Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 573
- 2,555
Mwanasheria Mohamed Salum amesema kuwa Kauli ya Kusema DP World watamiliki Maeneo yote ya bandari za Bahari, Maziwa na Nchi kavu ni kama posa tu, lakini mchumba mwenyewe atajulikana wakati wa kusaini mikataba midogo ya makubaliano itakayokuja baadae.
Amebainisha kuwa hilo ni jina tu lililotumika kama kichwa cha habari cha mkataba na halimaanishi kuwa mkataba utakuwa hivyo kwa baadae.
Pia, kwa kuwa kutakuwa na awamu mbalimbali za makubaliano, mikataba ijayo ndio itabainisha ni maeneo gani hasa ambayo DP World watapewa baada ya kumalizika kwa awamu ya kwanza ya makubaliano ya awali.
Ameyasema haya wakati akijibu maswali ya wadau kwenye mjadala unaoendelea Clubhouse ukiongozwa na Msemaji Mkuu wa Serikali ndugu Gerson Msigwa.
Chanzo: Msemaji Mkuu wa Serikali (Clubhouse)