Gereza la Hazwa

STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller

UKURASA WA TISA

TULIPO ISHIA UKURASA WA NANE

“Nahitaji kuijua historia yake yote kwa sababu kwa mara ya mwisho uliniahidi kwamba kama siku nikimpata akiwa hai basi utanipatia historia nzima ya maisha yake ndio maana leo nipo hapa” maneno ya raisi yalimfanya mzee huyo amwangalie sana kisha akafuta futa mauchafu ambayo yalikuwa kwenye mdomo wake akakohoa kidogo ili kuanza kumfahamisha raisi huyo ambaye alionekana kudandia gari kwa mbele bila hata kuijua spidi yake.

ENDELEA......................

Kibo Tanzania
Mita 1000 kutoka kilipo kituo kikubwa cha mwendokasi ambacho kinajulikana kama Kibo ndani ya nyumba moja ya kawaida usiku wa manane sebuleni walikuwa wamelala wanawake wawili ambao wote walikuwa wapo hovyo hovyo tu ikionyesha hapo walikuwa wamekunywa kupita kiasi chini kabisa kukiwa na vipisi vya sigara ni wazi walikuwa walevi wa kupindukia. Ni nguo za ndani tu ndizo ziliwafanya waonekane wana nguo mwilini ikionekana shughuli iliyokuwa hapo kwa muda mchache ambao ulipita haikuwa ya kitoto. Nyumba hiyo ndogo ilikuwa na ngazi za kupanda juu ni wazi ilikuwa ya ghorofa moja ndogo upande wa ndani wa chumba hicho cha juu walikuwa wamekumbatiana mwanaume mmoja na mwanamke mmoja pembeni yao kukiwa na chupa nyingi sana za pombe ghali ulevi lazima ulichukua nafasi yake kabla ya watu hao kupitiwa na usingizi.

Wote walikuwa wapo uchi kabisa wa mnyama baada ya kuzichosha nyeti zao ndipo walipo lala, mwanaume huyo alionekana wazi alikuwa ni mwarabu kwa mwonekano wake hakuwa mtanzania kabisa naye alikuwa kwenye usingizi mzito mno, simu iliita kwa fujo hali ambalo ilimfanya mwanaume huyo anyanyuke kwa spidi ya ajabu kutoka usingizini akiwa uchi, miguu yake ilinyooshwa kwa nguvu mwili ukajiviringisha akaenda kudunda ukutani na kujibana kwenye kona mpaka alipo ona hakuna tatizo ilikuwa ni sauti ya simu tu aliibutua kwa mguu haraka ikaja kwenye mkono wake hakutaka kuwaamsha wanawake hawa ndiyo sababu aliidaka kwa wepesi sana. Aliibeba na kwenda kujifungia chooni kuongea na simu hiyo ambayo ilikuwa ya mhimu sana mpaka kupigiwa usiku wa manane namna hiyo.

“Hello big boss”

“Ni lini utaacha kulala na wanawake hovyo” sauti nzito ilisikika upande wa pili

“Bosi umejuaje?”

“Mimi ni mzoefu sana na hivi vitu mtu akiwa amelala kawaida sauti yake tu najua ila kwa wewe hapo unaongea kwa kuhemeana sana na unaonekana unajibanza usisikike unadhani kinaweza kuwa nini kama sio wanawake?”

“Nisamehe sana bosi lakini nilikwambia kwamba mimi siwezi kuishi bila kufanya mapenzi na wanawake”

“Kujiendekeza kipuuzi hivyo na hao hao ndio watakao kuua siku moja”

“Nisamehe sana kiongozi”

“Umempata”

“Hapana”

“Umefikia wapi?”

“Ni muda mrefu sana hakukuwa na taarifa zake sehemu yoyote ile juzi kuna mtu aliposti picha akiwa naye ila kwa sekunde kadhaa tu picha hizo zilifutwa na kutolewa kabisa kwenye mitandao, nilijaribu kufuatilia sana lakini hakukuwa na ishara yoyote ile ila inaonekana kwamba ni idara ya usalama wa nchi ya Libya ndo ilihusika na kuzifuta hizo picha japo mpaka sasa hakuna kithibiti kamili juu ya hili jambo. Nilianza kufuatilia kwa umakini kuhusu hili jambo mpaka nilipokuja kugundua sehemu ambayo alikuwa anaishi, alikuwa na mke mmoja na mtoto kama ulivyo niambia kwamba kila mtu anaye mhusu basi anatakiwa kufa haraka sana nilimteka huyo mwanamke na kumtishia aniambie mumewe yuko wapi alikata kabisa basi nilicho kifanya nilimbaka kisha nikamchinja yeye na mtoto wake baadae nikawatupa hadharani kwa kutegemea kwamba kama akisikia vifo vya hiyo familia yake basi lazima angejitokeza hadharani hapo ndipo ingekuwa nafasi yetu kuweza kumkamata” maelezo yake yalihitimishwa na ukimya mzito kutoka upande wa pili ni wazi mtu huyo alionekana kuingia kwenye mawazo mazito sana.

“Qader the same mistake ilifanyika nadhani nilikwambia kitu ambacho alikuja kukifanya mtu huyo siyo wa kumchukulia masiara sana kwa taarifa nilizo zipata kuhusu yeye nahitaji afe haraka sana kwenye mikono yangu mwenyewe, kama ukipata dalili za uwepo wake niambie haraka kuna watu nimewatuma wapo huko huko Tanzania wenye uwezo zaidi yake watakuja kumchukua huyo lazima ahukumiwe kwenye mikono yangu mimi mwenyewe na sio mtu mwingine yeyote yule sitaruhusu kitu kama hicho kiweze kutokea nikiwa bado mzima wa afya huyo mjinga ameniletea maumivu makali sana kwenye maisha yangu ni lazima aweze kulipia hicho kitu” sauti upande wa pili iliongea kwa msisitizo mno kisha simu ikakatwa.

“Nimekuelewa bosi” alikuja kushtuka baada ya kugundua kwamba simu ilikuwa imekatwa kwa muda mrefu sana. alitulia na kuhema kwa nguvu alitaka kutoka ndani ya hicho choo alisita baada ya sikio lake la upande wa kulia kucheza cheza, aliinyanyua simu yake na kubonyeza mara mbili tu ilitokea ramani nzima ya hiyo nyumba ikiwa na video pembeni alibonyeza video hiyo alianza kuona kila kilichokuwa kinaendelea ndani ya hiyo nyumba alitabasamu baada ya kuona vivuli kadhaa vikizunguka kwenye geti dogo la hiyo nyumba alichukua bisi bisi moja na koti akalivaa kisha akatokea mlango wa nyuma na kwenda kukaa karibu na sehemu ambayo ilikuwa na gari.

“Ni usiku sana saivi kwenye nyumba za watu mnatafuta nini bila taarifa za msingi?” aliuliza baada ya kuwabananisha wanaume watatu wakiwa wanahangaika kufungua mlango wa kuingilia ndani wote walikuwa na mapanga mikononi mwao.

“Tuna shida na milioni hamsini za kitanzania haraka kabla hatujakufanyia kitu kibaya” aliongea mmoja wao shida yao ilikuwa ni pesa tu.

“Mhhhhhh ni hiyo pesa tu ndo mmenijia na mapanga kwamba mnahitaji kuniua moja kwa moja au?”

“Ikitokea hujatoa hiyo pesa basi lazima ufe hapa hapa moja kwa moja” alidondoka chini mmoja bisi bisi ilizama kwenye shingo yake mwanaume huyo alikuwa anakimbia ni suala ambalo lilihitaji kujiuliza kwamba anakimbiaje mpaka anawahi kufika sana namna hiyo, aliivutia bisi bisi hiyo upande wa pili wa shingo ya kijana huyo. Wenzake walishangaa walijua wamekuja kumvamia mtu mrembo hawakuelewa aina ya maisha ambayo alikuwa anayaishi, wapili alihesabiwa sekunde mbili tu kichwa chake kilitobolewa mara nne na kuchorwa alama ya msalaba.

“Shiiiiiiiiiiii” mmoja aliyekuwa amebaki alitaka kupiga makelele alizuiliwa na mwanaume huyo akae kwa kutulia hayo mambo waliyataka wenyewe wakati huo alikuwa akitetemeka miguu yote alishuhudia wenzake wote wakiuliwa kwa sekunde chache mno sasa alibaki yeye mwenyewe.

“Kawatuma nani mje hapa?”

“Hakuna mtu tuliona tu una begi la pesa pale Mikasa Lounge unavyo ondoka na wale wanawake watatu ndiyo maana tukaamua kukufuatilia mpaka tulipojua unapo kaa ndio tukawa tumepanga kuja kuzichukua pesa zile”

“Unajua hizo pesa zimepatikana vipi”

“Hapana”

“Napenda wanaume wapambanaji kwama wewe kwa kuutafuta mkate wa kila siku iwe ni kwa njia yoyote ile kikubwa mfuko ujae ila babati mbaya sana umeingia sehemu ambayo siyo” maneno yake yalimalizwa na teke la singo ambalo liliivunja shingo ya kijana huyo mara moja tu, hakutaka kupoteza muda mbele yao baada ya kugundua kwamba kumbe walikuwa ni vibaka wa kawaida tu na sio watu wa hatari kama yeye alivyokuwa akidhania mwanzo. Akiwa amesimama hapo akiwakagua kagua vijana hao waliingia wanaume sita wenye suti mmoja wao alienda kumfuta huyo mwarabu aliye julikana kama Qader kwa damu ambazo zilimrukia wakati anafanya mauaji baada ya kumaliza kumfuta waliibeba miili ya hao vijana watatu na kuondoka nayo mwanaume alijiweka sawa na kuingia ndani kama hakuna kitu kilicho fanyika.

Bado ulikuwa ni usiku wa manane alienda mpaka sebuleni na kupitiliza kwenye friji alitoa pombe kali na barafu moja ambayo aliiweka ndani ya pombe hiyo na kuigida yote kwenye glasi alihisi mwili wake umekuwa vyema sana, aligeuka kwenye masofa pale ambapo walikuwa wamelala wale watoto kike wawili wakiwa na nguo za ndani tu pepo la ngono lilimpanda kwa kasi alienda na kuwavua nguo zao za ndani wote wawili na kumuinua mmoja kisha akamuinamisha na kupachika mpini wake utamu ulio pitiliza ndio ulio muamusha mwanamke huyo ambaye alianza kutoa ushirikiano kwa miguno mikali iliyo mwamsha na mwenzie ambaye naye alihitaji huduma aipate kwa muda, mwanaume hakuwa mchoyo kwenye utoaji aliwatolea wote wawili uvivu kwa raha zake wakichoka walikuwa wakiongeza pombe walijikuta wanafanya kwa muda mrefu sana bila kuweza kuchoka wala kupumzika.

HAZWA
“Huwa sipendi mtu mwenye kichwa kigumu sana na huwa sipendi kuulizwa ulizwa maswali pale ninapokuwa naongea kazi yako kubwa ni kuyatega kwa umakini masikio yako leo naenda kukupatia hadithi ya hilo dumbwana kwa kuanzia asili na chimbuko lake mpaka yeye mwenyewe, kuna visa viwili tofauti tofauti hapa kwahiyo unapaswa uwe mtulivu ili unielewe” alijikohoza kidogo mzee huyu ambaye wengi walimtambua kama kichaa kisha akaendelea.

“Miaka mingi sana iliyoweza kupita ndani ya mji wa Tripoli alizaliwa mtoto mdogo wa kiume kwenye moja ya familia ambazo zilikuwa na ukwasi mkubwa sana kwa kumiliki visima vingi vya mafuta ambavyo mpaka leo vipo chini ya jina la hiyo familia, mtoto huyo kutokana na hali ya hewa ya ujangwa ndani ya nchi hii ilionekana kumkataa hivyo baba yake aliamua kumsafirisha mkewe na mtoto kumpeleka katika mji wa Antananarivo huko Madagaska ambacho kwa wana mahesabu huwa kinahesabika kuwa kisiwa cha tano kwa ukubwa duniani kikiwa na ekari za mraba milioni 144 huko pia huwa kuna ujangwa kwa muda flani lakini ndiyo sehemu ambayo mke wa huyo baba mwenye mtoto alichagua kwenda kwa sababu alikuwa akipenda sana maeneo ya visiwani, basi huyo mama akawa anakuja Libya kama mgeni mara moja moja kusalimia na kuondoka. Baadae alikuja kurudi moja kwa moja baada ya mtoto huyo wa pekee kuanza masomo yake akiwa amekuwa na umri mkubwa hivyo hakuwa mtu wa kukaa kwa sababu alisoma sana ndani ya bara la ulaya huko ambako hali ya hewa ilionekana kumkubali moja kwa moja hivyo mama yake hakuwa na sababu ya kubaki mwenyewe kule Madagascar akaamua kurudi nyumbani kwake na kwao pia Libya.

Hiyo ilikuwa familia ya mzee Mansour the Seniour, mtoto huyo alikuwa mwerevu na mwenye akili nyingi sana akitegemewa kuja kuichukua mikoba ya baba yake mzazi ambaye alikuwa anatarajia kumpatia robo tatu ya miliki zake zote mtoto huyo pindi atakapokuwa mkubwa na kumaliza masomo yake yote.

BUKOBA TANZANIA
Kwenye nchi ambayo inasifika zaidi kwa amani duniani huko wamebarikiwa sana utajiri wa mali kwenye nchi hiyo lakini pia amani ndicho kipaumbele chao kikubwa ila tofauti sana na ukienda kwenye ardhi ya Bukoba huko mkoani Kagera, ni hadithi zilizo andikwa namimi niliwahi kwenda mara moja huko ni watu ambao wanajikubali sana na kujiamini mno, ni haki yao kufanya hivyo kwa sababu wale jamaa ni wasomi sana na wana pesa isiyo ya kawaida. Wenyewe kipaumbele chao kikubwa huwa ni elimu kosa vyote uwe na shule kichwani watakuheshimu sana na sio elimu ya kubahatisha unatakiwa kuwa na elimu ambayo unaweza kusimama popote pale na ukajivuna kwamba wewe ni msomi vinginevyo basi hakikisha una pesa nyingi sana za kutosha inaweza kuwa msaada kwako kusikilizwa wanafahamika kama kabila la wahaya yes hao ndiyo wahaya.

Huko kuna familia moja ya mzee mmoja wa makamo ya kawaida tu aliyejulikana kwa jina la Philebert alikuwa amebahatika kupata watoto wa kiume wanne kwa umri wake wote alitamani sana kupata mtoto wa kike lakini MUNGU alikuwa anaonyesha njia yake kwa watoto wa kiume tu ilifika hatua akawa amekata kabisa tamaa ya kupata mtoto wa kike lakini MUNGU hajawahi kumtupa mja wake kama tu atakuwa ameamua kukivumilia hicho anacho kifanya, kwenye mpira huwa wanaita dakika ya tisini ila kwa mvumilivu huwa inaitwa amekula mbivu familia hiyo ilibahatika kupata mtoto wa kike mzuri sana na pekee, binti huyo ni kama ilikuwa neema kubwa ya hiyo familia kwa sababu alifanya familia ikawa na furaha ambayo mtu wa kawaida asingeweza kabisa kuielezea mbele ya uso wa mwanadamu mwenzie, mzee huyo aliandaa moja ya sherehe kubwa mno kuweza kumlaki bintiye wa pekee ambaye alimuita jina la Sekelaga likiwa na maana ya kufurahi au sifa kwa zawadi hiyo ambayo waliipata.

