Maagizo matano yametolewa na katibu Mwenezi Taifa wa CCM Mkoani Geita

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,399
3,916
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda (@baba_kegan) amesema CCM imetoa maagizo matano kwa mkoa wa Geita ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi ili kuboresha maisha ya wananchi na kuchochea maendeleo.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Bwanga wilayani Chato amesema maagizo hayo ni;

1. Mkuu wa Mkoa ameagizwa kuwapokea, kuwaskiliza na kuchukua hatua za utatuzi kwa wafabyabiashara wa mkaa kwa yeyote mwenye kibali na alidhulumiwa kwa kupokonywa mikaa yake na hata usafiri wake.

2. CCM imetoa siku nne kwa TARURA, hadi kufikia Novemba 15, mkandarasi awepo Bwanga kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha daladala.

3. Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameelekezwa kuweka msukumo zaidi kukamilisha utekekezaji wa mradi wa Maji Bwanga kwani tayari shilingi bilioni 1.6 zimetolewa.

4. Wakala wa Umeme Vijijini (REA) umeelekezwa kukamilisha uwekaji wa taa za barabarani katika Kata ya Bwanga.

5. Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) umeelekezwa kuharakisha mchakato wa ujenzi wa barabara katika Kata ya Bwanga wilayani Chato.
 
Back
Top Bottom