Gereza la Hazwa

SAKATA LA UCHAGUZI-PESA KWENYE DAMU (ELECTION SAGA-MONEY IN BLOOD)
INTRO...
Miaka mingi sana iliyokuwa imepita ikiwa ni miaka miwili kabla ya uchaguzi, serikali ya nchi ya Tanzania ilipokea taarifa mbaya kutoka kwa magaidi nchini Kongo kwamba raia wa Tanzania waishio huko wametekwa na ili kuwaachia serikali ilitakiwa kupeleka madini ya kutosha.

Sababu hiyo inamuibua waziri wa ulinzi ambaye anagoma kuhusu kupeleka madini hayo, ndipo anakutana na mkuu wa majeshi na wanakubaliana kukituma kikosi cha makomando SITA ambacho kiliitwa 6.0 (SIX POINT ZERO (hiyo zero iliwekwa kwa sababu maalumu, mwanzo ilikuwa ni 7.0). Makomando hao wanafika Kongo na kufanikiwa kuwaokoa mateka wote, wakawapandisha kwenye ndege huku wao wakiwa karibu na ziwa Tanganyika kusubiri usafiri kwani walikuwa wanafuatwa kupewa msaada ili kutoweka haraka kabla hawajashtukiwa.

Lakini huko Kongo kuna mizigo ambayo waliiokoa pamoja na mateka bila kujua ni mizigo ipi, baadae walikuja kugundua kwamba ni madini.Wakiwa wanajiuliza inakuwaje wanarudi na madini tena? Ndipo wanashangazwa na kinacho tokea.

Ndege ya raia wa Tanzania inatunguliwa ikiwa angani na kulipuka yote.....makomando hao wanashangazwa sana na hilo tukio na ndipo wanashtuka kwamba huenda huko walitumwa kufanya oparesheni nyingine na sio kuokoa watu, hapo wanayakumbuka madini ambayo walisisitizwa warudi nayo na kupewa onyo kwamba wasije wakaangalia ni mzigo gani. Wakiwa kwenye mshangao wa raia wao kulipuliwa wote ndipo msaada ambao ulikuwa umewafuata unafika walipo.

Wanaume ambao waliwafuata hapo hawakuwa kwa ajili ya kuwachukua bali kuwaua. Makomando hao wanakuja kushtuka ikiwa ni TOO LATE hivyo wanapigwa risasi vibaya sana miili yao ikibaki inaelea ziwani tu. Wauaji baada ya kuhakikiki kwamba wamemaliza kazi wanayabeba madini na kutoweka kuyapeleka kwa waheshimiwa walio toa amri ya kazi. Waheshimiwa wanatoa taarifa kwamba MAKOMANDO wamelidhalilisha taifa kwani badala ya kuokoa watu wao wameenda kuua raia wote wa Tanzania kisha wametoroka na madini hivyo wanatakiwa kusakwa popote pale duniani (WANAUME WANAUZIWA MSALA)

Kwa bahati mbaya sana mtoto mmoja wa kishua alikuwa ndani ya nchi ya Kongo kufanya utalii.....anafanikiwa kuuona mwili wa mtu ukielea majini hivyo akatoa amri walinzi wake wautoe na ndipo anagundua kwamba mtu huyo kwa mbali bado anahema, anaamua kuondoka naye na kwenda kwao UGIRIKI na mwili wa huyo komando mmoja ambaye anaitumia miaka miwili kitandani na baada ya kuja kuamka MATATIZO YANAANZIA HAPA. Wakubwa wakijua waliua wote lakini kwa bahati mbaya kuna kiumbe kiliishi. UMWAGAJI WA DAMU NDANI YA TAIFA LA TANZANIA UNAANZIA HAPA bila kujali kwamba ni damu za wenye hatia au wasio na hatia, nchi inachafuka na kuna mambo mabaya sana yanakuja kutokea. Hapa ndipo tunaanza kuzifunua kurasa hizi rasmi;

Baada ya miaka kumi na miwili kupita, Tanzania inapitia kwenye kipindi cha uchaguzi ambapo vigogo watatu wanaanza kuiwania nafasi hiyo kwa udi na Uvumba, wa kwanza alikuwa ni raisi mwenyewe (Huyu hakuna mtu aliyekuwa anamjua sura yake hata wananchi ambao alikuwa anawaongoza) utakuwa unajiuliza inakuwaje raisi aliye ongoza miaka 10 wananchi hawamjui?RELAX, wa pili alikuwa ni wa chama kimoja na raisi ambaye alitaka kumchallenge bosi wake na kutaka atoke Ikulu kwa lazima (huyu alikuja kususiwa IKULU, na alipokuja kugundua sababu ya kususiwa IKULU! Alikuwa amechelewa (TOO LATE).