Huyo mtoto wa kike alilelewa kama yai na kwa uwezo mkubwa wa familia hiyo ulifanya aanze kupelekwa shule za gharama sana akiwa binti mdogo mno, maisha yake yaliendelea mpaka pale alipo maliza masomo yake ya kidato cha nne ambapo alipelekwa India katika jiji la Mumbai baada ya kumaliza huko baadaye baba yake alimfanyia mpango wa kwenda ndani ya chuo kikubwa sana duniani ambacho kinapatikana katika taifa kubwa la Uingereza kiitwacho OXFORD UNIVERSITY.

Usipagawe sana bado tupo ndani ya HAZWA mzee ambaye wengi walimjua kama kichaa akimpatia historia na chimbuko la kijana mdogo ambaye wengi wanao mfahamu wanamuogopa sana kuliko kitu chochote kile kwenye maisha yao.

Hawa watu ambao historia zao mbili zinazochanganywa ni akina nani? na wanaingiaje kwenye mkasa huu?.......GEREZA LA HAZWA sehemu ya tisa natia nanga tukutane tena wakati ujao………bye bye.

Bux the story teller.View attachment 2411348

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller

UKURASA WA KUMI

TULIPO ISHIA UKURASA WA TISA

Huyo mtoto wa kike alilelewa kama yai na kwa uwezo mkubwa wa familia hiyo ulifanya aanze kupelekwa shule za gharama sana akiwa binti mdogo mno, maisha yake yaliendelea mpaka pale alipo maliza masomo yake ya kidato cha nne ambapo alipelekwa India katika jiji la Mumbai baada ya kumaliza huko baadaye baba yake alimfanyia mpango wa kwenda ndani ya chuo kikubwa sana duniani ambacho kinapatikana katika taifa kubwa la Uingereza kiitwacho OXFORD UNIVERSITY.

ENDELEA...........................

OXFORD UNIVERSITY

Hapa ndipo ilipo zaliwa historia ya hicho kiumbe kwa mara ya kwanza kwenye huu ulimwengu. Ni jioni moja wakati Mansour Omran ambaye mara nyingi walikuwa wakipenda kumuita the second kutokana na baba yake kuwa the senior akiwa kama yeye ndiye wa pili baada ya baba yake alikuwa akiingia kwenye maktaba ya vitabu kwa ajili ya kujisomea ndani ya chuo kikuu bora sana hicho, alikuwa akijongea bila wasiwasi wowote kusogea sehemu ambayo ilikuwa imemvutia sana yeye kuwepo hapo kwa pembeni kidogo alishuhudia watu wawili wakiwa wanazozana kilicho mvutia kuweza kusogea kusikiliza yale maongezi pale sio kwa sababu alikuwa anapenda kuingilia habari za watu hapana ila katika kuishi kwake sana ulaya alikuwa amejifunza kuongea lugha nyingi sana, aliona mwanamke mmoja mwenye asili ya kiafrika akiwa anazozana na mjapan mmoja ambaye alimpamia ila tatizo likawa lugha mjapan alikuwa hajui kiingereza na mwanamke huyo alikuwa anazungumza kiingereza hivyo wakawa hawaelewani kabisa kwenye suala la lugha.

Mansour alisogea pale na kwenda kuanza kuwatafsiria kile ambacho walikuwa wakizozana baadaye sana wakaja kuelewana wale watu wakaombana na msamaha yeye akiwa mkalimani wao basi amani ilitawala. Mjapan aliweza kuondoka lakini yeye na yule mwanamke walibaki wakiongea baada ya kujuana kwamba wote walikuwa wanatokea ndani ya bara la Afrika hivyo wakiwa ugenini kule wanakuwa kama ndugu na kitu kimoja. Hiyo ndiyo ilikuwa siku ya kwanza kukutana kwenye maisha yao ila waliweza kuutengeneza urafiki mkubwa sana hasa baada ya kugundua kwamba wote walikuwa wanasomea kitu kimoja kwa pamoja MASTERS OF BUSINESS ADMISTRATION (MBA) ilikuwa ni furaha sana kwa upande wao wote wawili.

“Ni muda sasa tangu tumejuana sijawahi kuwa karibu na mwanamke kabla ya hapa, nimejihisi mwenye furaha na kupata tumaini jipya la kuendelea kuwa hai najikuta sitamani kuipoteza hata dakika moja ya kuweza kuishi nawewe nahisi nakupenda miss Philebert” mwanaume aliongea taratibu tena kwa mujibu huku akitokwa na machozi ni wazi alikuwa amekolea sana kwa mtoto wa kike na usingeweza kumtoa kirahisi wala kiwepesi mtoto wa kishua huyu na msomi mzuri tu.

“Hey sorry unaniacha kidogo hapo unasimulia ni stori ya nani unaniachanganya” mheshimiwa Malek Salem raisi huyu wa nchi ya Libya aliuliza wakiwa wameketi kwenye hicho chumba cha gereza akipewa historia nzima ya kijana Alen.

“Nimekwambia tangu mwanzo huwa sipendi watu wenye vichwa vigumu ninapo ongea nawachukia sana watu wa aina yako kunifanya nirudie rudie kitu kimoja, inanisikitisha sana wewe ndiye raisi wa nchi kuanzia leo ebu achana na michezo ya kupiga punyeto inaonekana imekuathiri sana imefika sehemu una uwezo mdogo mno wa kufikiri sasa nakuachia ujisimulie wewe mwenyewe na toka kwenye hiki chumba mpuuzi wewe” mzee huyu alionyesha kuchukizwa sana kitendo cha yeye kukatishwa alichokuwa anakifanya mtu aliyekuwa anamfokea kiasi hicho usingeweza kuamini kwamba alikuwa ni raisi wa nchi, Malek ilimuuma sana mtu wa kawaida huyo kumfokea kiasi hicho ila aliamua kuwa mpole na kulihifadhi jambo hilo moyoni kwa muda ili aweze kujua kile ambacho alikuwa ana hamu nacho kuweza kukijua. Hakuuliza alitoka humo ndani akiwa anakimbia mpaka walinzi wake walibaki wanamshangaa, alimfuata mlinzi wake mmoja na kukwapua koti ambalo alikuwa amempatia wakati anaingia aliingiza ndani ya mfuko akatoka na sigara ya bei ghali pamoja na kiberiti kisha akarudi ndani ya kile chumba na kumrushia mzee huyo ambaye alionekaan kuchekelea sana kitu hicho.

“Kidogo saivi umeanza kuwa mwelewa hakikisha hauulizi ulizi tena kijinga nikiwa naendelea kuongea” alionekana kuchekelea kwa zawadi ambayo alipewa ya sigara hiyo aliuvuta moshi kwa nguvu na kumfanya ajihisi yupo dunia yake mwenyewe.

“Hivi uko siriasi na unacho kiongea hapa?” ilikuwa ni sauti ambayo bila shaka bwana Mansour hakuwa akihitaji kabisa kukosa kuisikia kwenye maisha yake ilitoka kwa mrembo Sekelaga.

“Nimekuwa mpweke kwa miaka mingi ujio wako kwenye maisha yangu ni kama tone moja la maji ambalo lilihitajika kuweza kuuokoa uhai wangu ndani ya jangwa la kutisha, siwezi kusema mimi ni bora sana ila natamani niwe mwanaume bora kwa ajili ya maisha yako namaanisha sana ninacho kiongea nakupenda sana” mwanaume alizidi kufunguka na kuupanga mdomo wake uyatamke yale ambayo yalifichwa kwenye uvungu wa moyo wake mwanamke huyo alikimbia na kwenda kumkumbatia mwanaume huyo kwa mara ya kwanza kwenye maisha yao waliweza kuikutanisha midomo yao shahidi akiwa ni kope za macho yao ambazo zilikuwa zinajifunika na kujifunua kila walipo karibiana zaidi. Ule ulikuwa ni usiku bora sana kwenye maisha yao waliamua rasmi kuivunja amri ya sita kwa huba lenye kina kirefu sana cha bahari, ni siku ambayo kila mmoja wao alikiri kwamba asingeweza kuishi bila mwenzake, ni siku ambayo iliandikwa historia mpya ya wapenzi wawili ambao waliamua kufundishana mapenzi wenyewe kutoka kwenye ushamba mpaka kuwa mfano bora kwa wapenzi wengine ambao walikuwa wakiwazunguka ila ndiyo ndiyo ile siku ambayo iliyaleta haya yote ambayo yanatokea kwa sasa.

Walipendana sana tena sana zaidi ya sana, neno mapenzi ni herufi ambazo ziliufanya ulimwengu wao kuwa wenye madini mengi na wachimbaji hao wawili wasingekubali kabisa kuweza kuyapoteza hayo ndiyo yalikuwa maisha yao halisia kabisa. Mungu huwa sio mwanadamu kama ilivyo siku zote watu hawa wawili waliyamaliza masomo yao huko shida ikawa kwenye kuondoka na kurudi nyumbani kwako, mmoja alipaswa kurudi Libya na mwingine alipaswa kurudi Tanzania ndani ya ardhi ya wahaya, je wangefanyaje na wanapendana sana? maamuzi waliyo yafanya ni kuzitaarifu familia zao kwamba wao wanahitaji kuoana. Kwa mwanaume halikuwa tatizo kubwa kwa sababu walikuwa wanahitaji afurahi akiwa ndiye mtoto wa pekee lakini ilikuwa ni tofauti na kwa mwanamke ambaye familia ilikuwa tayari imeandaa mtu wa kumuoa na binti huyo alisema kwamba hawezi kufanya hicho kitu kwani tayari ana mtu ambaye anampenda.

Familia ni mhimu sana ila mapenzi yana nguvu sana mwanamke yule aliamua kuondoka na kwenda Libya ambako aliolewa moja kwa moja na Mansour bila hata baraka za wazazi wake kikubwa aliizingatia sana furaha yake. Tangu anatoka kwenye chuo cha OXFORD mwanamke huyo Sekelaga alikuwa tayari amepata ujauzito inasemekana siku ile ya kwanza kukutana kimwili na bwana Mansour ndiyo ilizaa hayo mattunda, ilipita miezi miwili tu tangu aolewe aliweza kujifungua mtoto wa kiume ambaye ndiye rasmi alipewa jina la Zakaria Mansour (Juniour), tangu kujifungua kwake Sekelaga afya yake ilikuwa imeanza kudhorota sana kitu kilicho pelekea kifo chake baada ya miezi nane tu kupita hivyo bwana mdogo akawa amempoteza mama yake akiwa bado ni kijana mdogo hata hajamaliza muda wake wa kuweza kuyanyonya maziwa ya mama yake.

Iliwalazimu kupeleka taarifa zao kwa wazazi wa Sekelaga lakini walikataa kabisa kuhusu hilo jambo na waliwafukuza kabisa familia ya Mansour kwa sababu walidai binti yao aliwakataa hivyo hawana taarifa kama ni binti yao basi familia hiyo ilirudi nyumbani kwao Libya kwa masikitiko makubwa sana sasa jukumu la kumlea mtoto lilibaki kwa bwana Monsour Omran, alijitahidi sana kuwa baba bora lakini kazi ya malezi inamhitaji sana mwanamke kuliko mwanaume kwa sababu wanaume wana mambo mengi mno ndiyo sababu ya msingi huwa inapelekea watoto wengi wanampenda sana mama kuliko hata baba kwani mama huwa karibu zaidi na watoto kuliko baba. Hiyo ilipelekea mgongano mkubwa sana kwenye familia hiyo ya kitajiri wakimsihi aweze kuoa mwanamke mwingine ambaye atamsaidia kumtunzia mtoto wake huyo kwa sababu wazazi wake umri ulikuwa umeenda ilikuwa ni ngumu sana kumlea mtoto wakati yeye akiwa anasimamia biashara zote za familia ila kwake kilikuwa ni kitu ambacho kisingewezekana kabisa kwa sababu alijiwekea nadhiri ya kumpenda mwanamke huyo tu na sio kuoa mtu mwingine maana yake kama amekufa basi alikuwa tayari kuweza kuishi yeye mwenyewe.

Hakuna daktari mzuri kama muda hapa duniani ndicho ambacho walikiacha kiamue kwenye hayo mambo, ndani ya ile familia kuna mfanyakazi mmoja ambaye alikuwa ni mrembo sana, mwenye nidhamu sana na mwenye utii mkubwa mno, huyo ndiye ambaye alikuwa akishinda muda mwingi na Zakaria na alimjali sana kama mtoto wake wa kumzaa kabisa mr Mansour alikuwa akiliona hilo na alilichunguza kwa muda mrefu sana mpaka ilipo pita miaka miwili aliona mwanamke huyo anafaa kabisa kuwa mama wa familia yake ndipo alipo itafuta nafasi ya kuweza kumuelezea mwanamke huyo yaliyo kwenye mtima wake akimuomba asimkubalie kwa sababu ni bosi wake hapana bali afanye kile ambacho moyo wake utakisadiki.

Hakuna binadamu mtafutaji anaweza kukubali kuachana na kapu la pesa angali hana hata uwezo wa kununua maji ya mtaani kwa senti kadhaa tu, ombi lilikubaliwa kwa haraka likafikishwa mbele ya familia kabisa lilifurahiwa sana kwa sababu binti huyo aliishi hapo kwa zaidi ya miaka mitano walimjua vizuri kuanzia tabia yake, utu wake pamoja na malezi ambayo alikuwa amepewa kwao wakwe walimpokea kwa mikono yote miwili kwa sasa hakuwa mfanyakazi tena bali akawa kama mke wa ile familia. Maisha yalikuwa mazuri sana na taratibu Mansour the second alianza kumsahau mkewe kipenzi Sekelaga ambaye walidumu kwenye ndoa yao kwa muda mfupi sana wa mwaka mmoja tu ndoa ikiwa bado mbichi kabisa lakini hata hivyo kuna muda alikuwa akikumbuka maisha yake ya kusoma jina na sura ya mwanamke huyo lilikuwa halikauki kwenye uso wake na akili yake kwa ujumla hakuwa na uwezo wa kuurudisha muda nyuma hivyo kitu pekee ambacho alikuwa ana uwezo wa kukifanya kwa huo muda ilikuwa ni kumuombea tu aweze kupumzika kwa amani huko aliko tangulia.

