Punde hivi, nikiwa naskiliza kipindi chenu Power breakfast.
Nimekusikia Hando ukimuuliza Babra kama hua anatembelea Jamii Forums. Eventhough sikumsikia Babra akitoa jibu la moja kwa moja, kwamba hua anatembelea mara kwa mara, ama kwa nadra. Aidha nikakusikia ukimwambia Babra kwamba wewe (Gerald) unapaogopa sana Jf, kwa sababu watu wa hapa ni wakali mno!
Na kwamba ukileta mawazo yalio tofauti tu , kidogo na ya Ma'member wa hapa wanakuchambuaje!. Na hicho ndiyo kinachokufanya uwe unachungulia tu, na kuumwaga! Nichukue fursa hii kuwaambia karibuni Jamii Forums kwa mapana.
Hapa ni mahala salama, na pana mengi ya maana na ya faida tofauti na unavyofikiri. Achana na kuchungulia, tia maguu yote, mlete na babra, dinna, PJ, Gea, ikibidi na Jahazi lote livute lije.