Wa tatu alikuwa ndiye kipenzi cha Watanzania...huyu wananchi wote walihitaji aingie IKULU kwani walimpenda sana lakini siku chache kabla ya uchaguzi huyu anaye pendwa sana, mwanae mdogo anatekwa. Akiwa amepaniki asubuhi anapatiwa maiti ya mwanae ikiwa haina kichwa. ANACHANGANYIKIWA sana ila kabla hajapoa vizuri jioni mwanae mkubwa wa kike naye anapotea kwenye mazingira ya kutatanisha, anapagawa na kuamua kuibeba bastola yake kisha akaondoka nyumbani.

Alihitaji kwenda kuwabana wapinzani wake kwa kuhisi kwamba ndio ambao walihusika lakini aliishia kupigwa risasi nyingi sana na kupata koma na hapo ndipo simu inapigwa mpaka kwenye ardhi ya MALIKIA. Huko alikuwa anasoma mtoto wa kiume wa mzee huyo, lengo la kumpigia ilikuwa ni kumpa taarifa na kumtaka awe karibu na familia asije kuuawa.

Lakini kurudi kwake kunaibua mambo ya kutisha nchini, alidaiwa kuwa moja kati ya watu hatari sana na alikuwa na makubaliano ya kifo na shirika la kijasusi la MI6 Kwa siri sana ambapo alidaiwa kuhusika kukitengeneza kirusi kimoja hatari sana ambacho kiliishia kwenye mikono ya magaidi ikiwa ni siri ambayo aliishi nayo yeye tu maana familia ilimjua kama mtoto wa mama na hata vyombo vya usalama hivyo ujio wake unakuwa mwanzo mpya wa Tanzania nyingine ya kutisha kwa siri sana.

Unataka kujua kwamba kuna nini humu ndani? Basi ungana nami kwenye andiko hili la SAKATA LA UCHAGUZI-PESA KWENYE DAMU.

Simulizi hii ipo yote mpaka mwisho na unaweza kuipata kwa mfumo wa softcopy kwa bei ya shilingi 5000 tu za kitanzania.

5000 yako tu unapata burudani kubwa sana ya kusoma andiko bora sana hili la kipelelezi likiwa limejikita zaidi kwenye kuichambua SIASA na mambo yake ambayo yapo ndani.

Unaweza kufanya malipo kwa namba hizi.

0621567672
0745982347

Zote jina FEBIANI BABUYA.

Kwenye kalamu ni mimi FEBIANI BABUYA.

Chao


5cd1902acb2b45298e1a59afea1a415c.jpg


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
JIJI LA KAMALI ( GAMBLING CITY)

INTRO...........
Usiku wa kiza kinene ambacho kilikuwa kinasindikizwa na mvua ambazo hazikuwa na mpaka wa kuweza kuzielezea vyema, alionekana mwanaume mmoja akiwa ndani ya nguo zake nyeusi tii na begi jeusi usiku huo huku mwili wake ukiwa umefunikwa na koti kubwa jeusi pia ambalo lilikuwa refu kiasi kwamba lilivuka mpaka magotini.

Mikono yake ilifunikwa na gloves nzito nyeusi pia ambapo mkono wake wa kulia ndio ambao alikuwa ameutumia kuweza kushika begi lake mkononi akiwa anatembea kwa mwendo wa haraka sana huku akiwa makini mno kuonyesha wazi kwamba alikuwa anatakiwa kulifikisha begi hilo salama kabisa sehemu ambapo lilikuwa linahitajika kuweza kufika.

Akiwa kwenye mwendo wake huo wa haraka, wakati amefika katikati ya barabara ndogo ambayo ilikuwa imezungukwa na majengo marefu sana na pembeni yake kukiwa na vichochoro vingi, alihisi kwamba eneo hilo ni kama lilikuwa na mtu au watu wengine ukiacha yeye hivyo alizidisha hali ya umakini sana kwa hapo ambapo alikuwa amesimama.