Siku zilisonga na miaka ilikatika Zakaria alikuwa anakaribia kufikisha miaka minne familia ikiwa kwenye furaha kubwa, siku moja majira ya asubuhi ilikuwa ni wikiendi hivyo familia nzima ilikuwa ipo nyumbani siku hiyo walipokea ugeni ambao hata wao hawakuwa wakiutarajia kutoka kwa hao watu, ni jambo ambalo liliwashangaza sana kwa sababu ni ugeni kutoka serikalini ulikuwa ndio umeingia hapo alikuwa ni muidhini wa nchi wa kupima viwango wa madawa yatumikayo na wanadamu pamoja na kuyaruhusu kwa Tanzania tunamwita mkemia mkuu ambaye alikuwa anaitwa profesa Ajeeb akiwa ameongozana na waziri mkuu wa nchi hiyo kwa wakati ule ambaye alijulikana kwa jina la mr Khalfa ndio ambao walikuwa wameingia hapo.

Walikaribishwa kwenye kasri hilo la thamani kubwa sana ndani ya huo mji

“Bwana Mansour samahani sana tumekuja bila taarifa hapa kwako ila ni mhimu sana kwa sababu hakukuwa na ulazima wowote ule kufika hapa ila kikubwa tumekuja kwa sababu ya mwanao”

“Mwanangu kivipi?”

“Wakati huyo mtoto anazaliwa hospitali alichukuliwa vipimo kama watoto wengine ila anaonekana ana nguvu sana ambayo ipo ndani yake ambayo mpaka sasa inahitajika ikafanyiwe uchunguzi huenda akaja kuwa msaada mkubwa sana kwa taifa hili na nguvu hizo kama tukiziacha tu zinaweza kuja kuwa na madahara sana kwa baadaye hivyo inatakiwa akatibiwe pamoja na kuangalia namna nguvu hizo anaweza kuzitumia kulisaidia taifa”

“Whaaat una maanisha nini?”

“Mwanao ni genius ana high Intelligence Quotient kwa vipimo vya kisayansi lakini pia ni mtoto mwenye damu yenye nguvu kubwa sana anavyozidi kukua inaweza kuanza kufanya kazi”

“Noooo nooooo mwanangu hayuko hivyo ni mtoto wa kawaida tu kama wengine, na siwezi kumpatia mwanangu mtu yeyote yule amtunze kama ana huo uwezo huo sio ugonjwa ni yeye tu kabarikiwa, nawaheshimu sana kwa ujio wenu hapa msije mkaninunulia kesi kama mimi ndiye baba wa huyu mtoto hakuna binadamu ambaye anaweza kuniweka naye mbali tokeni humu ndani” alikuwa mkali mno mbele ya kucheza na maisha yamtoto wake alimpenda kuliko kitu chochote kile ndiyo ilikuwa alama ya mkewe kipenzi Sekelaga ambaye alikuwa amefariki kwa miaka kadhaa ambayo iliweza kupita. Viongozi hao walishangaa baada ya kuona mtu huyo kawashikia kabisa bastola kitu ambacho kiliishangaza mpaka familia yake ila kisheria alikuwa ana haki huyo ni mtoto wake yeye ndiye alikuwa ana maamuzi ya mwisho na hakuna mtu angeweza kumfanya kitu chochote kile.

Ilipita wiki moja hali ikiwa imeanza kutulia kwa uzuri sana ila waliipokea taarifa ambayo kwa mara ya kwanza ilimfanya Mansour aweze kuzimia, mtoto wake wa pekee Zakaria alikuwa amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha sana, walitafuta kila sehemu mtoto hakuwepo, walienda kuripoti kila kituo cha polisi bado mtoto hakuonekana, majarida yalibadikwa kila sehemu bado mtoto hakuonekana mji mzima alitafutwa mtoto Zakaria lakini hakuwahi kupatikana ilipelekea mpaka familia kukata tamaa ya kuja kumpata mtoto huyo baada ya kutafuta mwezi mzima na hakuna kilicho patikana.

Unahisi bwanamdogo amepoteaje akiwa na miaka minne tu kasoro? Kafa, kauliwa au yuko wapi mtoto mdogo kama huyu ambaye hawezi hata kukaa pekeyake kwa masaa mawili tu?......twende sawa ndani ya GEREZA LA HAZWA itatupatia majibu kamili mimi sehemu ya 10 sina kitu ambacho ninaweza kukiongezea tena.
JamiiForums1903779814.jpg

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
 
Sijawahi kuchukua uhalisia wa jambo lolote lile kwenye maandiko yangu, huwa nakaa nachora kila kitu na nikiweke vipi....ukifika kuanzia ukurasa wa 10+ nadhani utanielewa, haihusiani NA MTU YEYOTE, MAMLAKA wala taasisi yoyote ile sehemu yoyote ile duniani. Unaweza ukaileta sehemu au kitu ambacho unahisi inafanania, hakuna bosi wangu

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
Mkuu hongera sana hata ambaye anadhani una copy sijui anakuchuliaje. angekuwa Mel Gibson yule Director wa Avatar angemsifia sana na kazi zake ananunua hata kwa 50,000 lakini kwa sababu Mtanzania anaetumia uwezo aliopewa na muumba wake anaona kama ni jambo la ajabu sana. Mkuu FEBIANI BABUYA utatoboa tu Mkuu. hapa unaonekana unatuburudisha lakini Muumba wako anakithamini sana hiki kipaji alichokupatia kutuburudisha na kutuelimisha sisi.
 
Shukrani sana ndugu yangu, MUNGU akupe nguvu sana huko uliko tuzidi kusonga pamoja

Unahisi bwanamdogo amepoteaje akiwa na miaka minne tu kasoro? Kafa, kauliwa au yuko wapi mtoto mdogo kama huyu ambaye hawezi hata kukaa pekeyake kwa masaa mawili tu?......twende sawa ndani ya GEREZA LA HAZWA itatupatia majibu kamili mimi sehemu ya 10 sina kitu ambacho ninaweza kukiongezea tena.View attachment 2413162

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller

UKURASA WA KUMI NA MOJA

TULIPO ISHIA UKURASA WA KUMI

Ilipita wiki moja hali ikiwa imeanza kutulia kwa uzuri sana ila waliipokea taarifa ambayo kwa mara ya kwanza ilimfanya Mansour aweze kuzimia, mtoto wake wa pekee Zakaria alikuwa amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha sana, walitafuta kila sehemu mtoto hakuwepo, walienda kuripoti kila kituo cha polisi bado mtoto hakuonekana, majarida yalibadikwa kila sehemu bado mtoto hakuonekana mji mzima alitafutwa mtoto Zakaria lakini hakuwahi kupatikana ilipelekea mpaka familia kukata tamaa ya kuja kumpata mtoto huyo baada ya kutafuta mwezi mzima na hakuna kilicho patikana.

ENDELEA.....................

Tripoli

“kupitia jeshi la nchi ya Libya kwenye kitengo chake kimoja nyeti sana cha kivita kuna kambi kubwa ya siri ambayo iliweza kuanzishwa ndani yake kwa usiri mkubwa mno kupitia vikosi vya upiganaji vya Mih-30, Mih-42 na Mirak-zi9. Kambi hiyo ya siri ambayo ilianzishwa haikuwa kwa ajili ya hao wanajeshi ambao kila mtu angehisi kwamba ilikuwa hivyo bali ilikuwa maalumu kwa ajili ya kuwatengeneza watoto wadogo ili kupata wanajeshi shupavu kwa ajili ya kuja kuilinda nchi hii kwa jasho na damu kutokana na vita kali ambayo ilikuwa ikiendelea kusini kabisa mwa nchi ya Libya baada ya magaidi wa kundi la ALIH The Salijah of JAZIRAH ambalo lilisababisha machafuko makubwa sana ndani ya nchi kwahiyo ili kuweza kupambana na kundi hilo serikali ya nchi ilianzisha mpango wa CWO (Cease the War Operation) ulio simamiwa na waziri mkuu wa nchi hii ya Libya na ulikuwa ni mpango mashuhuri sana na wa siri mno kwa ajili ya baadaye ya nchi hii.

Ndani ya nchi mpango huu waliujua watu wawili tu hata mheshimiwa raisi wa wakati ule aliweza kufichwa na hakuwahi hata kuujua japo kwa nukta moja tu kutokana na kukosekana kwa uaminifu miongoni mwa hao watu. Waziri mkuu na muidhini mkuu wa viwango vya dawa nchini ndio watu pekee ambao walikuwa na uelewa na hilo jambo na ndio ambao walikubaliana kwa siri ili waweze kuiokoa nchi kutoka kwenye hiyo hali ambayo ilikuwa inaendelea kwenye miji ya The Al-Jawf town, The Al-Zighan town, The Rebian Town na The Al-Taj. Kwenye hiyo oparesheni hesabu zao ilikuwa ni kuwapata watoto wenye weledi mkubwa sana na akili kubwa ili waweze kusaidia kwenye mambo mengi ikiwa na mipango mikubwa sana ya baadae ya taifa hili ndipo ulikuja mpango wa kuanzisha shule ambayo nayo ilikuwa ni ya siri ilihitajika pesa nyingi kuwalipa hao watu ambao walitakiwa kuja kufundisha kwenye hiyo shule ambayo ilikuwa inahitajika kuanzishwa, ila huu mpango ulikuja ukafutwa baada ya kuona gharama zitakuwa kubwa mno kwahiyo kilicho shauriwa ni kwamba watu hao wangeenda kusoma kwenye vyuo vikubwa kwa baadaye baada ya kukomaa sana huku wakiendelea kutengenezwa kwa mazoezi makali mno ili kuweza kupunguza gharama na hawakuwa wengi walichukuliwa watoto sita tu pekee na hao watoto wote hakuna ambaye alipatikana kwa njia ya halali wote waliibwa”

“STOOOOOOOOOOP, kivipi watu wa serikali waibe watoto wa raia wao kirahisi sana hivyo bila ruhusa ya wazazi wao?” mheshimiwa raisi aliamua kumkatisha mzee huyu ili aweze kumuweka sawa kwanza mambo ambayo yalikuwa yanaongelewa yalikuwa ni mazito mno na tangu ameingia madarakani ilikuwa imepita miaka zaidi ya 12 na hakuwahi kabisa kuwa na taarifa za ndani kiasi hicho mpaka alibaki mdomo wazi tu akiwa anashangaa tu.

“Kati ya hao watoto sita ambao walipatikana kwa njia ya kuweza kupima uwezo wa kiakili na damu za watoto wanao zaliwa kwenye hospitali zote walipatikana watoto 50 ndipo walipo anza kupima uwezo wa akili kuanzia miaka kumi na mitano ijayo mpaka walipo patikana hao sita lakini shida kubwa ilikuja pale ambapo kila familia ambayo walikuwa wakiomba watoto hao hakuna familia ambayo ilikuwa ipo tayari kuruhusu hilo jambo litendeke na ilikuwa ni lazima ifanyike hivyo kwahiyo uliandaliwa mpango wa kuweza kuwaiba watoto hao kwa siri bila mtu yeyote kujua na walikuwa wakiibiwa kila baada ya masaa kumi anachukuliwa mtoto mmoja kitu ambacho kilifanya ndani ya siku mbili na masaa kadhaa wakawa wamepatikana watoto wote sita na kwenda kufichwa huko ambako walitakiwa kuyaanza maisha mapya kabisa na ndipo hapo ambapo familia nyingi sana zilianza kuripoti na kulalamika watoto wao kupatikana ila hakuna walichoweza kukipata kwani ilikuwa ni siri nzito ya watu wachache mno” alielezea kwa sasa alionekana kumpa nafasi raisi huyo kuweza kuuliza maswali ambayo yalionekana kumtatiza sana kwenye kinywa chake akiwa hana sehemu nyingine ya kuweza kuipatia majibu zaidi ya kwa mzee huyo kichaa kama alivyo julikana cha ajabu hakuwa na ukichaa wowote ule kwenye maisha yake.

“Kwa taarifa yako inaonekana wazi walikuwa wanachukuliwa kwenye familia ambazo zilikuwa zina uwezo mkubwa sana sasa iliwezekana vipi wakafanikiwa kuwaficha bila watu hao wenye ukwasi wa kutosha kujua walipo?” aliuliza swali lingine tena kwa mwanaume huyo.

“Umeiongoza hii nchi kwa muda gani ukiwa kama raisi?”

“Ni zaidi ya miaka kumi na miwili sasa”

“Unajua uwepo wa idara ya usalama wa nchi yako?”

“Ndiyo”

“Unawajua majasusi na makomando wangapi ambao wapo ndani ya hizo idara za usalama wa nchi yako mwenyewe?”

“Kwa sasa nawajua wapo miamoja kwa ujumla wao”

“Unahisi ni kweli wapo miamoja basi?”

“Yes, kwa sababu raisi lazima nipewe list ya majina yao siku tu naingia ikulu wakati napewa madaraka hiyo ni sehemu nyeti sana kwenye usalama wa raisi hivyo sio ombi ni lazima mimi niweze kujua kila kitu ambacho kinaendelea”

“Mhhhhhhhh nani amekwambia kwamba raisi ni lazima aweze kujua kila kitu ambacho kinaendelea kwenye nchi yake?”

“Mimi ndiye mtu mkubwa zaidi kwenye nchi, mimi ndiye mtu mwenye kauli ya mwisho zaidi kwenye nchi, mimi ndiye naamua nini kifanyike nini kisifanyike unadhani kuna kipi ninaweza nisikijue mimi kwenye nchi yangu mwenyewe hahhahahahaa”

“Hilo neno usije ukalirudia tena kwenye midomo ya watu ambao wapo kwenye nchi hii wanakuona ukikua, hakuna kitu kikubwa ambacho wewe hapo unakijua ndani ya nchi hii zaidi ya kufanya starehe na mahawala wako tu. Nikikuuliza hii nchi ina wanajeshi wangapi hujui, nikikuuliza tu kwenye ikulu yako mwenyewe ambako ndiko unaishi hujui kuna idadi ya watumishi wangapi na kwanini wawekwe kwa hiyo idadi hujui kwahiyo kuna muda huo mdomo wako utakuja kukufanya ufe ukiwa huelewi lolote”

“Hey unamaanisha kuna hadi mambo ya usalama ambayo mimi siyajui?” raisi alinyanyuka akatoka kitambaa mfukoni alijifuta jasho ambalo lilikuwa limeanza kumtawala kwenye uso wake kwa presha mno leo alikuwa anashangazwa sna na maneno ya mtu ambaye alikuwa mbele yake aliambiwa hakuna mambo ya mhimu saaaana ambayo yeye anayajua kuhusu nchi hii ambayo yeye alikuwa akijisifia sana kwamba anaijua.

“Hii nchi mpaka saivi ina majasusi miambili wenye mafunzo ya hali ya juu sana pamoja na makomando 79 wenye mafunzo ya juu mno kati ya hao 20 wanakulinda wewe kila unapokuwa kuhakikisha upo salama muda wote na……….”

