Geita, Chato: Mkandarasi arudia upya barabara aliyojenga chini ya Kiwango

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Barabara Chato.jpg

Taasisi ya Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Geita imemrejesha kujenga upya barabara ya Makurugusi kwenda Musasa wilayani Chato yenye urefu wa Kilometa moja na nusu kwa gharama zake baada ya mkandarasi huyo wa kampuni ya M/S Runazi General Supplies Company LTD kudaiwa kujenga barabara hiyo chini ya kiwango na kusababisha barabara hiyo kuharibika vibaya siku chache baada ya kukamilika.

Akizungumza mara baada ya kutembelea barabara hiyo kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Geita, Leonidas Felix anasema wamelazimika kumrudisha katika eneo la ujenzi ili aweze kujenga barabara hiyo upya kwa gharama zake kutokana na kujenga chini ya kiwango na kusababisha wananchi kulalamika kutokana na ubovu wa barabara hiyo.

ITV imezungumza na mkandarasi huyo Pancian Gasper akiwa katika ujenzi wa barabara hiyo nakusema barabara hiyo imeharibika mara baada ya kukamilika kutokana na kusombwa na mafuriko hivyo akalazimika kuijenga upya ili kutekeleza maagazo ya TAKUKURU.

Mhandisi wa TARURA wilaya ya CHATO Edgarevarist Kidasi amesema mkandarasi atakayebainika kujenga barabara chini ya kiwango atawajibika kujenga upya kwa gharama zake na kuchukuliwa hatua huku wananchi wakieleza namna wanavyopata adha ya usafiri kutokana na ubovu wa barabara.

Chanzo: ITV
 
Safi kabisa tulilalamikia sana hii barabara tangu kipindi cha Mwendazake lakini hakuna hatua zilizochukuliwa na huyo mkandarasi inasemekana alikuwa na unasaba na mkulu wa Awamu ya 5( mzee wa Mi5 tena na kulazimishwa aongoze maisha yote), nitoe pongezi kwa serikali ya Awamu ya Sita chini ya AyaniLedi Samia kwa kuhakikisha maduhuli ya wananchi yanatumika vizuri na kuwabana makanjanja wote.
 
Hao Tarura si ndio walikuwa wasimamizi kisheria, sasa wala haihitaji maagizo toka Takukuru waagize tena, wakati contractually Ina maana either Tarura walishindwa kumsimamia Contractor kujenga barabara kwenye viwango na contract huwa inasema nini cha kufanya au kama barabara baadae imeharibika kutokana na 'calamities', 'conditions of contract' huwa inaelekeza nini cha kufanya.

Mambo ya sijui TAKUKURU mpaka kuingilia kwamba imetoa maagizo sie ingawa ni'laymen' kwenye sekta hiyo, tunafahamu kinachoelekea kilitokea na nini cha kufanywa kitaalamu, na sio hizo'Isidingo'za Mhandisi huyo wa Tarura.

Kazi iendelee.
 
Hakuna mkaguzi wa TARURA ili kujua ubora kabla hawajaidhinisha ianze kutumiwa? Hapo TARURA anatakiwa ilitakiwa m1 aondoke kwa uzembe huo
 
Taasisi ya Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Geita imemrejesha kujenga upya barabara ya Makurugusi kwenda Musasa wilayani Chato yenye urefu wa Kilometa moja na nusu kwa gharama zake baada ya mkandarasi huyo wa kampuni ya M/S Runazi General Supplies Company LTD kudaiwa kujenga barabara hiyo chini ya kiwango na kusababisha barabara hiyo kuharibika vibaya siku chache baada ya kukamilika.

Akizungumza mara baada ya kutembelea barabara hiyo kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Geita, Leonidas Felix anasema wamelazimika kumrudisha katika eneo la ujenzi ili aweze kujenga barabara hiyo upya kwa gharama zake kutokana na kujenga chini ya kiwango na kusababisha wananchi kulalamika kutokana na ubovu wa barabara hiyo.

ITV imezungumza na mkandarasi huyo Pancian Gasper akiwa katika ujenzi wa barabara hiyo nakusema barabara hiyo imeharibika mara baada ya kukamilika kutokana na kusombwa na mafuriko hivyo akalazimika kuijenga upya ili kutekeleza maagazo ya TAKUKURU.

Mhandisi wa TARURA wilaya ya CHATO Edgarevarist Kidasi amesema mkandarasi atakayebainika kujenga barabara chini ya kiwango atawajibika kujenga upya kwa gharama zake na kuchukuliwa hatua huku wananchi wakieleza namna wanavyopata adha ya usafiri kutokana na ubovu wa barabara.

Chanzo: ITV
No ujinga wa kiwango cha lami kwa TAKUKURU eti kutaka mkandarasi arudie kazi kwa viwango.
Hivyo viwango amevijulia wapi?
Na anavikaguaje?
Mhandisi mshauri na msimamizi wako wapi?

Hii ndio ujinga wa Awamu ya Tano tusiotaka kukusikia.
 
Ukweli ni hela ya kazi anayopewa mkandarasi
Kuna watu nao wanataka mgawo

Ova
 
Back
Top Bottom