TANZIA Geita: Madiwani wawili wateule wa CCM wafariki dunia

Huwa nawashauri watoe ushirikiano kwenye vyombo sahihi ili hayo matukio yafanyiwe kazi.

Wasiwafiche mashahidi wala suluhu sio wakimbilie ubelgiji na kwenda kutoa taarifa BBC, Al Jazeera, DW.... na kwingineko ambako hadi sasa hawajawasaidia chochote
Unajianika ujinga na ukatili ulionao ?
 
Haya sasa, uchaguzi mdogo kabla hata ya uapisho.
---
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita kimepata pigo baada ya madiwani wake wawili wateule kufariki dunia kwa nyakati tofauti wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumamosi Novemba 7, 2020 katibu mwenezi wa CCM mkoani Geita, David Azaria amewataja madiwani hao wateule kuwa ni Masalu Luponya (Bugalama) na Magomamoto Zanziba (Buziku).

Azaria amesema Luponya aliugua wakati wa kampeni na hata siku ya uchaguzi Oktoba 28, 2020 alipigiwa kura na wananchi akiwa amelazwa hospitali ya Bugando.

Amesema Magomamoto aliugua ghafla juzi na alipelekwa Bugando lakini alifariki saa chache baadaye.

Amesema Luponya atazikwa leo nyumbani kwake Bugalama huku taratibu za mazishi ya Magomamoto zikiendelelea kufanywa na chama hicho kwa kushirikiana na familia yake.

Magomamoto alikuwa diwani wa Buziku kuanzia 2010 hadi 2020 na mwaka 2010 hadi 2015 alikuwa makamu mwenyekiti wa baraza la madiwani.

Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Geita, Jonathan Masele amesema kifo cha Luponya ni pigo kwa CCM na jamii iliyokuwa ikimzunguka.

Luponya wakati wa uhai wake alikua akisomesha wanafunzi 50 wa sekondari na 20 wa ualimu sambamba na kutoa huduma mbalimbali za kijamii kwenye kata hiyo.

Chanzo: Mwananchi
Kwa kidhungu inaitwa double D....dabulo deefi.... huwezi kukata rufaa kwa kifo ..tuna tume_ccm,police_ccm n.k contrary hakuna mungu_ccm wasipumzike kwa amani.
 
Hakuna ajuae siku wala saa Mwenyezi Mungu aziweke mahala pema roho zao
Katika kitu ambacho sikiwezi kabisa ni kufurahia kifo cha binadamu mwenzangu
 
Kwa hivyo wewe utashi ulio nao unaamini kwamba Mungu yupo pamoja na watu wanao unga mkono ushoga Mkuu? Ndivyo unavyo amini hivyo. Kwa hivyo unaamini kwamba Mungu yupo pamoja na watu wasio amini kwamba Mungu anaweza kuondoa adhaa ya magonjwa yanayo zuka kiajabu ajabu.

Chukua hili andiko baada ya hapo ulisome.
Biblia ambalo ni neno la Mungu inasisitiza kila mara kwamba ushoga ni dhambi, Soma nukuu zifuatazo: Mwanzo 19:1-13; Mambo ya Walawi 18: 22; Warumi 1:26-27; Wakorintho wa kwanza 6:9. Warumi 1:26-27 inatufundisha ya kwamba ushoga ni njia mojawapo ya kumkana na kutomtii Mungu. Mtu anapodumu katika dhambi na kutokuamini biblia inatuambia ya kwamba Mungu huwaachilia kutenda maovu zaidi ili wapate kujua ubatili wa maisha bila Uwepo wa Mungu. Wakorintho wa kwanza 6:9 inasema kuwa mashoga hawataurithi ufalme wa Mungu.

Mungu hakuumba mwanadamu mwenye tamaa ya ushoga au binadamu shoga. Biblia inatuambia mtu huwa shoga kwa sababu ya dhambi. (Warumi 1:24-27), na pia kwa sababu ya uamuzi wake mwenyewe. Mtu anaweza kuzaliwa na msukumo juu ya ushoga kama vile watu pia huzaliwa na msukumo juu ya fujo na dhambi nyinginezo. Hili halihalalishi dhambi yoyote inayofanywa na wanadamu. Je, mtu akizaliwa na msukumo wa hasira mbaya, ni halali aendeleze hasira zake mbaya? La, hasha. Hata kwa ushoga pia si halali.
Mkuu unafikiri mtu anayeamuru watu wauwawe na wale ambao wanatakiwa kuwalinda (Ishu ya Zanzibar) unafikiri dhambi yake ina unafuu wowote? Tena hii ni mbaya zaidi kuliko hizo hisia zako eti mtu anashabikia. Mwizi wa kura hana tofauti na wezi wengine kama wale wa EPA,ESCRO, Vibaka, matapeli ama majambazi. Fisiem wamefanya dhambi zote hizo mbele ya macho ya Watanzania, wana unafuu wowote? Dhambi ili iwe dhambi sharti iambatane na tendo. Kushabikia bila kutenda hicho unachokishabia haiwezi kuwa dhambi yenye viwango sawa na muuwaji na mwizi (wa kura). Usisome maandiko huku moyoni umejaa ufisiem.
 
Hakuna ajuae siku wala saa Mwenyezi Mungu aziweke mahala pema roho zao
Katika kitu ambacho sikiwezi kabisa ni kufurahia kifo cha binadamu mwenzangu
Siku jiwe akifa nisisherehekee?Kwakweli ninaweza kujizuia kwa muda kama mtu aliyebanwa na cheko halafu akaibana,kadri sekunde zinavyoenda ndio unaanza kuona sura yenyewe inamkatili na hatimaye inaanguka cheko lenyewe!
Kuna watu wanatesa wenzao mpaka inafikia stage unawaombea mabaya,unasema bora wafe tu!

Ndio maana kuna ule wimbo kwamba ,"Idd Amini akifa,mimi siwezi kulia.Nitamtupa kagera awe chakula cha mamba"!

Hujaimba wimbo huo huko shule ya msingi?Mpaka inafikia hapo basi ujue watu wameumizwa sana!
 
Kwani Tundu amekufa nikafurahia???

Huoni kama hao wanaomtishia ni sawa wawekwe hadharani ili washughulikiwe?

Acha kujichanganya utachanganyikiwa bure
Hiyo ndio hali halisi ndio matunda ya chuki
 
Back
Top Bottom