“Shut up. umeanza kuniona mimi ni mtoto mdogo sio, yaani nalindwa na walinzi wangu wale pale ambao wanajulikana leo unaniambiwa nalindwa na makomando ishirini hahhahhha usiniambie unaanza kuzeeka mapema hivyo nitakuu……” alifoka sana raisi ila alikatishwa

“Leo ndiyo siku pekee ambayo umeipata nafasi ya kuweza kukaa namimi huenda baada ya leo hatutakuja kuonana tena unapaswa uwe mpole kunisikiliza kwa umakini vinginevyo hakuna sehemu yoyote ambayo utakuja kuyajua haya mambo tofauti na kwangu kitu ambacho kinaweza kukufanya ukae siku chache sana kwenye hicho kiti ambacho bila shaka ndicho kinakupa kiburi” ilimlazimu kuwa mpole baada ya kutishiwa japo alikuwa ana hasira kali sana.

“Usingekuwa unalindwa na hao watu ungeshakufa muda mrefu sana kwa sababu umedhulumu nafsi za watu wengi ambao hawana hatia kuna watu familia zao zinakuwinda nafsi yako kuliko hata watu wanavyo itafuta pepo. Kuhusu hao watoto kwamba iliwezekana vipi kuwaficha nimekuuliza hapa namna unavyo ujua ulinzi wa nchi yako na hujui chochote kile mtu ambaye una mamlaka ya kila kitu kwenye nchi hii je kama wewe kuna mambo mengi tu tena mhimu kwa nchi huwezi kuyajua kuna raia gani anaweza kujua baadhi ya siri nzito kama hizo ambazo hata viongozi wakubwa pamoja na raisi mwenyewe wa wakati ule hakuwahi kuzijua?........ ukisikia kitu kinaitwa siri kwenye sehemu za usalama wa nchi basi huwa zinakuwa kwa watu wachache ambao kwa namna moja ama nyngine huwa wanafundishwa kwa miaka mingi sana namna ya kuwa na vifua vipana ndiyo sababu unaweza ukawakamata hapa utamtesa mpaka afe au atajiua yeye mwenyewe lakini katu hata siku moja hawezi kuja kukwambia hizo siri zitabaki kuwa zake na mtu aliye mpa mpaka MUNGU atakapo mchukua.

Hao watoto hakuna aliyeweza kujua kwa sababu walisambazwa kwenye nchi tofauti tofauti ikiwemo Marekani, Russia (Urusi), China, Thailand, Cuba pamoja na Malaysia. Walikuwa wakisoma kwa siri sana huku wakiendelea na mafunzo makali kwani kila nchi waliyo kuwepo watoto hao zilifunguliwa camp za muda ambako ndiko walikuwa wakihifadhiwa kwa muda wote mpaka pale ambapo wangerudi kwa mara nyingine tena kwenye ardhi za nyumbani. Baada ya miaka miwili watoto watano waliweza kufa kutokana na mazoezi makali ambayo yalikuwa hayaendani kabisa na umri wao hivyo akawa amebaki mtoto mmoja tu pekee ambaye kwa wakati huo alikuwa ndani ya nchi ya Malaysia, huyu ndiye aliyebaki kuwa tegemeo la pekee kwenye ile oparesheni ya kuja kuikomboa nchi kwa baadae baada ya wenzake wote kuweza kupotea kwenye uso wa dunia, mtoto huyo ndiye ambaye alikuwa anaitwa Zakaria Mansour ila kwa kule walimjua kama Aariz Salman ila huo ndio ulikuwa mwanzo mbaya zaidi kwenye historia ya hii simulizi kwani bwana Mansour alikuja kugundua mpango ambao ulikuwa umetekelezwa na mheshimiwa waziri mkuu pamoja na muidhini mkuu wa dawa za wanadamu, aliusoma mpango kuanzia nukta ya kwanza mpaka pale ulipokuwa umehitimishwa alikuwa na hasira kama mzazi kwani aliishi kwa kuteseka na kujua mwanae alishakufa lakini alikuwa hai kabisa na moja kwa moja alijua serikali ndiyo iliyo husika na kupotea kwa mtoto wake wa pekee.

Baada ya kuuelewa ule mpango mzima alizitafuta familia zote ambazo zilikuwa zimepotelewa na watoto wao ili waungane na kuwa kitu kimoja kwenye kupambana na hali ambayo ilikuwa imewakumba na ni wazi kabisa hawakupendezwa nayo kwa asilimia zote, lile lilikuwa ni jambo ambalo lilikuwa linaenda kuhatarisha usalama wa nchi na serikali nzima kwa ujumla kama lingeenda kwenye vyombo vya habari na watu wakajua uhalisia wa hayo mambo yalivyo tokea kwahiyo kwa ajili ya kusaidi hali hiyo iliamuliwa yachukuliwe maamuzi mazito sana ya kuweza kuziua familia zote sita kwa sababu hawakuwa na jibu la kuwapa na ukiangalia watoto watano walikuwa tayari wamekufa nini kingefanyika?.......

Kila mtu ambaye alikuwa akihusika kwenye zile familia zote sita alichinjwa hakuachwa hata ndugu wa mbali kama ushahidi na hakuna mtu kwa wakati ule ambaye alielewa kwmba ni nini kiliendelea kwa zile familia miili yao ilizikwa kwa kutupwa kwenye asidi hakuna ushahidi wowote ambao ulibakishwa kwa ajili ya watu ambao wangeamua kuifuatilia kesi hiyo. Ila hicho ndicho kilichokuja kupelekea kifo kibaya sana cha waziri mkuu yule na muidhini yule wa dawa kwa miaka ya baadaye baada ya taarifa kufika kwa mtu mmoja tu pekee ambaye alifanikiwa kupona kwenye hizo familia sita wengine wote wakiwa marehemu na ndiye huyo ambaye walimfuga wenyewe ila baadae walikuja kujutia wao wenyewe kwa ambacho alikuja kukifanya” maelezo ya mzee huyu yalikuwa yakimsisimua sana raisi alikuwa kila muda anajifuta jasho kuonyesha hali kubwa ya wasiwasi sana alionekana kuto yajua mambo mengi sana kwenye nchi yake.

“Nani ambaye aliufanya huo ukatili kwa kiongozi mkubwa sana ambaye analindwa sana kama waziri mkuu” aliuliza swali lake akinyanyuka kidogo na kuchuchumaa alikaa kwa muda mrefu sana ila hakuwa na namna maelezo ambayo aliyahitaji ni kama alikuwa amemegewa robo tu ya yale ambayo alikuwa anayahitaji kuyapata siku hiyo.

“Ndiye huyo ambaye wewe umemleta leo hii kwenye hili gereza la siri ambalo halijulikani”

“Whaaaaaat you mean Zakaria”

“Yes”

“How(kivipi?)” aliuliza kwa mshangao mkubwa ambao ulimfanya mzee huyo ambaye hakuonyesha dalili ya kuchoka kukaa hapo ni wazi alipazoea sana alimtazama kwa umakini rais huyo usoni ambaye alikuwa kama anataka kuchanganyikiwa, aliiwasha sigara ambayo alikuwa ameizima kwa muda akavuta mafunda mawili na kuuzamisha moshi kwenye mdomo wake kisha akaupitisha kwenye koo lake na kuutolea puani alifanya hivyo mara tatu na kuizima sigara hiyo akakaa kwa kuikutanisha miguu yake na kumgeukia mheshimiwa raisi sasa alihitajika kuingia kwenye ulimwengu rasmi wa kumfanya raisi huyo kuujua ukweli juu ya kitu ambacho kilimfanya bwana mdogo aliyekuwa anapewa stori yake kuwa kiumbe cha kutisha mno.

Bado hakuna kitu unakijua kuhusu Zakaria relax tumfahamu kiumbe huyu, unadhani kipi kilikuja kumfanya akawa binadamu wa kutisha mpaka anatafutwa na mamlaka za nchi za kaskazini ambao wamempata pamoja na mamlaka za nchi za magharibi ambao wanamhitaji kwa gharama yoyote? Zakaria ni nani hasa yeye?......nimechoka sana 11 natundika daruga mpaka wakati ujao tena.

Bux the story teller.
JamiiForums1555066020.jpg
 
Bux the story teller.View attachment 2418725
STORY: GEREZA LA HAZWA
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller

UKURASA WA KUMI NA MBILI

TULIPO ISHIA UKURASA WA KUMI NA MOJA

“How(kivipi?)” aliuliza kwa mshangao mkubwa ambao ulimfanya mzee huyo ambaye hakuonyesha dalili ya kuchoka kukaa hapo ni wazi alipazoea sana alimtazama kwa umakini rais huyo usoni ambaye alikuwa kama anataka kuchanganyikiwa, aliiwasha sigara ambayo alikuwa ameizima kwa muda akavuta mafunda mawili na kuuzamisha moshi kwenye mdomo wake kisha akautolea kwenye koo lake na kuutolea puani alifanya hivyo mara tatu na kuizima sigara hiyo akakaa kwa kuikutanisha miguu yake na kumgeukia mheshimiwa raisi sasa alihitajika kuingia kwenye ulimwengu rasmi wa kumfanya raisi huyo kuujua ukweli juu ya kitu ambacho kilimfanya bwana mdogo aliyekuwa anapewa stori yake kuwa kiumbe cha kutisha mno.

ENDELEA..................

“Akiwa ndani ya Kuala Lumpur Malaysia alikuwa ni mwanafunzi mwenye akili za kutisha kupita kiasi hivyo hakusoma kama wenzake ambao huwa wanasoma kwa muda mrefu sana alirushwa rushwa sana madarasa ndiyo sababu huwa inashangaza mtoto mdogo kama yule tayari ni Doctor of Philosopy (PhD) kwa wataalamu wa mambo ya akili za mwanadamu ni mtu mwenye akili za hali ya juu yaani Genius ndiyo sababu alifanikisha mambo yake kwa muda mrefu sana. Masomo yake yalimalizika salama kwenye nchi ya Malaysia ndipo ikaamuliwa akamalizie ndani ya nchi ya China katika chuo kikuu cha Beijing University of Technology ambako alisoma kwa miaka minne tu pekee na kupewa hiyo heshima ya kuwa doctor mdogo zaidi duniani akiwa amesomea USANIFU WA MAJENGO pamoja na uandishi na uchoraji ni kitu ambacho hakukisomea kwa kupenda kwake ila ulikuwa ni mpango ambao uliandaliwa kwa miaka mingi sana yeye kuweza kusomea hicho kitu.

Kwa hiyo miaka ambayo alikuwa akisoma huko hakuwahi kumjua mwanamke kabisa kwenye maisha yake yote hivyo akiwa China alichukuliwa mwanamke mmoja mrembo sana kutoka katika nchi ya Libya ambaye aliandaliwa ikiwa ni ushauri wa mwalimu wake ambaye alikuwa anamfundisha saikolojia huko huko china, unaweza ukajiuliza kwanini aliandaliwa mwanamke kwa ajili yake wakati alikuwa kazini? Sasa hapa ndipo unapo enda kuijua sababu ya msingi kwamba ni kwanini umoja wa nchi za magharibi mwa Afrika zinamsaka mtu huyo usiku na mchana na kwa gharama yoyote ile nisikilize kwa makini sana na unielewe hapa.

Wakati anatolewa Malaysia kwenda China alikuwa tayari amefikia umri wa kuanza kujielewa kabisa kwani alikuwa amekomazwa mno kiakili japo alikuwa bado ni kijana mdogo kutokana na kusoma shule kwa muda mfupi kulingana na uwezo wake wa akili ambao alikuwa nao, baada ya kufika China waliajiriwa watu sita kwa ajili ya kumfunza aina tofauti za mapigano ambayo yalikuwa yanapatikana kwenye nchi hiyo hivyo alikuwa hawezi kupata kabisa muda wa kusema atakuwa huru kwenda popote, kufanya starehe yeye alicho kijua ilikuwa ni mazoezi ya kutisha sana pamoja na masomo vitu viwili tu hakuwa na nafasi ya vitu vingine kwenye kichwa chake ndipo huyo mwalimu wake wa saikolojia alipoweza kushauri kwamba mtu huyo anahitaji kuwa karibu na mtu ambaye kama akimpenda inaweza kuwa nafuu kwani ameanza kuathirika kisaikolojia kutokana na kukosa kitu kinaitwa upendo kwenye moyo, kichwa na akili yake kwa ujumla na hilo linaweza kuja kuwa tatizo kubwa sana kwa baadae anaweza asiwe na moyo wa kibinadamu kabisa. Mwili wa mwanadamu uliumbwa kwa makusudi sehemu kubwa zaidi ya asilimia 80 zipo kwa sababu ya upendo ndio maana mtu ambaye anapendwa sana iwe na mtu wake wa karibu au ndugu zake ndiye mtu ambaye huwa anayafanya mambo yake kwa weledi sana ila mtu anapo ukosa upendo huwa anakuwa na haiba ya unyama na anaweza kuanza kufanya matukio ya ajabu sana. hapo sasa ndipo ilipoanza oparesheni mpya ya kumtafuta kigori ambaye hakuwahi kumjua mwanaume yeyote akiombwa kwenda kumtengeneza mtu huyo saikolojia ila huyo mwanamke hakuambiwa katu nyuma ya pazia kama hilo dubwana lilikuwa linatengenezwa kwa kazi maalumu, kwa mara ya kwanza ilikuwa ni ngumu sana kumshawishi ukizingatia alikuwa ni mtu wa dini sana ila palipo na pesa unatakiwa upaogope mno kupitia wazazi wake hilo jambo lilikamilika mapema tu na mwanamke huyo akasafirishwa mpaka China kwenda kukaa karibu na hicho kiumbe kwa miaka minne japo kwa tahadhari sana hakutakiwa kujua kabisa kwamba hicho kiumbe ni cha hatari hapo ndipo kisasi kilipo anza kutengenezwa sasa kivipi?” mzee huyu kabla hajaendelea na maongezi yake ambayo yalionekana kuanza kukolea sana kwa visa vya kusisimua ambavyo vilikuwa vimejipanga kwenye simulizi ya huyo binadamu mheshimiwa raisi aliweza kuingilia maongezi.

“Huyo mtoto muda wote huo hakuwahi kuwaza kuhusu familia yake au kuuliza? Maana yake kama alichukuliwa akiwa bado mdogo sana sasa inakuaje asiwakumbuke watu ambao walikuwa wapo karibu na yeye maana huwa ni kawaida kwa watoto unapomuweka mbali na mtu ampendae huwa inaleta matatizo makubwa sana”

“SAIKOLOJIA. Hili neno ndiyo sababu ya kila kitu, ombea uumwe ugonjwa wowote duniani ila sio kukumbwa na tatizo la saikolojia unakuwa sio wewe tena inakuwa ni nafsi nyingine japo itaishi kwenye mwili wako ndiyo sababu kubwa hata makomando wakikamatwa kwenye uwanja wa vita wapo radhi kujiua wenyewe na sio kuingia kwenye mikono ya wapinzani wao kwa sababu wanajua haya matatizo ya saikolojia yanaweza kuwafanya wakataja siri zote za nchi yao. Chukulia mfano wewe ukawekwa kwenye chumba ambacho kimejaa maiti ukafungiwa huko halafu kuna mauza uza kibao unahisi baada ya mwaka utatoka ukiwa ni wewe hapo na akili yako? Hapana utatoka ukiwa ni mtu mwingine kabisa japo mwili utakuwa ni ule ule ila nafsi haitakuwa yakwako tena sasa hicho ndicho kilichotumika kumbadilisha yule mtoto mpaka sasa hana kumbukumbu zozote kuhusu familia yake na wala hajijui vizuri yeye ni nani kwa aina ya maisha ambayo amelelewa alikuwa akimsikiliza mtu mmoja tu ambaye ndiye pekee alikuja baadae kupona kwenye huu mpango wa hawa wote walio husika nao.

