Gazeti la Nipashe limepotosha vikali

Ok .... kwani mizani za Tanroad zinapima uzito au ujazo? ....

enjoy your day
 
Ushaambiwa tani sasa unakuwa na akili kuwa TANI MOJA ya chuma ni nzito kuliko TANI MOJA ya manyoya.

Kumbe huko kwingine huwa unakisia tu
 
Kiswahili ni lugha pana na ngumu kuielewa.Mh.Raisi lugha aliyoitumia ya mafuso na landrover moja ni kutolea mfano kwa Wananchi waliyo wengi wapate kuelewa KINADHARIA ni nini haswa,Kwa mazoea tuliyozoea ya mtu wa Kawaida.Ndipo hapo ukiulizwa kilo moja ya pamba na jiwe ipi nzito,Kisha uje uangalie volume.Jaribuni kuwa waelewa
 
Nilimsikia Mh. Raisi lakini sikuelewa vizuri ana maanisha ujazo au ana maanisha tukitaka kuisafirisha mfano itabidi tuweke ktk magari yenye kuhimili vipimo vile vya uzito. Yaani tungeweka ktk gari mbili za tani 7 na mzigo mwigine tungeweka ktk pickup.
 
Nadhani 'kujaza lori' walimaanisha kufikia maximum capacity ya ubebeaji wa lori , na capacity ya ubebaji wa lori hupimwa kwa uzito (weight) sio ujazo (volume)
 
Lorry la tani saba litabebaje mzigo uliozidi tano 7 Huko si kutakuwa ni kufuata standard ulizowekewa? Kilicho ongelewa ni kwa kufuata viwango sio siasa au uswahili
 
Kizunguzungu mtindo mmoja.

Phd holder ndio alituambia hivyo!!!!

Halafu yeye anawashangaa wenzie eti ni maprofessor gani!!😀😀
Ninyi ni majinga flani hivi
 
Marandu, I am very conversent with units-- metric units. Naelewa what it relly means by density!.. cubic centimeter moja ya mercury ina uzito wa 13.5 grams!
Nakupata vizuri! being a chemist and physicist!
 
Nashukuru Marandu kwa maelezo yako ila tueleweshe kidogo weye mtaalam. Huo uzito huwa unapungua kutokana na density au? Nadhani mkuu alikuwa anamaanisha kuwa, ili kuibeba huyo dhahabu tani 15, ungelihitaji fuso 2 zigawiwe uzito wa tani 7 kila moja. hata kama ukubwa wa mzigo ni kama mikate 4 ya boflo na hiyo baki hata kama ni ndogo kama skonzi moja ndio ingesafirishwa na p/up. Kama sio hivyo, nielimishe mkuu wala usichoke
 
Yaani unachomaanisha hapa ni kwamba Fuso moja haiwezi kubeba kipande cha dhahabu chenye kipimo cha 1M x 1M x 1M? Kwa maana ya Fuso ya tani 7!?
 
Nadhani 'kujaza lori' walimaanisha kufikia maximum capacity ya ubebeaji wa lori , na capacity ya ubebaji wa lori hupimwa kwa uzito (weight) sio ujazo (volume)

Aliyesema haya sio picha aliyotaka Kuiweka akilini kwa Mwananchi mwananchi wa kawaida!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…