Kwame Nkrumah
JF-Expert Member
- Dec 2, 2008
- 886
- 376
UONGOZI wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania(Tucta) umeamua kuingilia uhuru wa wafanyakazi kwa kupanga kuwashawishi kumchagua mtu unayemtaka awe Rais wa Tanzania.
Kaimu Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholaus Mgaya, jana alitangaza kwamba mwezi ujao, Kamati ya Utendaji ya Tucta, itakutana kujadili wafanyakazi wampe kura mgombea gani.
Mgaya alisema hayo alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Nne wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Utafiti, Sayansi, Teknolojia na Habari (Raawu) unaofanyika Dar es Salaam.
Sambamba na hayo pia Tucta ililalamikia kima cha chini cha mishahara ikisema nyongeza haijatosheleza na kupendekeza posho za wakurugenzi na viongozi wengine wa juu, ambazo ilisema ni asilimia 59 ya fedha yote ya mishahara nchini, ipunguzwe ili kujazia kwenye mishahara ya wafanyakazi.
Mgaya jana aliendelea kutumia propaganda potofu inayoenezwa na Chadema juu ya kauli ya Rais Jakaya Kikwete kwa wafanyakazi, inayodai kuwa alikataa kura za wafanyakazi 350,000.
Akizungumza na wafanyakazi katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam Mei mwaka huu, kuhusu madai ya nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma, Rais aliweka bayana kuwa uwezo wa Serikali kuongeza mshahara kwa kiwango wanachokitaka Tucta ni mdogo.
Hata hivyo, kutokana na shinikizo la wafanyakazi lililokuwa likijaribu kumtisha Rais kwamba atakutana nao kwenye uchaguzi, Rais pia aliweka wazi kuwa kama uchaguzi unatumiwa kama kigezo cha kuifanya Serikali ilipe mishahara ambayo haina uwezo nayo, bora azikose kura hizo.
Kwa hilo Rais angepongezwa kuwa ana ujasiri wa kuwa muwazi na kueleza hali halisi kuliko kupokea vitisho akatoa mambo ambayo hayana ukweli na kudanganya wananchi, lakini bahati mbaya hili linapotoshwa na hata kutengenezewa fulana, alisema mmoja wa wajumbe wa mkutano huo ambaye hakutaka kutajwa jina.
Lakini Mgaya katika kusisitiza hilo la kura alikaririwa akitoa mfano:
Mtu akikualika kwenye karamu halafu akakataa kula chakula utamlazimisha kula? Huwezi, hivyo na sisi tutamtafuta yule anayeweza kula tutampa kura zetu asiyetaka basi, kwani wahenga walisema ukisusa wenzio wala.
Alisema tayari wameanza maandalizi ya kikao hicho cha kamati ya utendaji ambacho ndicho kitakachotoa jibu la nani apigiwe kura na wafanyakazi wote nchini, ambapo pia shirikisho hilo limesema lina uwezo wa kumwita mgombea yeyote katika vikao vyao, aeleze namna atakavyoshughulikia maslahi ya wafanyakazi.
Akizungumzia madai ya wafanyakazi, alisema hadi sasa hayajatekelezwa kwa kuwa kiwango kilichoongezwa na Serikali ambacho ni Sh 125,000 ni cha chini na hakiendani na msimamo wao katika katika kikao cha majadiliano ambao walikubali kushusha kima cha chini mpaka Sh 160,000.
Alisema awali madai halisi ya Shirikisho hilo yalikuwa ni Sh 315,000 kwa mshahara wa kima cha chini lakini juzi Serikali ilitangaza kuongeza Sh 125,000 na kupunguza asilimia moja ya kodi ya mshahara (PAYE) tofauti na matakwa yao kuwa kodi hiyo ipunguzwe kwa asilimia 15.
Haya yote hayaridhishi wala hakuna kitu cha kujivunia, vita yetu iko palepale na katika kikao chetu pia tutajadili suala la mgomo, alisema Mgaya.
Alidai kuwa katika utafiti uliofanywa na Shirikisho hilo, walibaini kuwa fedha nyingi za mshahara zinaishia katika posho za wakurugenzi na viongozi wa juu ambapo Waziri akifungua mkutano analipwa Sh milioni 1.2, Naibu Waziri Sh 900,000 na Katibu Mkuu Sh 600,000 na hivyo kupendekeza posho hizo zipunguzwe kwa manufaa ya wafanyakazi.
Tunavyofahamu sisi asilimia 59 ya fedha za mishahara nchini ni posho na asilimia 41 ndio mishahara, ambayo kati yake takribani asilimia 30 inapotea, tunaomba fedha hizo za posho angalau Sh bilioni 55 ziongezwe kwenye mishahara
ili iboreshwe na si kungangania kuwa fedha hakuna, alisema.
Aidha, alisema kuhusu pensheni kwa wafanyakazi wastaafu, bado haijashughulikiwa na bado wastaafu wanalipwa pensheni ndogo inayoanzia Sh milioni mbili hadi nne, wakati amefanyakazi kwa zaidi ya miaka 30.
Hii si haki, mbunge anayekaa kwa miaka mitano bungeni analipwa Sh milioni 40 na zaidi, lakini mfanyakazi anayetumikia nchi kwa miaka 30 analipwa Sh milioni mbili, alihoji.
Alisema kutokana na masuala yote kutoshughulikiwa ipasavyo, bado shirikisho hilo halijakata tamaa hivyo katika kikao hicho pamoja na kutafakari mgombea wa kumpa kura, pia litajadili suala zima la mgomo ili wafanyakazi wapate haki yao.
Juhudi za kumpata Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya kuzungumzia suala hilo hazikuzaa matunda kutokana na simu yake kutopatikana.
MY TAKE: Kuna kamati ya Bunge ya Mashirika ya umma, ambayo kama sikosei inaongozwa na mbunge wa upinzani. Huu ni wakati muafaka wa kuonyesha demokrasia ya kweli kupitia kamati hiyo.
HabariLeo | Wafanyakazi kuchaguliwa mgombea urais