Basi yule mwanamke baada ya kufika China alianza kuweka ukaribu na bwana mdogo ambaye mara ya kwanza ilikuwa ni ngumu sana kwa sababu hakuwahi kuyazoea hayo maisha huku kwa siri akiendelea kuwekwa sawa ila kadiri siku zilivyokuwa zikizidi kwenda alijikuta akianza kumzoea yule mwanamke kwa kuwa ndiye ambaye alikuwa anamjali na kumuongelesha kila alipo muona taratibu alijikuta ananza kumpenda na matokeo yake baadaye wakaja kupendana kweli sasa ikawa sio maigizo tena kama ilivyokuwa imekubaliwa kwenye kazi. Alikuwa mwanamke wake wa kwanza hata kwa mwanamke yule ndiye aliyekuwa mwanaume wake wa kwanza kumpenda kwenye maisha yake yote kwa mara ya kwanza huyo bwana mdogo alianza kuonyesha tabasamu lake kwenye maisha yake mpaka siku anamaliza kwa mara ya kwanza baada ya miaka zaidi ya kumi na mitano kupita alikuwa anakanyaga tena kwenye ardhi ya nchi ya Libya akiwa kama binadamu mpya, walirudi watu watatu tu pekee yeye, huyo mwanamke wake pamoja na mwalimu wake ambaye miaka yote hiyo ndiye aliyekuwa kama mlezi wake kwa kila kitu ambacho yeye alikuwa anakifanya.

Jioni moja akiwa mwenye furaha sana sehemu ambayo alikuwa anaishi na huyo mwanamke wake baada ya kupokea taarifa kwamba mwanamke huyo alikuwa ni mjamzito nadhani hakuwahi kulijua neno familia kwenye maisha yake ndiyo sababu kubwa ambayo ilimfanya kuwa na furaha iliyopita kiasi namna hiyo, muda huo aliingia mwalimu wake mlezi huyo ambaye alikuwa anamsikiliza na kumheshimu mno lakini hakuwa pekeyake alikuwa ameongozana na watu wawili, mtu wa kwanza alikuwa ni yule waziri mkuu wa zamani wan chi ya Libya ambaye kwa sasa alikuwa ni mshauri mkuu wa raisi ambaye alikuwa ni mpya madarakani lakini mtu wa pili alikuwa ni muidhini wa dawa za binadamu ambaye mpaka sasa bado alikuwa kwenye nafasi yake ile ile, hakuishi kabisa kwenye nchi hiyo japo alikuwa anajua vizuri sana kuongea zaidi ya lugha kumi miongoni mwa hizo Lugha kilikuwepo Kiswahili na hakuwahi kujua sababu ya yeye kuweza kufundishwa hiyo Lugha wakati haihusiani kabisa na taifa lake la Libya.

“Aariz unajijua wewe ni nani na kwanini upo duniani?” hi huyo mlezi wake ambaye alimuuliza swali hilo. Kwake halikuwa geni sana ila hakutegemea kuulizwa kwa ssbabu tangu anakua yeye amekuwa akiambiwa kila muda kwamba yeye ni alama ya taifa la Libya popote pale anapokuwepo hivyo hakuwa na shaka kwamba yupo kwa ajili ya kulilinda taifa lake hicho ndicho kilicho mshangaza zaidi kwanini aulizwe swali ambalo miaka yote amesisitizwa kuwa hivyo?

“Ndiyo mimi ni aseti bora na kubwa zaidi ndani ya nchi hii hili ndilo la mhimu zaidi kwangu na nipo tayari muda wowote kuhakikisha nalitetea taifa langu na bendera ya nchi yangu kwa ujumla” alijibu kikakamavu akiwa anakunywa juisi taratibu.

“Good, sasa naomba nikukutanishe na hawa watu wawili ambao ndio watu mhimu zaidi kwenye safari yako ya maisha kuliko hata mimi, hawa hapa wawili ndio watu pekee ambao waliamua kutumia pesa zao ambazo wamezitafuta kwenye ujana wao kuhakikisha wewe unatengenezwa na kukamilika kiasi hiki ili kuja kulilinda taifa hili naweza kusema hawa ndio watu wa mhimu zaidi kwenye maisha yako” alihitimisha maelezo yake akionekana wazi aliongea vizuri na vigogo hao wawili waliitikia kwa vichwa, Aariz Salman ambalo ndilo lilikuwa jina lake alilokuwa analitumia kwa sasa kwenye maisha yake na hakuwahi kujua kama ana jina lingine aliinama na kutoa heshima kwa watu hao kwani walionekana kuwa na umuhimu mkubwa sana kwake kisha akaketi chini kuwasikiliza.

“Ni matumaini yetu kwa sasa umekuwa mwanaume kamili na msomi sana hilo hatuna shaka nalo kabisa, haya yote yamefanywa kwako na sio kwa mtu mwingine kwa sababu uwezo wako uliwahi kuonekana mapema kabla ya wengine labda kama ulikuwa hujui tu mlikuwa sita wenzako watano walikufa kwenye mazoezi kwenye nchi mbalimbali ambazo walipelekwa hivyo mtu pekee ambaye uliwahi kupona kwenye hili jambo ni wewe (Aariz alishtuka kusikia hicho kitu hakuwahi hata siku moja kujua kwamba walikuwa wapo wengi na kuna wenzake ambao walikuwa wameshakufa tayari japo alijitahidi sana kuto uonyesha mshtuko huo moja kwa moja mbele ya wakubwa wake ambao ndio waliowekeza pesa za kutosha kwa ajili ya kumtengeneza yeye na kuwa dubwana la ajabu). Hili jambo limefanywa sio kwa sababu ya kujifurahisha wala kupoteza muda hapana ila ni jambo la kuweza kuliokoa taifa letu pendwa na kulipatia ulinzi ambao linastahili kwa muda sahihi.

Kwenye mikono yako kwa sasa una kazi kubwa mbili za kuweza kuzifanya kazi ya kwanza, ni miaka mingi sana kusini mwa nchi yetu sasa tunaelekea kuipoteza ardhi ya ile sehemu na kila kilichopo kule kutokana na kundi moja kubwa sana ka kigaidi liitwalo ALIH tHe SALIJAH OF JAZIRAH kuweza kuishikilia ile sehemu ambayo ndiko iliko hazina kubwa zaidi ya mafuta yanayo iendesha nchi, nadhani mipango yao ni mwaka ujao wawe tayari wameteka eneo lote lile kitu ambacho ni cha hatari kupita kiasi na kitaipelekea nchi hii kwenye umaskini wa kutupwa litakuwa ni jambo la kutisha zaidi kuwahi kuikumba nchi hii hivyo umeandaliwa wewe ili kuweza kuliokoa taifa wakati linapitia kwenye hii changamoto kubwa na vita kali ya kiuchumi na hili linahitajika kufanyika haraka sana baada ya hapo ndipo utakapokuja kuambiwa mpango wa pili ni upi ambao unahitajika kufuata baada ya huu hapa” maelezo ambayo yalimuacha mdomo wazi Aariz hakuwahi kujua kama nchi yake ilikuwa kwenye wakati mgumu sana namna hiyo na wala hakuwahi kusikia sehemu yoyote ile ndani ya serikali yoyote duniani ikilalamika kuhusu hilo jambo.

“Kwanini hili jambo serikali haijalifanyia kazi kwa miaka yote hiyo mpaka mruhusu watu kuanza kuitawala ardhi ya serikali kiasi hicho?”

“Serikali imefanya kila namna ya kutuma wanajeshi na makomando huko lakini imekuwa ni kazi bure wote huwa wanakufa na kurudishwa wakiwa maiti ndiyo sababu ya msingi tukaja na huu mpango ili kuliokoa taifa” muidhini mkuu wa dawa za binadamu alijibu akiwa mkavu kabisa kwenye uso wake.

“Sasa kwanini halijawahi kuripotiwa kwenye vyombo vya habari?” aliuliza swali lingine tena.

“Ilifanyika kuwa siri nzito kwa sababu kulionekana kuwa na usaliti ndani ya serikali kuanzia viongozi wa ngazi za juu akiwepo mheshimiwa raisi mwenyewe hivyo kama haya mambo yangeruhusiwa kujulikana kwa watu wengi basi mauaji yangezidi zaidi ndio sababu ukaandaliwa huu mpango wa siri sana ambao ni watu wachache walikuwa wakiujua”

“Whaaaaaaat you mean hata mheshimiwa raisi wa wakati huo hakuwa akijua juu ya hili?”

“Ndiyo”

“Why?”
“Hata yeye alikuwa ni mhusika mkuu kwenye hilo kundi”

“Whaaaaaaaaaaaaaat” Aariz hakuweza kuamini hicho kitu alishtuka sana

Mipango ndani ya mpango tupo taratibu sana na GEREZA LA HAZWA hatuna haraka, mambo yanazidi kuwa mengi muda unaendelea kupungua kuna mengi ambayo hata hatujayagusa kabisa humu ndani ila kupitia kalamu yangu unaenda kugusiwa moja baada ya jingine utaelewa kwanini ujio wa mke wa Aariz kwa mara ya kwanza China ulisababishaje yeye kuanza kutafutwa sana na mamlaka za nchi za magharibi mwa Afrika. Niseme nini tena 12 nanyoosha mikono juu natupa kalamu chini sina la nyongeza.

Bux the story teller
 
UKURASA WA KUMI NA TATU

TULIPO ISHIA UKURASA WA KUMI NA MBILI

"Yes baada ya uchunguzi mzito wa muda mrefu tulikuja kugundua kwamba raisi ndiye mtu ambaye alikuwa amewapa kibali watu hao cha kufanya mambo ikiwa nayeye alikuwa mnufaika mkubwa wa kile ambacho kilikuwa kinaendelea kule hivyo tuliandaa mpango akauawa kisha baadae tukampenyeza raisi mwingine madarakani ambaye yupo mpaka saivi"
"Subiri kwanza huyo raisi anaye zungumziwa hapo kwamba alipenyezwa ni Mimi au Kuna mwingine kabla yangu" Malek Salem aliingilia kati hayo mazungumzo hayo ili aelewe anazungumziwa nani

"Hapana wewe ulikuja miaka miwili baadae wakati huu ulikuwa unaandaliwa tu" alitoa macho sana na kufuta jasho lake.

"So kipi kinatakiwa kufanyika Kwa sasa?" Aariz aliuliza swali Hilo Kwa sababu mbele yake kulikuwa na kazi nzito sana na hakukuwa na namna yoyote ile ya kuweza kuikwepa.

"Kuanzia Kesho unatakiwa kusafiri haraka ukamalizane na hilo kundi la magaidi kisha ukirudi Kuna kazi ambayo utapewa nyingine ya kuweza kuifanya baada ya hapo utaondoka Libya na kwenda Tanzania kupumzika"

"Why Tanzania?" Aliuliza Kwa mshtuko mkubwa
"Maliza kazi Kwanza utaambiwa sababu ya kwanini unaenda Tanzania"

"Nihakikishieni tu ulinzi wa mke wangu"

"Yes ni jukumu letu kumlinda ila hatakiwi kujua kuhusu kitu chochote kile juu ya maisha yako na kwamba wewe ni nani hata hiyo Kesho anatakiwa kujua tu kwamba wewe unasafiri kibiashara na sio kitu kingine chochote kile"

"Yule ni mke wangu Kuna ubaya gani akijua?"

"Hizi sio kazi za kukaa na kumhadithia kila mmoja kile unacho kifanya, ni watu wachache sana ambao tupo mbele yako hapa pekee ndio tunaojua uwepo wako na umuhimu wako kwenye nchi hii hivyo hakuna mtu mwingine anapaswa kujua vinginevyo utaruhusu afe, Kwa kila ambaye anatambua uwepo wako lazima afe litakuwa ni tatizo kubwa sana hata kama.ni mkeo wa ndoa hupaswi kumuamini sana kiasi hicho sisi kama nchi tunayajua vizuri haya mambo ndio maana tuna mapandikizi kibao kwenye makundi ya kigaidi wengine ni wanawake wazuri sana na wameolewa huko japo magaidi wanawaita wake zao ila ni majasusi wetu hivyo kuwa makini sana, maelelezo atakupa kiongozi wako" walimaliza kuongea hao wanaume kisha wakaondoka bila hata kuaga kilichokuwa kimewaleta hapo walikuwa wamekikamilisha kilichokuwa kimebaki ni utakelezaji wa kazi.

Siku ya pili yake mwanaume alikuwa kwenye gari moja yenye spidi kubwa sana Kwa sababu ilikuwa miongoni mwa gari ambazo zilitengenezwa Kwa ajili ya watu maalumu, alikuwa anaenda na muda ndicho kitu ambacho kilikuwa mhimu sana kwake kwa wakati huo, usiku wa siku hiyo ulitakiwa kumkutia sehemu ambayo alikuwa anaenda japo hakujua ukubwa wa kazi ambayo alikuwa ameiendea huko ila alikuwa ana imani kwake usiku mmoja ulikuwa ni mkubwa sana na ungemtosha kabisa kumaliza kile ambacho kilimpeleka. Masaa 15 ya kuwa njiani yaliweza kumpeleka kwenye pori moja ambalo lilikuwa linasadikika kumilikiwa na hao magaidi ambao ndio walikuwa wamelishika eneo zima la kusini mwa nchi ya Libya.

Kulitulia sana na hakukuwa na dalili yoyote ya uwepo wa mtu hata mmoja wala uwepo wa kiumbe chochote kile chenye kupumua mithili ya mwanadamu, umbali wa kilomita mbili mpaka kuanza kuingia ndani kabisa ya kwenye pori hilo ndiyo sehemu ambayo aliweza kupaki gari yake, baada ya kushuka alitembea hatua tano mbele na kugusa moja ya jani la mti ambao ulikuwa upo kando ya hicho kinjia ambacho hakikuwa rasmi mwili wake ulimsisimka mno aligeuka huku na huko lakini hakuona mtu ila tayari alikuwa ameshapata jibu ya kwamba hilo eneo kulikuwa na watu wa kutosha maili kadhaa kutoka hapo alipokuwa alichuma jani hilo na kulitafuna kisha akalitema baada ya kujiridhisha kwamba huo haukuwa msitu wa asili bali ni miti ambayo ilikuwa imepandwa na mwanadamu lakini kutokana na kazi ambayo ilikuwa inafanyika ndani ya hiyo misitu iliifanya kutengenezwa kana kwamba mtu angehisi kwamba ni ya asili.

Pembeni ya bega lake la kulia kulikuwa na upanga mmoja na visu viwili lakini chini ya kitovu chake alionekana kuvaa nyuo ya kuvutika ambayo kama ungefunua ndani ungegundua mwili ulikuwa na silaha zaidi ya kumi na mbili zilizokuwa zimefichwa kiunoni kuanzia bastola zenye uwezo mkubwa na vifaa vingine vingi vya kutumika kwenye eneo la mapambano.