Masikio yake yalimtekenya vizuri mithili ya funguo zinapokuwa zinazamishwa kwenye kufuli na kumpa taarifa hiyo, alikuwa ni mtu wa kuutumia sana mlango wake wa sita wa fahamu huo wa hisia hivyo alikuwa na uhakika kwamba hisia zake zisingeweza kumsaliti kamwe kwani alikuwa akijiamini sana kwenye jambo hilo hivyo akawa na uhakika kwamba kulikuwa na ugeni ndani ya hilo eneo.

Alisimama na kutulia ili kuweza kujua kwamba huyo mgeni alikuwa anatokea upande upi huku akiwa ameyafumba macho yake kuweza kujipa hali ya utulivu zaidi kwenye masikio yake. Akiwa bado amesimama hapo alihisi kama kuna kitu kilikuwa kinakuja kwa kasi sana sehemu ambayo alikuwa amesimama hivyo aliinama kwa kasi mno mithili ya radi ya mvua.

Wakati anainama alipishana na shoka ambalo lilienda kukita kwenye ukuta mmoja wa jengo la pembeni. Aligeuka haraka sana ila wakati anageuka alitumia muda mrefu ambao ulimpa nafasi mtu ambaye alikuwa ameingia hapo kufanya kile ambacho alikuwa anakitaka.

Alihisi kifua kinamuwasha mithili ya mtu aliye tafuna pilipili kichaa maana spidi ambayo mvamizi aliitumia kumkita hapo kifuani haikuwa ya binadamu mwenye mifupa ya kawaida bali alikuwa ni mashine haswa kama namna umeme unavyo safari kwenye zile njia zake. Alipokea mishindo ya haraka na mabuti makali na kumfanya begi kumtoka mkononi huku ikionekana wazi kwamba mabuti hayo yalitokea kwa mtu ambaye alidhamiria kabisa kumuua ndiyo maana hakumpa hata nafasi ya kuweza kumtazama maana mvamizi huyo uso wake ulifunikwa kwa kitambaa cheusi na hata mvamiwaji hakupata hiyo nafasi ya kumtazama kwa ukaribu.

Mwanaume huyo licha ya kurushwa mbali na mabuti hayo hali ambayo ingemfanya auvunje mgongo wake kwa kujibamiza kwenye kuta za mawe mazito za majengo ambayo yalikuwa pembeni, hakuwa fala kufa kijinga namna hiyo. Mkono wake ndio ambao aliutumia kukita kwenye kuta hizo na sio mgongo ambao ulitua ukutani kwa nguvu sana.

Kasi ambayo alitua nayo kwa mkono wake ililifanya koti lake kujivuta kidogo na kwenye mkono wake ikaonekana alama ya tatoo (tatuu) ambayo ilisomeka kama 001. Baada ya kujichomoa hapo ndipo aligeuka na kumuangalia mtu ambaye alionekana alihitaji kumuua, mtu huyo alikuwa kwenye mavazi meusi kama yeye na koti kama lake, yaani kiufupi wote walikuwa wamevaa sawa ila utofauti wao ni kwamba mvamiwaji alivaa kofia aina ya pama kichwani ila mvamiaji alikuwa amejifunika tu kitambaa kwenye uso wake hivyo sura yake haikuwa ikionekana kabisa.

Baada ya hapo ulipigwa mkono wa hatari mno mpaka umeme ulipo katika ghafla sana ndipo mvamiwaji alitulia akiwa makini sana maana hakuwa akimuona mtu ambaye alitakiwa kumshambulia huku akiwa amepigwa vibaya sana na umeme huo kukatika alishukuru sana japo ilikuwa ni hatari maana angeweza kuuawa bila kujua mhusika yuko wapi ila aliamini kwamba angepata dakika chache za kupumzika maana bila hivyo ni lazima angekufa.

Akiwa anaangaza kwa umakini huku na huko umeme ulirudi tena ghafla sana na ndipo alipo gundua kwamba ndani ya eneo hilo hapakuwa na mtu mwingine zaidi yake, mvamizi alikuwa ameondoka muda mrefu sana ila chini palikuwa na karatasi nyeupe ambayo ilikuwa imesainiwa kwa damu huku ikiendelea kunyeshewa na mvua.

Aligeuka na kuangalia pale ambapo begi lilikuwa limedondokea ili kujua usalama wake ila kwa bahati mbaya sana begi halikuwepo kabisa eneo hilo, alishtuka sana akionyesha hofu ya wazi moyoni na kwenye uso wake hivyo hakuwa na namna zaidi ya kuisogelea ile karatasi ili aweze kusoma kile ambacho kilikuwa kimeandikwa.

“KAMALI YANGU YA MWISHO, NDIYO KAMALI YAKO YA KWANZA” hayo ndiyo maneno ambayo yalikuwa yameandikwa hapo. Aliogopa sana baada ya kuisoma huku akionekana wazi kwamba mikono yake ilikuwa inatetemeka wakati huo. Hiyo ilikuwa ni kauli ambayo alikuwa anaitumia mwanaume mmoja ambaye alimuua yeye mwenyewe kwa mkono wake miaka kadhaa ambayo ilikuwa imepita huko nyuma, huku begi ambalo lilionekana kuwa na nyaraka mhimu mno likiwa limepotea kizembe sana.

Inawezekanaje mwanaume ambaye alimuua kwa mkono wake mwenyewe bado awe hai? Hilo begi lina nini mpaka mtu ambaye alisemekana kwamba alikufa aweze kupotea nalo? Nini maana halisi ya JIJI LA KAMALI na jiji hilo lina mambo yapi na siri zipi labda?

Unategemea kukutana na nini humu ndani? Mimi nashika kalamu yangu sasa nakaa mezani, kazi yako wewe ni kuhakikisha unaenda nayo nukta kwa nukta ili uweze kuifunua kila kurasa kuweza kuzisoma serikali tatu kwa wakati mmoja ndani ya JIJI LA KAMALI.

Simulizi hii inasomwa kwenye group la WhatsApp tu pekee na haitapostiwa mahali pengine popote hivyo nicheki haraka nikuunge kwenye group langu la WhatsApp uanze kusoma simulizi hatari sana ya watu wenye jiji lao la KAMALI (ni hatari sana).

Kujiunga bei yake ni shilingi 3000 tu, yaani ukilipia 3000 nakuunga kwenye group haraka sana.

Usikae kinyonge wakati naingia kujifungia ili ufurahi na kwenda kuisherehekea vyema likizo yako ndefu. Maandishi yapo yanakusubiri wewe tu, usijibane ukataka kukosa simulizi hii bora ya kusisimua eti kisa 3000 tu.

Lipia kupitia namba

0621567672 ( WhatsApp)

0745982347

Zote FEBIANI BABUYA

Nataka watu 30 tu wa mwanzo nianze nao haraka sana, unaweza kuwahi kabla nafasi hazijajaa ili usije ukaikosa

Niwatakieni asubuhi njema.

Kalamu ni yangu mwenyewe;

FEBIANI BABUYA.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)-Simulizi mpya na bora sana ya kipelelezi/kijasusi imetoka rasmi kwa mfumo wa softcopy (nakala laini)

Hii ni moja kati ya movie bora sana iliyopo kwenye maandishi ambayo utaisoma mwaka huu....Kuna mwanaume alipigwa zaidi ya risasi sita kwenye mwili wake kisha akaenda kuzikwa akiwa hai.......Alizikwa porini ambako hakukuwa na binadamu yeyote yule anayeishi LAKINI cha kushangaza mwanaume huyo alikutwa anaishi na yupo hai miaka kumi na mbili iliyo fuatia baadae.....Walichanganyikiwa na ndipo alitumwa BEAST mmoja kwenda kumtafuta ili kujua mtu aliyezikwa anakutwa vipi mtaani! Ni bonge moja la simulizi NICHEKI UJIPATIE NAKALA YAKO LAINI uendelee kufurahi.....

Softcopy yake inapatikana kwa shilingi 5000 tu.

Nicheki WhatsApp kwa namba 0621567672 uweze kuipata yako.

Kama unalipia namba za malipo ni hizi hapa

0621567672

0745982347

FEBIANI BABUYA.

Karibu tuyafurahie maandishi, ndipo chanzo kikubwa cha akili na maarifa kilipo jificha.
FB_IMG_1701864748679.jpg


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Jaman kama kuna mtu ana hii story ya gereza la hazwa naomba kuanzia sehemu ya 60mpaka final anisaidie
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom