FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 1,035
- 1,925
NOTE
HADITHI ZANGU ZOTE NI ZA KUBUNI TU HAZIHUSIANI NA MTU YEYOTE, TAASISI YOYOTE WALA MAMLAKA YOYOTE ILE WALA HAZILENGI KUMCHAFUA MTU, TAASISI AU MAMLAKA YOYOTE.
HADITHI: GEREZA LA HAZWA
UTANGULIZI....................
Mvua ilikuwa ni Kali sana majira haya ya usiku ikiambatana na upepo mkali ambao uliweza kuilaza chini miti yenye mizizi dhaifu, radi za kutisha ziliupamba masitu huo na kuufanya kuwa na mwanga kwa mbali majira hayo ya usiku wa manane. Ni ndani ya msitu Elnino upatikanao kusini mashariki mwa nchi ya Libya, ni msitu unao tisha sana hata ikiwa ni mchana una historia ya kupotezesha watu waliokuwa wanaingia humo hali iliyo pelekea watu kuanza kuogopa kuingia kwenye huo msitu, miti minene na iliyo shonana ilifanya giza muda wote hata muda wa mchana ndani ya msitu huo na ndiyo sababu ulimiliki viumbe vya kutisha sana kwa usalama wa maisha ya watu.
Majira haya ya usiku wa manane palitulia sana mvua na mjongeo wa maji ndicho kilichokuwa kinasikika sana na upepo mkali pamoja na radi zisizoisha zilizalisha mwanga ndani ya msitu huo, ndani ya tope zito mwanaume mmoja ambaye usoni kwake kulichafuka nywele za kutisha na ndevu zilizofanya hata sura yake isionekane alionekana akiwa anakimbia mno kuweza kuyaokoa maisha yake, hakuwa na namna angeweza kusimama alikuwa anakufa na hakuwa tayari hilo litokee, nyuma yake walikuwa wanakuja kwa kasi sana wanaume sita ambao wanne walivaa nguo za kininja hao walikuwa wanapotea na kurudi huku wawili wakiwa wamevaa magwanda ya jeshi ni wazi walikuwa ni makomando japo kwa lile giza ilikuwa ni ngumu kujua magwanda yao ni ya nchi gani.
Kisu kilikuwa kinakuja huku kikiwa kinajizungusha kilimkosa kichwa kikapita na nywele zake alihema kwa nguvu kisha hakuonekana tena, watu hao walifika hapo mmoja alijaribu kuvuta hisia kujua mtu huyo ameingia wapi lakini upepo ulikuwa unayapotezea utulivu masikio yake. Walipeana ishara ya kutawanyika wote wakionyesha alama ya kuua kwenye shingo kama wakimpata, baada ya kutawanyika hatua kumi na tano mbele yule komando mmoja ambaye alikuwa kwenye gwanda lake alihisi kuna tone limemdondokea lakini lilikuwa na harufu akajua wazi hilo ni jasho mkono wake ulikuwa kiunoni taratibu, ni kweli kuna mtu alitoka juu ya mti akishuka kwa kasi mithili ya paka kwenye kila kiganja kidole cha katikati kilikuwa na kitu kama pete ila haikuwa Pete kwa ajili ya mapenzi na mapambo bali Pete hizo zilikuwa na nyembe Kali sana tatu tatu kila upande na kufanya kuwa sita.
Komando aliikoki bastola yake mwa kisigino cha mguu wake aliirusha juu akiwa ameiachia kwa nguvu sana ikiwa inaelekea juu ya mti mrefu sana ambao ni wazi kwa juu kulikuwa na mtu anashuka kwa nguvu, bastola hiyo ilikuwa inajifyatua risasi yenyewe wakati huo komando alikuwa anapanda kwenye mti huo kama anatumia uchawi lengo alikuwa anamfuata mtu ambaye naye alikuwa anakuja aliko, bastola ilitoka risasi zote sita hakuna iliyo mgusa mtu huyo ikapigwa teke kwa nguvu wanaume walikuwa wamekutana Kati kati ya mti ilipigwa mikono kwa dakika moja kila mtu akiwa ameshikilia mti kwa miguu yake. Nywele za mtu huyo ambaye alionekana kuwa mchafu sana zilicheza upande wa jicho la kulia alijirusha kama anataka kupanda juu mpaka mti ulibonyea kwa nguvu alizotumia komando yule wakati anataka kumfuata alishangaa haoni chochote mbele yake alihisi mtu yupo nyuma yake wakati anageuka alikuwa amechelewa shingo yake ilikuwa inatoka damu nyembe zaidi ya sita ziliiharibu shingo yake, alijaribu kuchomoa bastola nyingine shingo yake ilikuwa tayari imevunjwa.
Baada ya kufanya hayo mauaji aligeuka nyuma mtu huyo mwenye nywele nyingi baada ya kutua chini kisu kilikuwa kimezama kwenye mgongo wake kilimlegeza sana lakini hakutaka kufia kwenye mikono ya hao watu wa kutisha ambao ni wazi aliwaogopa mno huenda alikuwa akiwajua namna walivyo, alianza kukimbia kwa nguvu wote watano waliobaki walikuwa wapo nyuma yake wanakuja kwa kasi ya ajabu, alisimama ghafla mbele yake kulikuwa na maporomoko makubwa na ya kutisha ambayo hayakuonekana hata yameishia wapi, alitoa damu mdomoni zaidi ya visu vidogo vitatu vingine vilikuwa vimezichana mbavu zake, hatua kumi kutoka hapo alipo kwa nyuma yake walisimama maninja wanne na mwanaume mwenye gwanda mmoja baada ya kujua hakuwa na sehemu ya kwenda, hakuhangaika hata kuwaangalia alijirusha huko chini ambako alikuwa anabeti maisha yake.
"He is not a human, he's completely a devil"
"But no survive, he is no more there"
"Let's go and take Donald's body"
Baada ya kumaliza mazungumzo yao kwa lugha ya kiingereza waliondoka hapo wakiwa kwenye tope zito ila kwao halikuwa na uzito wowote ule. Huyu mwanaume aliyekuwa anakimbizwa inasemekana alikuwa na miaka 10 ndani ya GEREZA na hakuwahi kutamka neno lolote lile mpaka siku anatoka ilikuwa ni lazima auawe kwa kufanya kosa la kutoroka kwenye gereza ambalo lilidumu kwa miaka 200 na hakuwahi kutoroka mwanadamu yeyote yule kwa aina ya ulinzi uliokuwepo na hakuna mfungwa hata mmoja ambaye alikuwa anajua wapi gereza hilo lipo, kuna binadamu leo yeye alikuwa nje ya GEREZA hili........what happens???? Nisikumalizie uhondo wako muda utaamua
Ni nini kilimpeleka gerezani? Hilo gereza liko wapi? Ni nani huyu binadamu hasa mpaka watu wamuandame sana kiasi hiki usiku wa manane na aliwezake kutoka huko? Je kwenye hayo maporomoko kuna kutoka kweli????????.......
GEREZA LA HAZWA.....na kalamu ya Bux the story teller