"Mhhhhhhh kirahisi namna hiyo aliweza vipi kugundua kwamba maili kadhaa hilo eneo kulikuwa na watu wengi kama ulivyosema?" Kuna sehemu Malek Salem alikuwa anaachwa hakusita kuuliza ili aelewe kwa usahihi, swali lake lilimfanya mzee huyo ambaye alikuwa hana hata tone la kuigiza la wasiwasi amtazame tena na kutikisa kichwa chake kana kwamba alikuwa anasikitika baada ya kuona raisi huyo vitu vingi mno alikuwa yupo nyuma hususani kwa akili na haikutakiwa kabisa mtu mzembe kama huyo kuweza kuliongoza Taifa hiyo ilikuwa ni dalili mbaya.

"HISIA, hii ndiyo silaha kubwa sana ya watu wa kazi hususani makomando ambao huwa wanaandaliwa kwa ajili ya kazi maalumu, kwa tafsiri ya kisayansi huwa kuna milango mitano ya fahamu na imethibitishwa kwa weledi sana ila tofauti sana kwa hawa viumbe wao kwao milango ya fahamu sio mitano bali huwa ni sita hapo ndipo unapo ongezeka huo wa hisia na ndio huwa mlango wao wa fahamu wa mhimu zaidi ambao huwa wanautumia kufanyia maamuzi, huwa wanaziamini hisia zao kuliko mtu yeyote yule haijalishi ni nani ila hisia zake zikimtuma kwamba jibu ni Z hata aje mama yake mzazi amwambie kwamba jibu ni Q hawezi kumuelewa na hayo ndiyo maisha yao ya kila siku.

Sasa utajiuliza hizo hisia zinawasaidiaje kuyajua matukio ya hatari namna hii? Usijichanganye na tezi ya Adrenalin ambayo huwa inamsaidia kila binadamu pale anapokuwa kwenye sehemu ya hatari, hawa watu hisia huwa zinatengenezwa kwa utulivu wa hali ya juu, huwa wanaandaliwa anakuwa na uwezo wa kuihisi hatari hata kabla haijamkaribia, mwili wake unakuwa kama kifaa cha umeme hauwezi kutulia kama kuna vitu vibaya vipo karibu yake lazima kuna ishara atazipata kupitia mwili wake kama mwili kumsisimka sana, vinyweleo vya mwili wake kusimama, sikio kucheza na hata pua kutikisika zipo nyingi sana na huwa zinatofautiana kulingana na mhusika mwenyewe na aina ya mafunzo ambayo yeye anayo. Sio kila mtu anaweza kupatwa na hii hali ila kuna watu wachache ambao huwa wanachaguliwa na ndio huwa wanapewa mafunzo ya namna hii ambapo kwa baadae huwa wanakuwa watu wa hatari sana na ndiyo sababu sio kila mtu anatakiwa kuyapata haya mafunzo, huwa wanakuwa na uwezo wa kusikia hata hatua ya unyayo kwa umbali mrefu sana, au hata kama mtu anahema kidogo mno wanaweza kumsikia pale wanapokuwa kwenye hali ya utulivu, mapigo ya moyo au mjongeo wowote ule wa binadamu au kitu kitoacho sauti hata angekuwa wapi kama yupo kwenye eneo ambalo litakuwa halina viumbe wengi wa kuichanganya akili yake basi ni lazima akusikie tu.

Nadhani sasa umeelewa kwanini aliweza kutambua uwepo wa watu wengi maili kadhaa kutoka hiyo sehemu aliyokuwepo.(Aliweka kituo na kumwangalia raisi huyo kwa usahihi ambaye aliishia kuitikia kwa kutikisa kichwa tu aliamini kulikuwa na watu halafu kulikuwa na viumbe wa kutisha kimojawapo ndicho hicho ambacho alikumbana nacho kwenye hii stori alitamani sana kupata mtiririko mzuri wa kuelewa chimbuko la huyu mtu na namna alivyoweza kuwaua viongozi wake na kutenda unyama ambao mpaka leo imebaki kumbukumbu ya kutisha zaidi ndani ya taifa hilo).

THE HORROR WILD PATH
Ni kibango kidogo sana ambacho kilikuwa juu ya mti alikiona, mahali ambapo kilihifadhiwa sio kila mtu mwenye haya macho ya kubahatisha angefanikiwa kukiona kwa weledi, alitabasamu baada ya kugundua kwamba alikuwa mahala sahihi kabisa na wala hakukosea aliifuata njia ambayo ilikuwa inaelekezwa kwenye hicho kibango, alikuwa akitembea kwa tahadhali sana kwa sababu ilionekana kuwa sehemu ya watu wa kutisha japokuwa hakuna mtu ambaye aliwahi kuthibitisha kwamba hilo eneo walikuwa wanaishi watu kweli na ndiyo sababu ambayo ilifanya ikawa ni ngumu sana kushindana na hao watu hata makazi yao rasmi yalikuwa hayajulikani kabisa kwamba ni wapi wapo . Kwa takribani nusu saa ilipita akiwa anatembea baada ya kufika sehemu ambayo ilikuwa na mti mkubwa sana mapigo ya moyo yaliongezeka akajibanza kwenye mti kwa haraka ni kweli alipishana na mshale mkali ambao ulipita pembeni ya jicho lake na kwenda kukita kwenye mti ambao ulikuwa upo mbele yake. Hakutaka kukurupuka ndiyo sababu alitulia kwanza ili ajihakikishie kama wapo wangapi alitoa kisu chake kilichokuwa kinang'aa sana akakiweka pembeni majira hayo ya jioni ili kiweze kuakisi watu ambao walikuwa wapo upande ambao alikielekezea ila haikuchukua hata sekunde moja kilitawanyishwa kwa risasi mwanaume akaamua kujitokeza hadharani.

"Ni nani wewe na unatafuta nini kwenye haya maeneo?" Ni sauti ambayo iliyoanza kuchanganyika kama vile ni sauti ya mnyama huenda ni kwa sababu mtu huyo maisha yake yalikuwa ya porini sana, alitokea kwenye mti mrefu sana akatua chini akiwa ana bastola nne kwenye kiuno chake aliruka mpaka chini, wakati Aariz anamwangalia mtu huyo alitokezea mwanaume wa pili kutoka pembeni ambaye alikuwa ameshika upinde kwenye mkono wake na bila shaka ndiye alikuwa amerusha mshale ambao ulimkosa, alitaka kunyanyia mdomo wake mbele yake aliibuka mtoto wa kike kutokea ardhini ambako ilionekana ni wazi kulikuwa na shimo ambalo alikuwa amejifichia humo, alitabasamu baada ya kugundua walikuwa wachache tu hao watatu.

"Mna muda gani tangu muanze kuishi haya maisha na mnaishi huku ili iweje wakata kuna maeneo mengi sana ya watu kama nyie kuishi huko mjini?" Aariz au waweza kumuita Zakaria huku Tanzania wanamwita Alen aliuliza akiwa anasogea sehemu ambayo alikuwa amesimama mtoto wa kike aliye ibuka kutoka chini ya ardhi usoni alikuwa mweusi kama vile amepaka masizi ila kwa nyuma alionekana kubeba kifurushi ambacho kingewatatiza wanaume wengi sana kama angekuwa maeneo ya mjini ambako hicho kitu huwa ni ugonjwa wa watu wengi sana.

"Mhhhhhhh umeingia bila taarifa kwenye himaya za watu hilo ni Jambo la hatari sana kwa mara ya kwanza nilijua huenda ni mwenzetu ila nimeshtuka baada ya kukuona upo tofauti sana, sasa huenda utayaokoa maisha yako kwa kutupa sababu ya msingi kwamba umefuata nini huku eneo ambalo wanadamu wa kawaida hawaruhusiwi kabisa kuingia" aliuliza Yule mmoja ambaye kwa mara ya kwanza ndiye aliye tokeza akiwa na bastola mkononi.

"Ok mm nahitaji kukutana na kiongozi wa hili kundi lenu la kigaidi la Alih the Salijah of Jazirah" aliongea bila wasiwasi wowote japo maneno yake yaliwafanya wale watu wote watatu waangaliane na kukonyezana kana kwamba walikuwa wanazungumza kwa macho yao. Risasi tatu zilitoka kwenye bastola ya yule mwanaume huku akiwa anakuja kwa kasi sehemu aliyokuwa yupo Aariz, hata yule mwenye upinde aliachia mishale mitatu kwa nguvu kwa wakati mmoja akiwa anakuja kwa kasi ya ajabu lakini hata Yule mwanamke aliyekuwa na bisu kubwa mkononi mwake alihesabu moja, mbili......alijirusha kwa nguvu kuelekea mahali ambapo alisimama Aariz kwenye kiza cha wasitani ambacho kilikuwa kimeanza kutanda kwenye hayo maeneo.

Risasi tatu, mishale mitatu, na watu hatari watatu vyote vilikuwa vinakuja kwa pamoja kweye mwili wa mwanaume mmoja tu ambaye alikuwa amewekwa kati.......kipi amekifuata kwenye hili pori la kupandwa?, Huyo kiongozi anaye mhitaji ni kweli yupo huku? Je nini kinamkuta katikati ya hawa watu?? .....binafsi 13 niseme nakusanya nyaraka zangu tukutane ukurasa wa 14.

UKURASA WA KUMI NA NNE

TULIPO ISHIA UKURASA WA KUMI NA TATU

ENDELEA.......................
Kitendo cha kufumba na kufumbua macho mbele yao hakukuwa na mtu yeyote yule zaidi ya mshale mmoja ambao ulienda kukita kwenye mti hata mwanamke huyo ambaye alikuwa na bisu kubwa kwenye mkono wake akiwa anaenda kumshambuliza Aariz kwa spidi kali aliishia kuchoma ardhini tu hakuambulia chochote kile, hiyo hali iliwashtua wote watatu walibaki wanaangaliana bila kupata majibu sahihi kwamba mbele yao alikuwepo mtu halafu ghafla sana akapotea walijaribu kuhusisha hilo jambo na nguvu za giza lakini walikuwa ni watu hatari mno nguvu za giza huwa hazifanyi kazi mbele yao. Mwanamke huyo alifumba macho yake na kutuliza sana akili na kuziacha hisia zifanye kazi yake akaanza kuvuta hisia kwa lazima kana kwamba anarudisha matukio yote ambayo yametokea kwa muda mchache hapo nyuma, mbele yake alikuwa anaona picha ya namna mtu yule alivyokuwa amesimama mishale mitatu ikiwa inakuja kwa nguvu pamoja na risasi tatu ukijumlisha na wao watatu walivyokuwa wanakuja kwa nguvu, hisia zilimpelkea kuona namna mwanaume huyo alivyojigusa kwenye eneo lake la bega la kulia vilichomolewa visu viwili na panga moja kwa spidi ambayo macho ya kiumbe cha kawaida yasingeweza kuhisi uwepo wa utofauti wowote hilo lilimpa onyo kuhusu spidi ya huyo mwanaume namna anavyokuwa na kasi kubwa anapokuwa anahitaji kujitetea mwenyewe

Visu viwili vilitupwa kwenye risasi mbili na kuzikinga kwa ujumla lakini kuna swali moja alijiuliza kwanini havikupiga kelele aliweka kiporo kwanza, ule upanga mmoja ulimalizana na risasi ya tatu kwa upande wa mishale aliona mwanaume huyo wakati anaachia visu hivyo na upanga wake alikuwa tayari amejiburuza chini na kuteleleza ungedhani hiyo sehemu mvua ilikuwa imenyesha lahasha ni uwezo tu wa huyo mwanadamu ulifanya Kila kitu kionekane cha kawaida tu mbele yake, baada ya kujiburuzisha hivyo aliruka sarakasi kwa spidi na kuidaka mishale miwili Kisha mmoja aliukwepa ukaenda kukita kwenye mti. Hisia zake ziliishia hapo sasa alihitaji kuhakikisha kama je ni kweli huo mshale upo kwenye ule mti ambao aliuona? Alisogea hatua kumi mbele mpaka kwenye mti ambao mshale wa kwanza ulio mkosa Aariz wakati wanaingia hapo ulikita raundi hii aliikuta mishale iko miwili na sio mmoja tena basi moja kwa moja aligundua kwamba alichokuwa anakiona kwenye hisia zake ni cha kweli hakuna hata kimoja ambacho alikuwa amekikosea mpaka hapo alielewa huyo mtu yupo karibu sana na hilo eneo na huenda ni hatari mno kwao aligeuka taratibu sana mwanamke huyo akiwa makini sana aliangalia pembeni aliona mwenzake mmoja akiwa anaangalia juu ya mti akajua wazi anamtafuta mtu huyo lakini alivyokuwa anageuza macho yake kwenda upande wa pili ambako alikuwa yupo mwanaume mwingine alimuona mwenzake akiwa amesimama anaangalia mbele lakini nyuma yake alikuwa yupo mtu mwingine alijua wazi ndiye huyo, kwa wepesi alihitaji kumpa ishara mwenzake ni kama alikuwa amechelewe aliona tu mshale unazamishwa kwenye shingo ya mwenzie na kumtoboa vibaya sana alikufa akiwa hajui kama nyuma yake kulikuwa na mtu amemsimamia.

"Mhhhhhhhh unawezaje kuyafanya haya mambo kwa wepesi sana namna hii?" Yule mwanamke aliuliza akiwa anamwangalia Aariz vizuri sana kana kwamba walikuwa wanasomeana namna ya kuvamiana hiyo ndiyo sauti ambayo ilimshtua yule mwenzake ambaye alikuwa anaangalia juu ya mti ilimfanya ashtuke sana baada ya kuona mwenzie yupo chini akiwa kimya kabisa na karibu yake alisimama huyo mwanaume ambaye ndiye waliyekuwa wanamtafuta mpaka muda huo

"Usiseme kwa wepesi kana kwamba unaweza nawewe kuyafanya haya mambo ni wanadamu wachache tu kati ya mamia ambao wanaweza kuyafanya kwenye dunia hii IMPULSIVE CHOP-CHOP hii ni aina mpya ya mapigano ambayo imetambulishwa duniani kwa mara ya kwanza miaka miwili iliyopita na mchina mmoja hivi anaitwa TIENG ZU huyo ni moja ya walimu wangu walio nifundisha nikiwa huko China ni mtu ambae huwa hacheki kabisa kiufupi ni mkatili mno na ndiye mgunduzi wa hiyo staili mpya na mimi ndiye mtu wa kwanza kabisa kuijua baada ya yeye kiufupi ni kwamba mimi ndiye mwanafunzi wake wa kwanza kumfundisha aina hiyo ya mapigano, ni kitendo ambacho mtu anafanya maamuzi ya haraka kuliko hata akili yake inavyo fanya kazi, unafundishwa kuwa mwepesi kuliko hata karatasi na mazoezi yake yanaweza kuufanya moyo wako ukajaa maji na kukupelekea kifo, akili na nguvu vyote vinaenda kwa pamoja kiasi kwamba akili inafanya kazi tofauti na wanadamu wa kawaida na hapa wanahitajika watu wenye uwezo mkubwa sana kiakili ndiyo sababu sio Kila mtu anaweza kufundishwa hayo mambo lakini pia mazoezi ya nguvu ambayo kwa wewe hapo navyo kuona ulivyo mzito sidhani kama unaweza kumaliza hata masaa mawili kama hautakuwa umekufa basi utalala zaidi ya miaka mitano kitandani sasa mimi hivyo vyote vipo kwenye mwili wangu hivyo kwa watu wenye akili, nguvu na macho ya kawaida kama nyie naweza kuwaua wote hapa na asijue hata mmoja kwamba nimewaua mnakuja kushtuka mnapokuwa kwenye hatua zenu za mwisho mkiwa mnaipambania pumzi yenu ya mwisho. Nimefurahishwa sana na namna unavyo umiza kichwa baada ya kugundua namna nilivyozikwepa hizo silaha zenu pamoja na nyie wenyewe mpaka mkashindwa kunipata" Aariz aliongea akiwa mtu ambaye kwake tabasamu lilikuwa ni adimu sana kwenye maisha yake lakini alifanya hivyo kama kumjibu huyo mwanamke aina ya swali ambalo alikuwa amemuuliza hakuwa na wasi wasi wala presha wakati huo alikuwa anainama chini kuokota visu vyake ambavyo alivurudisha sehemu yake na kuushika upanga wake baada ya kuzibandua risasi ambazo zilikuwa zimenasa hapo.

