Gazeti la Jamhuri: Nyani walewale msitu tofauti

Kiranja

JF-Expert Member
May 19, 2007
751
336
Balile, Manyerere waacha New Habari kuanzisha linaitwa Jamhuri, kwa lengo la kukamilisha mkakati wa Lowassa kuingia Ikulu 2015, akiwa na malengo maalumu kutoka Ubunge Monduli na kuingia Ikulu ya Magogoni.

---------------
October 10, 2011
Wapendwa wanachama wa Jamii Forum salaam.

Kwanza naomba kutangaza kwa mara ya kwanza kuwa leo hii nimejiunga katika mtamdao huu. Miaka yote nimekuwa nikisoma postings kama wasomaji wengine napenda kuwapongeza waanzilishi wa mtandao huu wenye nafasi ya pekee katika jamii tunayoishi.

Kubwa lililonifanya nijiunge leo ni taarifa inayoendelea kujadiliwa humu ndani juu ya uanzishwaji wa gazeti la Jamhuri. Kwa kuwa siku zote mimi ni muwazi, nimeona ni vyema kwanza nisiingie humu kwa majina bandia, bali nitumie jina langu halisi. Pili, napenda kuwafahamisha wanajamii kuwa ni kweli tumeanzisha gazeti la Jamhuri. Ni kweli pia wakurugenzi wa kampuni iliyoanzisha gazeti hili; Jamhuri Media Limited ni Deodatus Balile, Manyerere Jackton, Absalom Kibanda na Mhariri mwingine ambaye jina lake nitalitaja siku za usoni.

Gazeti hili tunalimiliki sisi waandishi wanne asilimia 100. Nawahakikishia hakuna mkono wa mwanasiasa yoyote. Hawa wanaomtaja Edward Lowassa kuwa ndiye mmiliki, napenda kuwahakikishia kuwa wamekosea. Tunao uzoefu wa kutosha katika kuanzisha magazeti. Nimeshiriki kuanzisha gazeti la Mwananchi na Mwanaspoti mwaka 2000, nikashiriki kuanzisha gazeti la Tanzania Daima na Sayari, mwaka 2004. Hakika nilipata uzoefu wa kutosha katika taaluma hii.

Yapo mambo si msingi wa mada hii leo, kwamba kwa nini nilitoka Free Media Ltd, hapa sitayajadili lakini niliokwishazungumza nao kwa njia ya simu, hakika walinihurumia na kunipongeza kwa uamuzi niliouchukua. Kosa nililofanya mwaka 2004 la kuanzisha taasisi ya kitaaluma bila kuwa na maandishi ya kimkataba, lilikuwa fundisho kubwa na hili nimelizingatia katika kuanzisha Jamhuri Media Limited, kuwa si vyema katika biashara ya habari kama kweli una nia ya kuitumikia jamii, kushirikisha wanasiasa.

Wanasiasa kama raia wema, ni sehemu ya jamii hii. Sisi kama sisi hatuna mtaji. Wakati tunajiandaa kuanzisha na hatimaye kukopa benki, tumepata wasamaria ambao hawana masilahi ya kisiasa. Hatuko tayari kufanya kazi kwa mashinikizo ya kisiasa. Tutaitumikia jamii, kwa uadilifu mkubwa, ubunifu na kuweka mbele utaifa (kutetea rasilimali za nchi). Karibuni mtuunge mkono hata kwa kutuchangia sehemu ya mtaji (kifedha na hata kwa ushauri).

Ndugu zangu Watanzania, sisi tumefika mahala tumethubutu. Hakuna aliyezaliwa kuwa mmiliki wa vyombo vya habari, na wengine kuwa watumishi wake. Ikiwa kuna yeyote anatutilia shaka, kwa sasa tunaomba atupe nafasi. Kadri tutakavyochapisha nakala zetu, atatujuvya iwapo tupo kuchumia matumbo kama wanavyosema au la. Nawahakikishia mimi si mmoja wa wachumia tumbo.

Tuungeni mkono, tuliendeleze taifa letu kwa kukupeni habari sahihi bila mikingamo. Sisi kauli mbiu yetu ni kuwa TUNAANZIA WENGINE WANAPOISHIA.

Asanteni
October 31, 2011
Taarifa ni kuwa Lowasa katika mkakati wa urais wa 2015 anaanzisha magazeti 5 kwa mpigo ili kufanya kampeini kuanzia sasa.

Gazeti la kwanza litaanza kuchapishwa wiki ijayo Linaitwa
Jamhuri litakuwa chini ya Deodatus Balile na waandishi wengine akiwemo Manyerere nk.Litaaanza likiwa linatoka kila wiki.

Chanzo ni mimi mwenyewe, niko jikoni.

December 05, 2011
Habari nilizozipata usiku huu ni kwamba gazeti mnalolisubiri kwa shauku kubwa liitwalo JAMHURI linalomilikiwa na EL nitaingia mtaani Jumanne hii.

Anzeni kupata toleo la kwanza hadi mfikie hatua ya ku-judge kama linampigia debe kweli EL kwa 2015, linampigia debe kwa 2012 CCM chaimanship au kuna jingine nyuma ya pazia.

