kusemaje yaani ?
 
Back
Top Bottom