Gazeti la Mwananchi online lafungiwa miezi sita na kulipishwa faini milioni 5 kwa kupotosha

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania kuiptia Kamati ya Maudhui imesitisha leseni ya utoaji wa huduma za maudhui mtandaoni ya Mwananchi Newspaper kwa kipindi cha miezi sita, na kuwapiga faini ya Tshs milioni 5.

Adhabu hiyo imetolewa baada ya kubainika kuwa Aprili 13 kupitia mitandao ya kijamii Mwananchi Newspaper ilichapisha taarifa ya kupotosha kinyume cha Kanuni Na. 5(1)(a) na 12(l) za mawasiliano ya kieletroniki na posta, 2018

Mwananchi Newspaper waliitwa kujieleza kwanini wasifungiwe Aprili 15, na wakakiri kuwa kweli walikiuka kanuni hizo. Kwa kufuata sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Kifungu cha 28(1)(b) na (d) sura ya 172, ya mwaka 2017 wamepewa adhabu hizo

Iwapo Mwananchi Newspaper atashindwa kutekeleza adhabu hiyo TCRA itachukua hatua zaidi

====
Gazeti namba moja tanzania. Lenyekutupa habari za uhakika
 
Ila walijichanganya sana huwezi kupotosha taarifa ya mkuu wa nchi kwa kiwango kile. Sijui huwa hawahariri habari kabla ya kuposti.
 
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania kuiptia Kamati ya Maudhui imesitisha leseni ya utoaji wa huduma za maudhui mtandaoni ya Mwananchi Newspaper kwa kipindi cha miezi sita, na kuwapiga faini ya Tshs milioni 5.

Adhabu hiyo imetolewa baada ya kubainika kuwa Aprili 13 kupitia mitandao ya kijamii Mwananchi Newspaper ilichapisha taarifa ya kupotosha kinyume cha Kanuni Na. 5(1)(a) na 12(l) za mawasiliano ya kieletroniki na posta, 2018

Mwananchi Newspaper waliitwa kujieleza kwanini wasifungiwe Aprili 15, na wakakiri kuwa kweli walikiuka kanuni hizo. Kwa kufuata sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Kifungu cha 28(1)(b) na (d) sura ya 172, ya mwaka 2017 wamepewa adhabu hizo

Iwapo Mwananchi Newspaper atashindwa kutekeleza adhabu hiyo TCRA itachukua hatua zaidi

====
unajuwa bado nipo kwenye maamuzi ya serikali kulifungia gazeti la mwananchi.u najuwa naamin kabisa kuwa kuna kinachoendelea nyuma ya pazia tusissma tu kuwa gazeti lina ukosoa uwongozi wa awamu ya 5 sio kweli,gazeti ni chombo cha wazi,kila mtu anasoma,sitaki kuamin kama amekaa mtu mmoja na akawa na chuki zake na kuamua kuandika habari za upotoshaji kama inavyo daiwa.
kuna gazeti la TANZANITE la mwenye miliki ni cprian musiba,lakin nani asiojuwa shombo za mtu huyo?nani asiojuwa maneno machafu ya mtu huyo lakin ni lini mtu huyo amechukuliwa hatua na serikali?kama wataka uhuru huo wayaache magazeti yaandike kinacho onekana.
 
Hawa mwananchi waliweka video Twitter Rais akinunua samaki magengeni watu wamejaa wakati huu wa corona,baadaye serikali ikakanusha kwa siyo video ya mda huo ni ya siku nyingi mno.Ndo zogo ilipoanzia ,pia the citizen tv walisema JPM ni mkaidi akawapiga biti .
natamani sana kuijuwa hiyo habari ambayo iliandikwa.manake siku hizi ukiandika ukweli,basi wewe upo kwenye hatari,ukisema ukweli upo kwenye hatali,unajuwa tunanyimwa sana uhuru wa kuongea na uhuru wa vyombo vya habari.

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
 
Tovuti ya mwananchi haiko hewani kwa muda sasa mwenye kujua atujuze
 
Attachments

  • mwananchi.PNG
    mwananchi.PNG
    9 KB · Views: 1
Back
Top Bottom