Gazeti letu la Udaku JF..

Paw apiga marufuku matumizi ya vijineno vikolezeo kama lol, aisee, hakyanani, jf is never boring, wanchekesha, hunijui sikujui achana na mimi

asema adhabu ya matumizi hayo ni life ban
waleta mtambo wa kung'amua hata ukijiandikisha kwa ID nyingine unakula ban hadi kwenye nyumba yako unayoishi
 
lizzy na klorokwini waendelea na mipango ya 'party ya kusheherekea phd ya kloro'
ingawa imethibitika hiko chuo ndio kile cha mrema na mama rwakatare lol
 
The Finest apandishwa kizimbani kwa kosa la kujisaidia kwenye gari la manispaa, akijitetea mahakamani amesema hiyo ni aina mpya ya maandamano ambayo ameianzisha ili serikali iangalie upya suala la mgao wa umeme.
 
Mmmhh ukiwaendeza hawa jamaa humu hutalala baadae wajameni
 
Dah! atakua kakomesha wengi. Kwaza washawasha, figaniga, alafu Memo (Asee...Duh!) na wengine wengi...
 
Ndoa ya Mwanakijiji matatani, yasemekana kuwa na tabia ya kumchenga mkewe kuanzia mida ya jioni hadi asubuhi.

Ashangaa mkewe kupata ujauzito wa mapacha 3

ahaha kutafuta suluhu kwa babu DC
 
The Finest apandishwa kizimbani kwa kosa la kujisaidia kwenye gari la manispaa, akijitetea mahakamani amesema hiyo ni aina mpya ya maandamano ambayo ameianzisha ili serikali iangalie upya suala la mgao wa umeme.
Hii kali! yaani naona kabisa wanafunzi fulani wa chuo chetu those days wangeweza kujitetea hivo! hahahaha
 

Kisa cha Rev. Masanilo kutoonekana kwenye thread hii chafichuka!
  • Akutwa kajichimbia Guest house na mke wa mzee wa kanisa Chalinze :tongue:
  • Awashambulia waandishi wa Jf udaku na kuharibu camera zao
 
lizzy na klorokwini waendelea na mipango ya 'party ya kusheherekea phd ya kloro'
ingawa imethibitika hiko chuo ndio kile cha mrema na mama rwakatare lol

Hahahahahaha

Baada ya uchunguzi wa kutosha JF Udaku yagundua kwamba Boss sio bontauni. Mwenye akanusha madai na kudai japo alizaliwa Magadini bado nae ni mjanja maana alianza kuvaa boxa na singilendi miaka ya themanini.
 
" Waifu akiwa mbali basi hata makalio ya frozen chicken yananiturn on". Hivi ndivyo alivyonukuliwa The Boss akiliambia gazeti letu baada ya waifu wake kumtimua na gunia la mkaa.
 
Ashadii afichua siri. Aeleza JF udaku kwamba alifeli chekechea, "bila mzee wangu kunipa sukari nimpelekee mwalimu mkuu siku ya krisimasi nisingeingia darasa la kwanza. Huko nako kilichonifanikisha ni kuibia mtihani wa muandiko.Haki ya nani bila hivyo nisingekua naandika thread zilizonyooka" alinukuliwa akisema huku akionyesha namba za LIKE alizopokea.
 
Habari zilizotufikia punde zinavujisha na kuelezea kinaga ubaga kwamba afrodenzi amejifungua katoto sura mchina, miguu mwafrika. Akitafutwa na gazeti letu ili aelezee kadhia hii amejibu kwa mkato na kusema "Alelluyah"
 

Habari hizo zinaendelea kusema kwamba , hata alipokutana na Kaizer ilibidi wauze vitumbua na kumhonga msimamizi wa mtihani redio ya mbao isiozidi thamani ya elfu sita enzi za ninteen hakuna kondom ili Ashadii afanikiwe lengo lake hilo, mapenzi ya wawili hao yamebatizwa jina la "titanic wa kiborloni" ili kuenzi jitihada zao bila kujali uhalali wake.
 

Hahahahaha.

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba Klorokwini, yule lawyer maarufu wa JF amekamatwa kwa kosa la kuuza kesi za JF. MalariaSugu alikua tayari kukiri kwamba Klorokwini ndie haswa aliefanikisha ban lake la maisha kufutwa. Alipopatikana kwenye line alisema "hatujui, hatumjui hivyo tuachane nae."
 
Kamera zetu zimewanasa MJ1 na Mbu wakilishana karanga badili ya zabibu, Na wapendanao wawili hao walikuwa wepesi sana kuzielekeza shutuma zao kwa ugumu wa maisha uliosababishwa na serikali ya CCM ambao umewakosesha wao uwezo wa kumiliki hela ya kununua zabibu
 

lol............
 




I am Literally crying kwa FURAHA ya kicheko... Hakyanani vilee.... THANKS GUYS.... Dah! This thread imenipa furaha that will last for a Week if not a Mount!! Dah!!

Lizzy... Klorokwini dawa yenu yachemka.... lol
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…