Unaukumbuka ugomvi wa Sunny Deol na Shah Rukh Khan?

Fakyuol

Senior Member
Nov 26, 2023
142
311
Yash Chopra (marehemu) alikuwa ni moja ya wafanya filamu wakubwa India. Director huyu mzito alifanya filamu nyingi nzuri kupitia kampuni yake, Yash Raj Films, ambayo imekuwa ikitoa filamu kubwa na maarufu nyingi.

Moja kati ya hizo filamu ni DARR (1993), ambayo ilikuwa na Sunny Deol, Sha Rukh Khan na Juhi Chawla. Ingawa Shah Rukh Khan alicheza kama adui wa filamu lakini watu walimpenda sana mhusika wake. kumbuka wakati filamu hii inatoka Sunny Deol alikuwa Yuko juu sana katika soko la filamu wakati Shah Rukh Khan alikuwa ndiyo anajipambania kutoka. Na filamu hii ndiyo ilikuwa ya kwanza kwa Shah Rukh Khan kufanya na Mzee Yash Chopra.

Filamu ya Darr ilikuwa na mafanikio makubwa katika mauzona kutangazwa kuwa blockbuster katika Box Office. Ingawa Sunny DEOL alikuwa ndiyo mhusika mkuu ambaye ni shujaa wa filamu alicheza kama mume anayewajibika katika ndoa, lakini uhusika wa Shah Rukh Khan ndiyo ulisifiwa na wakosoaji na watazamaji pia. Sunny Deol ndiyo aliyeumia ni Sunny Deol wakati nyota ya SRK ilipoanza kung'aa hapa, kwani baada ya hapa hakuongea na SRK kwa miaka 16.

Tatizo ni kwamba, Yash Chopra alimuhadi Sunny Deol nafasi kubwa mafanikio zaidi kwenye filamu hii lakini ilipotoka ilikuwa tofauti na maneno ya Yash Raj. Licha ya watu kusema Sunny na SRK walikuwa Wana nafasi sawa lakini Sunny aliona SRK alipendelewa.

Kwenye interview moja ya karibuni na The Hindustan Times, Sunny Deol aliongelea juu ya mafanikio ya filamu hii na vile hakuna kuwa watazamaji walimpenda mno adui wa filamu. Kwa maneno yake alisema:

"Mwisho wa siku, watu walinipenda Mimi kwenye filamu. Walimpenda SRK pia. Ishu ilikuwa Mimi binafsi sikujua kuwa watu wangeweza kumpenda mno adui."

Kwenye interview view hii, sunny Deol aliweka wazi vile alivyoangushwa na Yash Chopra na kusema hatofanya naye kazi tena. Sunny Deol aliongelea hilo akisema:

"Naamini katika kufanya kazi kwa uaminifu. Kwa bahati mbaya, tuna waigizaji na nyota wengi ambao hawaliwezi hili. Labda ndiyo namna wakipata umaarufu wao. Sitofanya kazi na Yash Chopra Tena. Huyu mtu hatimizi ahadi zake. Sina kumbukumbu zake nzuri, alisaliti Imani yangu kwake."

Sunny anasema wakati wakifanya filamu, alijaribu kumgusia Yash Chopra juu ya mwisho wa filamu hii. Alisema kuwa yeye kama shujaa wa filamu alicheza kama komando wa jeshi inawezekana vipi kupigana na kijana wa mtaani mwenye tamaa ya mapenzi tu bila ya ujuzi wa kupigana! Anaweza kumchoma kisu komando akiwa anamuangalia? Yash Chopra hakufanyia kazi hilo shauri lake, Sunny Deol alikasirika Hadi kufikia hatua ya kuchana suruali yake kwa hasira.

Filamu hii siyo tu ilimpa umaarufu mkubwa Shah Rukh Khan bali pia Ile namna alitamka "K-k-k-k-kiran" ni maarufu hadi leo huko India.

Wewe una maoni gani juu ya hii filamu?

#telebongo
Credit owner
 
Nimetamani kweli kuitafuta niitizame!

Vipi lakini humo hakuna masongi songi na kufia kwenye mauwa,maana kilichonishinda movie za kihindi ni huko kuimba imba na sterling kufia sehemu usiyoitarajia
 
Hii film niliona mwaka 1998 sterling alikuwa sun deol mke wake akawa mwana dada juwi chawla ....upande wa adui mnyama shah rukh khan ....

sasa filam ni ya dakika kama 150 yaani masaa mawili na nusu muda mwingi wa hii filam alikuwa akioneshwa zaidi shah rukh khan na mwanadada juwi.... wakati sun deo muda mwingi haoneshwi

Shah rukh khan alioneshwa katika romantic scenes nyingi kuliko sun deol.... ndo chanzo shah rukh khan kuwa villain and sterling wa movie kwa pamoja

Mimi sipend movie za kihindi ilia hii nzuri sana niliona mwaka 1998 huko iringa mafinga kwa tajir mmoja wa mbao
 
Back
Top Bottom