TANZIA Geita: Madiwani wawili wateule wa CCM wafariki dunia

Sasa kama mnalijua hlo mbna mnauwa wenzenu???

Laiti ungewaza vizuri ungeondoa chuki kwa vyama na kudeal na wauaji.

Kwa hii style ya uandishi wako akatokea na mCCM mwenye style hiyo watanzania watachinjana ila bahati hao CCM wanafuata taratibu hawatukani wala kutuhumu vyama pinzani






Na huo ndio ustaarabu wa mtanzania
 
Hongereni wote mnaoshabikia misiba ya wenzenu na kuwaombea wengine wafe mkiwa nyuma ya keyboards. Mbarikiwe sana kwa kuweza kujipa moyo kwamba mna kibali cha kuishi duniani milele huku mkiwaombea wengine wafe.

Wengine tunaamini kwenye neno hili. "Lakini, juu ya siku au saa hiyo, hakuna mtu ajuaye itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye" Mathayo 24:36
Hao walompigia sim kama sio watu wake aweke mawasliano hapa. Hakuna anayetaka kumuua aache kujitisha

Ila kama anapenda kuishi ubalozini vile

Kwenye uzi wa Lisu uliandika hivyo.

Ni halali pia wengine kufurahia Vifo vya Madiwani wa CCM kama wewe ulivyofurahia Lisu kutishwa
 
Kwenye uzi wa Lisu uliandika hivyo.

Ni halali pia wengine kufurahia Vifo vya Madiwani wa CCM kama wewe ulivyofurahia Lisu kutishwa

Kwani Tundu amekufa nikafurahia???

Huoni kama hao wanaomtishia ni sawa wawekwe hadharani ili washughulikiwe?

Acha kujichanganya utachanganyikiwa bure
 
Haya sasa, uchaguzi mdogo kabla hata ya uapisho.
---
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita kimepata pigo baada ya madiwani wake wawili wateule kufariki dunia kwa nyakati tofauti wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumamosi Novemba 7, 2020 katibu mwenezi wa CCM mkoani Geita, David Azaria amewataja madiwani hao wateule kuwa ni Masalu Luponya (Bugalama) na Magomamoto Zanziba (Buziku).

Azaria amesema Luponya aliugua wakati wa kampeni na hata siku ya uchaguzi Oktoba 28, 2020 alipigiwa kura na wananchi akiwa amelazwa hospitali ya Bugando.

Amesema Magomamoto aliugua ghafla juzi na alipelekwa Bugando lakini alifariki saa chache baadaye.

Amesema Luponya atazikwa leo nyumbani kwake Bugalama huku taratibu za mazishi ya Magomamoto zikiendelelea kufanywa na chama hicho kwa kushirikiana na familia yake.

Magomamoto alikuwa diwani wa Buziku kuanzia 2010 hadi 2020 na mwaka 2010 hadi 2015 alikuwa makamu mwenyekiti wa baraza la madiwani.

Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Geita, Jonathan Masele amesema kifo cha Luponya ni pigo kwa CCM na jamii iliyokuwa ikimzunguka.

Luponya wakati wa uhai wake alikua akisomesha wanafunzi 50 wa sekondari na 20 wa ualimu sambamba na kutoa huduma mbalimbali za kijamii kwenye kata hiyo.

Chanzo: Mwananchi

Diwani mteule ameteuliwa lini?
 
Mods wanahariri hadi comments?Kama mimi sijaguswa na vifo hivi halafu nikasema wazi kabisa,kosa liko wapi?Hii JF imekuwa kituko kweli!
 
Ila huwa unashangilia wakipigwa watu risasi ?

Huwa nawashauri watoe ushirikiano kwenye vyombo sahihi ili hayo matukio yafanyiwe kazi.

Wasiwafiche mashahidi wala suluhu sio wakimbilie ubelgiji na kwenda kutoa taarifa BBC, Al Jazeera, DW.... na kwingineko ambako hadi sasa hawajawasaidia chochote
 
Back
Top Bottom