Mwanamke huyo ilimuuma sana baada ya kuambiwa yeye alikuwa mzito sana kwake ilikuwa ni dharau kubwa sana lakini aliamua kumezea kwa kuamini hiyo dharau sio muda mrefu alikuwa anaenda kuilipa kwa mwanaume huyo na angeijutia hiyo kauli yake.

"Imewezekana vipi risasi hazijapiga kelele kwenye hivyo visu vyako wakati vinazuia hicho kitu?" Ni kitu ambacho mwanamke huyu alitamani sana kukijua tangu mwanzo baada ya kujiuliza namna risasi hizo zilivyoweza kupotea bila kupiga kelele baada ya kunasa kwenye hivyo visu vyake.

"Hivi sio visu ambavyo vinapatikana kama hivyo ambavyo mnavitumia kukatia nyama na nyanya majumbani kwenu, hivi ni visu maalumu ambavyo vimetengenzwa kwa sumaku, kazi yake kubwa huwa ni kusaidia kutolea risasi hususani kwa watu wa kazi kama sisi ninapo pigwa risasi mwilini mwangu sina haja ya kwenda kulazwa hospitali tena nakichukua hiki kisu nakigandamiza kwenye jeraha baada ya hapo kinalazimisha kuivuta risasi kwa nguvu na kuitoa nje kwa sababu vina sumaku kali sana ambayo huwa inavuta kitu chochote chenye asili ya chuma kama risasi japo kuna maumivu makali mno lakini kunakuwa hakuna namna ila pia ni silaha ambazo hutakiwi kukutana nazo kama nikizitoa kwenye mkono wangu zinasafiri kwa kasi ya ajabu ambayo kushindana nayo inahitajika mtu ambaye sio mzito kama mlivyo nyie hapo watatu" mwanaume wakati anamalizia tu maelezo yake alihisi upepo mkali unavuma unakuja alipo ni yule mwanaume mmoja ambaye alikuwa amebakia mkononi mwake akiwa na upinde wake alisikitika wakati huo alikuwa ameushika ule mshale mmoja kati ya ile miwili aliyo idaka wakati anapotea mahali hapo.

Alijivuta miguu yake kuelekea nyuma ungedhani kuna mtu anamvuta wakati huo alikuwa anaipunguza kasi ya yule mwanaume ambaye alikuwa na kasi ya kutisha akiwa anarusha mateke yake yote mawili, alivyo karibia mahali alipokuwa Aariz alijirusha juu sana lilikuwa ni kosa sana wakati anatua chini kumshukia mwanaume mguu wake ulikutana na ule mshale ambao kiuhalisia hakujua umerushwa muda gani alishuka bila balansi yoyote hakufikia chini shingo yake ilifikia kwenye goti la kulia la Aariz shingo ilipinda na kumfanya mtu huyo kutoa sauti ya uchungu kwa taabu vile visu viwili vilivyokuwa chini ya bega lake vilichomolewa na kuzamishwa kwenye shingo ya yule mwanaume alikufa akiwa hajabahatika hata kumgusa mwanaume huyo, mwanamke yule alijikuta anayafumba macho kwa kuushuhudia ule ukatili hapo alikuwa amebakia pekeake.

"Kuna muda nataka niamini kwamba wewe sio binadamu lakini hakunaga roboti la hivyo nina imani wewe ni mwanadamu wa kawaida tu kama tulivyo sisi hapa nimeshangaa sana namna ulivyoweza kuwaua kiwepesi wanaume wa kazi kama hao" mdada wa watu aliongea huku akiwa anautoa mnyororo wake wa chuma kwenye kiuno chake ambao ulikuwa na miiba ya chuma na kuukunja kwenye mkono wake wa kushoto mkono wa kulia akiwa na bisu lake kubwa ambalo alikuwa akiliamini mno.

"Hawa bado walaini mno mifupa yao ni dhaifu sana sidhani kama wanaweza kuhimili hata ngumi mbili tu, nina masaa nane ya kukaa huku baada ya hapo inabidi nirudi nyumbani ambako nimemuacha mke wangu akiwa mjamzito na nina imani muda wowote atanifanya niitwe baba, ni mwanamke ambaye sijawahi kumkoromea wala kumgusa hata kibao kwa sababu nampenda sana hivyo ninapo kuona mbele yangu naona kama namuona mke wangu mkono wangu unakuwa mzito sana kuunyanyua kukupiga wewe hapo muda huu ulitakiwa uwe upo kumpikia mumeo ebu nambie haraka njia ya kwenda ninako enda huko then uondoke hapa nisikuone tena Wala tusije kukutana tena kweye mazingira kama haya sitakuja kukusamehe tena" mwanaume aliyaeleza vyema maelezo yake akiwa anasimama baada ya kufuta damu kwenye visu ambavyo alitoka kumuulia yule mwanaume pale chini.

Alishtuka baada ya chuma kumkosa kidogo tu kwenye shavu lake, teke zito lilitua kwenye kifua chake na kumrudisha hatua kadhaa nyuma aligundua mwanamke huyo alikuwa serious tofauti nayeye alivyokuwa anamdhania mara ya kwanza angeleta masiara angejikuta kwenye wakati mgumu aliuweka sawa mkono wake akakanyaga chini kwa nguvu majani yalipeperuka kwa nguvu sana wakati huo huyo mwanamke alikuwa anakuja kwa kasi eneo alilokuwepo Aariz ule upepo wa majani ulimzonga usoni ikamlazimu kuzuia kwa mikono huku akipunguza spidi alikutanishwa na goti la kidevu aliachia kila alichokuwa amekishika kwenye mkono wake na kwenda kujibamiza kwenye mti mkubwa uliokuwa upo pembeni, alitua chini huku akishuhudia mguu wake ukivunjwa kama mtu anavunja muwa mmoja ili vipatikane vipande viwili kimoja ampatie rafiki ake, alibaki ameduwaa akihisi ni ndoto ya kufikirika maumivu makali ndiyo yaliyo mshtuka kutoka kwenye hiyo ndoto ya kweli kabisa alipiga makelele akiwa anamwangalia mwanaume huyo kwa hasira lakini hakuwa na cha kufanya alilaani sana hali hiyo ambayo ilikuwa inamtokea mahali hapo kwa huo muda, mwanaume alikaa pembeni yake akiwa anamwangalia kwa masikitiko mwanamke huyo ambaye alimuonya mapema lakini kujifanya anao uwezo mkubwa wa kupambana naye ndicho kilicho mpelekea kwenye hayo majuto.

"Mimi huwa sio mtu wa kujielezea sana wala kuongea ongea huenda ni kwa sababu ya maisha ya pekeyangu ambayo nimelelewa tangu nimeanza kujijua kwenye huu ulimwengu na hicho ndicho kitu ambacho kimenifanya kutokuwa mtu wa majigambo sana wala kujisifia ila kiuhalisia mimi nikiamua kupigana sitakiwi kupigana na binadamu wa kawaida kama wewe nina uwezo wa kumuua kwa sekunde thelathini na tano tu binadamu ambaye kidogo anafanya mazoezi kama nyie ila kwa wale wa kawaida kabisa sekunde tano huwa ni nyingi mno, inaniuma sana kumfanyia hivi mwanamke sipendi ila sina namna, mwanamke ndiye kiumbe pekee ambaye alinitoa kwenye upweke na kunifanya nikatabasamu kwa mara ya kwanza kwenye maisha yangu na huyo huyo mwanamke muda sio mrefu anaenda kunifanya nakuwa baba usije ukarudia tena kufanya kitu kama hiki" mwanaume alitamka kwa sauti yake nzito mno huku akiwa anatoa kikopo kidogo cha maji ya baridi sana kilichokuwa mithili ya barafu hata mwanamke huyo baada ya kukigusa alishangaa mwanaume huyo aliwezaje kukaa nacho muda wote huo kwenye mwili wake. Hayakuwa maji kama yalivyokuwa yanaonekana ilikuwa ni dawa ya kutuliza maumivu ule ubaridi wake ulimfanya mwanamke huyo aheme kwa nguvu sana baada ya kuyanywa mguu ulikuwa umevunjika lakini hakusikia maumivu kwa wakati huo alijihisi kuwa nafuu sana mwanaume alikuwa amekaa pembeni yake naye alipiga funda moja la hayo maji ya baridi sana ambayo kiuhalisia ilikuwa ni dawa Kisha akairudisha pale ilipokuwa mara ya kwanza.

"Unaweza kupigana kwa muda gani?" Ni swali ambalo lilimshangaza Aariz kutoka kwa mwanamke huyo.

"Kwanini unaniuliza swali kama hilo?"

"Nimefungua hilo lango hapo mbele mkono wa kushoto ambapo ni miti huwa inashonana tunatumia antidote ambazo zimetengenezwa kwa damu yangu pia huwa kuna miale ya umeme ila kwa sasa utaweza kuingia hapo ila baada ya hapo kuna mlango mkuu wa kuanza kuingilia kambini mlango huo unalindwa na kiumbe kimoja hivi ni binadamu ila mara nyingi huwa anapigana kwa mkono mmoja kama akiitumia mikono yake miwili inakuwa ni ngumu kwa mtu kumaliza hata sekunde arobaini na tano sasa huyo mtu jicho lake ndiyo nywila ya kufungulia kwenye ile miale ya lango la kuingilia kambini, pembeni ya jiwe kuna alama nyekundu hapo ndipo ilipo lock ya mlango jicho lake likiwekwa hapo ndipo miale hiyo hupotea na mlango unafunguka, kumpata mwanaume huyo ni lazima upige mluzi mara mbili ndipo huamka maana huwa ni mtu wa kulala sana" alielezea kwa urefu sana mwanamke huyo na kumpa tahadhari mapema Aariz.

"Kwanini unaniambia yote haya?"

"Nimeua watu wengi sana sio kwa kupenda ila kwa sababu ya maisha yangu nimelelewa kuua tu nilitamani sana kutoroka ili niachane na hii kazi ila kilikuwa ni kitu ambacho hakiwezekani, huko ndani kuna binadamu ambao wameishi maisha yao yote kwa ajili ya mapigano kunatisha hata kutazama namna wanavyo waua watu huo ndio msaada wangu kwako kukuelekeza namna ya kufika huko na kama utabahatika kutoka ukiwa hai basi utakuwa binadamu mwenye bahati kubwa sana" alimaliza maelezo yake na kujing'ata juu ya ulimi povu lilianza kumtoka mdomoni sekunde mbili tu alipoteza maisha. Aariz alielewa kwamba mwanamke huyo alikuwa amejiua mwenyewe aliishia kusikitika tu baada ya kuona saa ambayo mwanamke huyo alitumia kufungulia hayo malango ya siri huko porini, aliichukua akamfumba macho kisha akabeba vifaa vyake na kuanza kuelekea ulipo huo mlango.

Atatoka kwa mafanikio huko aendako? Nadhani umeanza kidogo kumjua huyu mchimba madini wa Arusha uhalisia wake ulivyo. Ilikuja kuwaje mpaka akachimbe madini Tanzania?.....14 naweka kalamu chini nasema bye-bye

Bux the story teller
 
Habari, ni matumaini yangu mpo wazima wa afya kabisa.

Leo ni siku nyingine njooni msome hadithi huku mkiburudika na ofa ambazo hazielezeki kirahisi.

1. ULIMWENGU WA WATU WABAYA kipande kimoja ni shilingi mia tu za kitanzania (100).

2. I WANT TO DIE JUDGE...kipande kimoja shilingi mia tu za kitanzania, lakini pia leo GEREZA LA HAZWA Leo natoa ofa ya Pekee.

3. GEREZA LA HAZWA.....Leo kipande kimoja kinauzwa 100 badala ya 150 hii ni kwa leo tu, ipo mpaka 82 kwa sasa.

Namba za malipo ni zile zile
0621567672 (WhatsApp)
0745982347

Zote jina ni FEBIANI BABUYA, natuma Kote WhatsApp na kwa wale wa simu ndogo natuma messenger Facebook.

Njoo uburudike na kalamu yangu.
Kama naitaka yote kiasi gani

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
UKURASA WA KUMI NA TANO

TULIPO ISHIA UKURASA WA KUMI NA NNE

ENDELEA..............................
Baada ya kuingia ndani ya yale malango ya siri ambayo yalikuwa yanafunguliwa na watu maalumu ile sehemu ilijifunga tena hakushtuka ni kama alitarajia hicho kitu alitembea kwa hatua thelathini kukawa na ukimya ulio mpa shaka hiyo sehemu haikusikika hata sauti ya ndege akipiga kelele inamaanisha hata mjongeo mdogo tu wa kitu ilikuwa ni rahisi sana kuusikia, alipiga mluzi kama alivyokuwa ameelekezwa kwa mara ya kwanza hakukutokea kitu chochote ilimbidi kurudia tena kufanya hivyo kuna mwanaume alifumbua macho yake kwa spidi na kunyanyuka kwa staili ya kutisha akidogo ambayo ungedhani kuna mtu alikuwa anamsukuma mgongoni. Visu vidogo sita vilikuwa vinakuja kwa spidi kali mno utulivu wa lile eneo ndio ulio mhankikishia uwepo wa vitu vingine hapo alikimbia kuelekea mbele ya mti mdogo uliokuwa mbele yake aliupanda kwa kutumia miguu yake alijirusha sarakasi ya nyuma visu vikiwa vinamkosa na kugonga kwenye mti huo ila bahati mbaya sana kisu kimoja kilimbaraza kwenye kiganja chake cha mkono na kumpatia maumivu kiasi akifanikiwa kutua chini japo alikutana na bahati iliyokuwa mbaya sana alikuwa anaelea juu juu kwa mtama mzito ambao alipigwa alijaribu kujizungusha alichelewa ngumi tano zilizama kwenye mwili wake akiwa bado hajatua chini teke lilizamishwa kwenye mbavu zake akawa anaelekea kwenye mti mkubwa hapo angejigongesha vibaya sana mwanaume aliitumia miguu yake kujigeuza na kudunda kwenye mti huo akasimama vizuri baada ya kutua chini nwili wake kiasi fulani alihisi maumivu makali angekuwa mla chipsi wa magomeni tungesha msahau habari yake ingeishia hapo hapo.