Tahadhari: USINIULIZE SOURCE PLZ

December 06, 2011
Nilikuwa nalipitia Gazeti jipya la kila wiki la JAMHURI ambalo nakala yake ya kwanza imetoka leo. Gazeti hili linalodaiwa kumilikiwa na waandishi nguli Deodatus Balile na Manyerere Jackton limekuwa likipigiwa upatu kwa muda mrefu kwamba litakuwa bora na hata kauli mbiu yao ni kwamba "Tunaanzia wanapoishia wengine" inaashiria hilo.

Kilichojitokeza katika pitia yangu ni kwamba gazeti hili halijaja na kitu kipya au chochote kinachoakisi weledi wa uandishi na ubobevu wa wamiliki wake. Habari zimeendelea kuwa ni nyepesi, na character assassination ya wale wanaochukuliwa kwamba ni maadui wa wenye magamba imeendelezwa. Kwa ujumla "layout" ya gazeti hili na hata maudhui yake yanafanana sana na gazeti la Mtanzania na pengine ni sahihi kwamba wao wameanzia pale yanapoishia magazeti dada ya gazeti hili, nikimaanisha Mtanzania na Rai.

Kwa haya niliyoyaona humu, ni dhahiri kwamba kumbe misitu tu ndiyo imebadilika lakini nyani ni wale wale.
 
Ni kweli, wawili hao wameandika barua za kuacha kazi New habari. Nasikavyo katika mradi huo yumo pia na Kibanda wa Tanzania Daima.
 
Ok!. Lakini aking'ang'ania hatafika mbali. Uwaziri mkuu alipewa kwenye sahani akakimbilia shimoni. Uraisi nasikia anautafuta Nigeria na huo huwa haudumu
 
Lowasa jamani anajisumbua. Uwaziri mkuu ulimshinda atawezaje uprezidaa. Anajisumbua. Hakuna wa kumchagua. Asidhani waTZ ni wajinga kiasi hicho. Aachane na kigazeti hicho. Rais wa 2015 anajulikana naye ni Dr.S......LA.
 
Balile, Manyerere waacha New Habari kuanzisha linaitwa Jamhuri, kwa lengo la kukamilisha mkakati wa Lowassa kuingia Ikulu 2015, akiwa na malengo maalumu kutoka Ubunge Monduli na kuingia Ikulu ya Magogoni. Mwenye taarifa kamili atujuze
Sasa hii ni tetesi au nini? Inaonekana kama unafahamu halafu mwenye uhakika atujuze zaidi, hili ni pungufu la watoa thread wengi humu jamvini. Kama kitu hujui basi leta ili wanaofahamu zaidi wadadavue. Back to the topic, sifahamu chochote ndiyo kwanza umenizindua juu ya hilo lkaini ukweli Lowasa kuwa rais 2015 ni ndoto.
 
wacha waende wanapotaka... ndio uhuru wenyewe wa habari... unahusisha pia wanahabari kwenda wanapotaka
 
Balile, Manyerere waacha New Habari kuanzisha linaitwa Jamhuri, kwa lengo la kukamilisha mkakati wa Lowassa kuingia Ikulu 2015, akiwa na malengo maalumu kutoka Ubunge Monduli na kuingia Ikulu ya Magogoni. Mwenye taarifa kamili atujuze

Hawa wamesha fail tangu mwanzo jamhuri maana yake nini? Halafu, kama nikweli, hawa watu wataendelea kutunika mpaka lini, kwa nini wasiache kazi na kwenda kujiajiri, kama wana elimu.. Mbona imewafanya watumwa? Kibanda ana gazeti lake la Umoja (kama ni lake) juzi nimeingia super market Tegata nikaliona kwenye shelf, nilipolichukua nikagundua ilikuwa ni issue ya February, hivi kuna mmoja wenu angependa kusoma habari za February leo???. Balile atakuwa dissapointed kwa sababu alityamani sana kuwa ceo wa habari corp. Anyway waanzishe tu hilo gazeti lao, lakini wajue tu kwamba watz kwa sasa hawadanganyiki.
 
Balile, Manyerere waacha New Habari kuanzisha linaitwa Jamhuri, kwa lengo la kukamilisha mkakati wa Lowassa kuingia Ikulu 2015, akiwa na malengo maalumu kutoka Ubunge Monduli na kuingia Ikulu ya Magogoni. Mwenye taarifa kamili atujuze

bora raisi awe mrema kuliko mamvi
 
Jamani kwa taarifa za uhakika za jana jioni hizi habari ni sahihi, infact huu mpango wa kuanzisha hilo gazeti ulianza miezi mingi kidogo iliyopita ila ukapoa kidogo lakini sasa nadhani "mtaalam" keshapima upepo na ameona muda ni muafaka. Kibanda naye yumo.
 
Hata kama ni kweli kwamba Lowasa hakuhusika ktk richmond, faili lake lilishachafuka kulisafisha ni kazi ngumu mno!
 
Lowasa jamani anajisumbua. Uwaziri mkuu ulimshinda atawezaje uprezidaa. Anajisumbua. Hakuna wa kumchagua. Asidhani waTZ ni wajinga kiasi hicho. Aachane na kigazeti hicho. Rais wa 2015 anajulikana naye ni Dr.S......LA.

kinachonishangaza ni jinsi anavyotegemea mnigeria joshua kumwingiza ikulu
joshua got nothing to do in this land,nenda akakufanye uwe rais wa nijeria
tamaa mbele mauti nyuma
 
Back
Top Bottom