Kulikuwa na kiza kwa sababu ilikuwa tayari ni usiku ila kulikuwa na miale ya mwanga wa kutosha ambayo ilikuwa inatumika kama taa za ulinzi ila cha ajabu ukiwa nje huwezi kuona aina yoyote ile ya mwanga hivyo walikuwa wanaonana kwa usahihi, mbele yake alisimama mwanaume mmoja ambaye alikuwa na suruali kubwa sana pamoja na buti juu yake alivaa vesti nyeusi, usoni alikuwa ana rangi rangi ambazo bila shaka ni tattoo ambazo alikuwa amezichora mwenyewe kama pambo, mikono yake ilikuwa imegawanyika kwa usahihi ni mwanaume wa kazi haswa alikuwa, huyo ndiye alipewa maelezo kwamba anatakiwa kumalizana naye ili aweze kuingia ndani kwani yeye ndiye alikuwa ufunguo kwa kutumia jicho lake na hiyo siri waliijua wachache sana na kama sio yule mwanamke kumwambia basi angetwanga maji kwenye kinu.
Aliangaza macho kwa umakini kwa sekunde chache za kuhesabu mkono wake wa kulia mita kama kumi na tano kutoka hapo alipokuwa amesimama aliona kuna jiwe kubwa kiasi ambalo lilikuwa linawaka alama nyekundu kwa pembeni yake alitabasamu baada ya kuelewa kwamba hilo ndilo alipaswa kutumia kuingilia hapo vinginevyo angeuliwa na mionzi mikali ya umeme ambayo kwa macho ya kawaida usingeweza kuiona kabisa.

"Who are you (wewe ni nani)?" Aliuliza yule mwanaume akiwa anaufunga vyema mkono wake kwa kitambaa kigumu baada ya kumkosa mwanaume huyo aliyekuwa mbele yake kwa takribani visu sita.

"I'm an innocent citizen who purposely is here to rescue his country from demise( )" alijibu kijasiri sana akimaanisha alikuwa ni raia asiye na hatia yoyote ambaye yupo pale maalumu kwa ajili ya kuliokoa taifa lake kutoka kwenye kupotezwa.

"Which country are talking about dude, do you know exactly who are the people who sent you ? Hahahaha haha ok let me kill this idiot who calls himself an innocent citizen" alicheka kwa dhihaka sana wakati anamuuliza Aariz kwamba anaizungumzia nchi gani na kumuuliza kwa msisitizo kwamba anawajua vizuri watu walio mtuma? lakini hakujali sana akamalizia kwa kujisemea acha amuue huyo mpumbavu ambaye binafsi alikuwa akijiita raia asiyekuwa na hatia. Kisu kimoja alikiweka mdomoni bastola zake tatu alizitoa kwenye kiuno chake na kuzitupa chini kwa dharau hilo ni kosa ambalo angelijutia maisha yake yote kwa yale mapigo ambayo alimpiga Aariz kwa mara ya kwanza yalimpa uhakika kwamba ni mrahisi kama maharage ya Mbeya maji mara moja tu hivyo kutumia silaha kwa mtu dhaifu kama huyo ungekuwa ni uonevu hakujua alifanyalo yule mwanadamu. Alijikusanya na kuhesabu mara moja mara mbili mara tatu nguvu alizokuwa nazo wakati anakuja alikuwa ana uhakika hiyo ngumi ingemtawanyisha na kumlaza mtu ambaye alikuwa mbele yake, lahaula alipiga hewa alishtuka sana hakuna mtu ambaye alikuwa ana uwezo wa kupigana naye na akaikwepa kasi ya ngumi zake, alihisi kwa nyuma kuna mtu aligeuka kwa teke aina ya acrobatic double kick aliambulia kutua chini tu mtu ambaye alikuwa anatamani kummaliza kwa wepesi alikuwa yupo sentimita kadhaa kutoka pale ambapo yeye alitua.

Alimkadiria sana lakini hakummaliza mwanaume ambaye kiuhalisia alionekana kutokuwa mwongeaji sana, mara ya tatu wakati anajikusanya ili amfuate alikutanishwa na mateke mawili na ngumi nne kwenye mwili wake alihisi kama kuna viungo vimevunjika baada ya kudondoka chini, mwili ulikuwa mzito sana alihisi kama anaona kiza kuna kidonge alikitafuna haraka kwenye mdomo wake akanyanyuka ni wazi kilikuwa kinatumika kuongeza nguvu.

"How is this possible winning me by just one punch? Noooooooo" alipiga makelele na kuipanga mikono yake tayari kwa mapigano sasa Aariz naye alitulia na kuukunja mikono yake ngumi nzito zilikuwa zinarushwa kutoka kwa hawa wanaume wawili usiku huo ambazo zilichukua dakika tano wakiwa wanarushiana kwa spidi yule mwanaume alianza kupoteza uelekeo kila ngumi ambayo ilikuwa inaingia kwenye mwili wake ilikuwa inamletea udhaifu mkubwa sana ndani ya sekunde zingine thelathini alikuwa amepiga magoti mbele ya mwanaume ambaye yeye wenyewe alimdharau na kutupa bastola zake chini akiamini kwamba visu pekee vingetosha kumuweka chini dharau zilimponza, aliangalia upande ambao bastola zake zilikuwepo ilikuwa ni mbali sana asingezifikia kwa wakati huo, alijiangalia mkono wake mmoja ulikuwa umetobolewa na kuvunjwa mmoja tu pekee ndio ambao ulikuwa unafanya kazi vizuri hatua za taratibu Aariz alikuwa anasogea pale alipo yule mtu.

"Nimepata taarifa zako chache kabla ya kukufikia wewe ni mwanaume imara sana ambaye ungelitumikia taifa lako vizuri basi ungekuwa mtu bora sana, leo nimeingia kwenye kitabu cha wauaji rasmi kwenye haya maisha sio kwa kutaka hapana ila ni kazi ambayo ipo mbele yangu ndiyo inanilazimu mimi kuwa hivi nikiwa bado kijana mdogo sana siijui hatima yangu ila sitaki kuacha wananchi wangu wakiteseka nikiwa bado nipo hai, nahitaji unitajie wakubwa wako nawapataje kwa sababu mnaonekana mnajua mnacho kifanya haiwezekani watu wa kawaida muwe mna ulinzi mkali wa namna hii na nchi haijui hili ni tatizo kubwa kwa taifa nahitaji kuwajua vizuri kwa haraka sana" Aariz aliongea kwa msisitizo akiwa amesimama mbele ya yule mwanaume ambaye ndiye alikuwa mlinzi wa hayo maeneo. Yule jamaa alikosea baada ya kutaka kumvizia Aariz ili achomoe kisu kwenye mwili wa Aariz, mwanaume aliruka juu kiasi kwani aliliona hilo alitua na teke ambalo lilimpata mwanaume huyo shingoni alijigonga chini na kutoa kelele za maumivu mkono wake mmojaa ambao ulikuwa salama ulidondoka chini baada ya kukatwa na upanga kisha mwanaume akaitoa bastola na kuishika kwenye mkono wake alimmiminia mtu huyo risasi kumi kwenye mapaja yake yote mawili alikuwa ni kilema huyo tayari asingeweza kufanya mjongeo wowote ule alimwangalia kwa hasira sana zilizokuwa na utulivu ndani yake akairudisha bastola mahali pake akiwa ameushika upanga wake kwenye mkono akasogea mahali alipo yule mwanaume akachuchumaa na kumshuhudia namna alivyokuwa mgumu licha ya hayo yote kumtokea lakini hakutoa tena sauti bali alikuwa alikuwa akigugumia kwa maumivu kimya kimya tu.

"Kwenye maisha yangu sipendi sana kuongea ongea ndio maana mimi mwenyewe huwa sio muongeaji sana ila unapo nilazimisha mimi kuwa muongeaji sana madhara yake ndiyo haya, usijione wewe ni bora sana mbele ya watu ambao hauwajui ulitakiwa kunijibu kistaarabu tu wala tusingefikia kote huku ila dharau yako ndiyo imekuponza mpaka yamekuwa yote haya ziangalie sana kauli zako, nahitaji unitajie kila kinacho endelea huko ndani mara moja" Aariz hakuwa na masihara sana kwenye kauli zake hivyo aliamini mwanaume huyo ni lazima atakuwa amemuelewa vizuri kabisa.

"Kwa usalama wako ondoka hapa muda huu kabla mambo hayajaharibika huko ndani huwezi kufanikiwa kutoka ukiwa hai"

"Mhhhhhh usidhani nimekuja hapa kwa kubahatisha kama unavyo fikiria wewe hapo hata huko nje nilikotoka niliambiwa wewe ni mtu hatari sana lakini nadhani umeona kilicho kutokea hapa muda huu" mwanaume huyo alimeza mate maana alichokuwa anaambiwa kilikuwa cha kweli kwa asilimia zaidi ya miamoja.

"Huko ndani kuna watu zaidi ya miambili ambao wote ni wanajeshi iila kati ya hao kuna watu kumi na wawili tu ndio watu hatari sana na huwa wanatumika kwa kazi maalumu hasa pale inapohitajika kutumia nguvu kubwa, watu hao huwa wanakaa sita sita ukisha ingia hapa utakutana na walinzi wa kawaida tu ila baada ya hapo utakutana na hao sita kati ya hao kumi na mbili na wanajeshi wengine saivi lazima wamelala kwa sababu hakuna hatari yoyote ambayo imehisiwa kuwepo kwa takribani mwaka sasa hali hiyo imepelekea kila siku wawe wanawahi sana kulala na sheria ipo hivyo kwahiyo hapo utakutana na kambi ya kwanza hiyo haina tatizo sana kwenye hiyo kambi kuna jumba moja kubwa sana ambalo limejengwa mithili ya tanki la maji ni kubwa mno humo ndo kuna silaha za kila aina. Ni kweli ukiingia humo utakutana na maji ya kweli kabisa ila maji yapo chini sana kwa juu yake pembeni kuna mlango ambao unafunguka wenyewe kila baada ya dakika tano na kufunga kila baada ya dakika tano ukiingia huko kuna ngazi za kwenda ardhini hilo ndilo ghala linalotumika kuhifadhia silaha zote ambazo zinatumiwa na kundi hili.

Ukitoka hapo utakutana na fensi ya waya ukifanikiwa kuivuka hiyo huko ndiko aliko mkuu wa hii kambi kuna nyumba moja nzuri sana humo ndimo anamoishi yeye kabla ya kuifikia nyumba hiyo mkono wa kulia kuna jengo kama gudauni kubwa humo kuna mateka wapatao miamoja ambao ni wanawake na kazi yao ni kuwaburudisha wanaume humo ndani na hutumika kama chombo cha starehe ila mkono wa kushoto mkabala na nyumba ya kiongozi kuna gudauni lingine ambalo limejengwa kisasa humo kuna wanajeshi wengine huwa wanaishi kwa siri sana sasa hapo ndipo utakuwa moja kwa moja unatazamana na nyumba ya kiongozi ambamo humo kabla ya kukutana naye yeye unapaswa ukutane na hao wanaume wengine sita wanao kamilisha kundi la hao watu wa kazi 12 huwezi kumgusa huyo kiongozi kabla hujakutana nao hao watu sitaki kukutisha ila sina imani kama ni wanadamu wa kawaida" alijikohoza kidogo kupooza maumivu baada ya kutoa maelezo ya huko ndani ambako mwanaume huyo alihitaji kuingia kwa lengo la kulimaliza kundi hilo lakini pia alimhitaji sana huyo kiongozi wa hao magaidi ambaye ndiye huwa anasababisha vita na amejimilikisha hilo eneo la kusini mwa Libya.

"Mhhhhhh huyo mtu ameoa au ana familia?"

"Yes ana familia mtoto wake ni miongoni mwa hao wanaume sita ambao utakutana nao wanamlinda huko ndani, hakuna taarifa za wazi sana kuhusu mama wa mtoto huyo japo inasemekana alimuua mwenyewe ila kwa sasa ana wanawake kumi ambao anaishi nao ndani kwake kama wake zake"

"Huwa anafanikiwa vipi kuyabeba mafuta kuyasafirisha nje wakati mipaka ya nchi inalindwa?"

"Mimi sina nafasi kubwa sana ya kuweza kujua mambo ya mhimu ila inasemekana kuna viongozi wakubwa serikalini ndio wamemuweka hapo ndio maana anaweza kufanya chochote na hakuna mtu atajua wala kumgusa, taarifa huwa zinatoka serikalini na kumfikia mapema sana hata wewe nimeshangaa sana ujio wako wa siri hapa ndani haijawahi kutokea" sasa hapo Aariz kuna vitu vilikuwa vimeanza kuzunguka kwenye kichwa chake ndiyo sababu huyo mtu alikuwa na uwezo mkubwa wa kutengeneza miundombinu mikubwa kama hiyo huko msituni kulikuwa na watu wakubwa serikalini ambao walikuwa wanamtumia, kwa maelezo aliambiwa kwamba raisi ndiye aliyekuwa akishirikiana naye lakini walimuua na alisikia kutoka kwa waziri mkuu sasa ni nani hasa mwingine alikuwa yupo nyuma ya hili? Hakukuwa na mtu wa kumpatia jibu hapo alinyanyuka kwa nguvu na kuzamisha mkono wake kwenye sehemuya jicho la huyo mwanaume alilinyofoa jicho hilo kwa nguvu hali iliyo mpelekea mwanaume huyo kupiga makelele mengi sana akitapa tapa kuhitaji msaada.

Mwanaume alisimama na kuitoa bastola yake tena alikifumua kichwa cha huyo mtu bila huruma na kusogea pale kwenye lile jiwe alipachika lile jicho likiwa bado linacheza cheza kwenye mboni sekunde kumi tu alianza kuona mionzi mikali ikipishana na kurusha cheche baada ya muda palitulia na mlango mlaini mithili ya kitambaa ulijifungua rasmi alikuwa anaona kinacho endelea ndani sasa ndo alikuwa ameanza kuingia kwenye kambi yenyewe halisi ambayo ndiyo ilikuwa tageti yake kubwa.

Aariz kwenye mikono ya wanaume zaidi ya 200 mpori mpori wa Kagera huyu atapona kweli? Naweka kalamu pembeni sehemu ya 15 inafika mwisho niseme bye-bye.

Bux the story teller
316800359_134223399425483_2497697911145617876_n.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom