Muhingo Rweyemaumu yeye anasemaje?
Nasikia Manji kamumwaga licha ya kujipendekeza.
Muhingo Rweyemaumu yeye anasemaje?
Kamura nakuunga mkono asilimia 100% kuwa hawa jamaa are old enough to stand on their own feet.Hivi Balile, Manyerere na Kibanda hawawezi kuanzisha gazeti lao mpaka wafadhiliwe na Lowassa? Mbona ni Wahaririri wa siku nyingi na Waanzilishi wa Tanzania Daima?
kama manyerere naye ameingia kuupepea ufisadi wa EL basi nguvu ya pesa ni zaidi ya tsunami. huyu kijana alikuwa mzalendo safi, BASI TENA...echaro chafwaa!!!!Tusubiri tu tutasikia mengi mwaka huu, loh!
Kibanda is very smart kuungana na mchumia Tumbo Balile .Yaani Balile hana tofauti na Nape na FF haoa jamvini.Kibanda siamini kwamba naye anachumia tumbo .
kama manyerere naye ameingia kuupepea ufisadi wa EL basi nguvu ya pesa ni zaidi ya tsunami. huyu kijana alikuwa mzalendo safi, BASI TENA...echaro chafwaa!!!!
Muhingo Rweyemaumu yeye anasemaje?
Karibu sana Balile,Ni kweli hilo gazeti la Jamhuri lipo
Wapendwa wanachama wa Jamii Forum salaam.
Kwanza naomba kutangaza kwa mara ya kwanza kuwa leo hii nimejiunga katika mtamdao huu. Miaka yote nimekuwa nikisoma postings kama wasomaji wengine napenda kuwapongeza waanzilishi wa mtandao huu wenye nafasi ya pekee katika jamii tunayoishi.
Kubwa lililonifanya nijiunge leo ni taarifa inayoendelea kujadiliwa humu ndani juu ya uanzishwaji wa gazeti la Jamhuri. Kwa kuwa siku zote mimi ni muwazi, nimeona ni vyema kwanza nisiingie humu kwa majina bandia, bali nitumie jina langu halisi. Pili, napenda kuwafahamisha wanajamii kuwa ni kweli tumeanzisha gazeti la Jamhuri. Ni kweli pia wakurugenzi wa kampuni iliyoanzisha gazeti hili; Jamhuri Media Limited ni Deodatus Balile, Manyerere Jackton, Absalom Kibanda na Mhariri mwingine ambaye jina lake nitalitaja siku za usoni.
Gazeti hili tunalimiliki sisi waandishi wanne asilimia 100. Nawahakikishia hakuna mkono wa mwanasiasa yoyote. Hawa wanaomtaja Edward Lowassa kuwa ndiye mmiliki, napenda kuwahakikishia kuwa wamekosea. Tunao uzoefu wa kutosha katika kuanzisha magazeti. Nimeshiriki kuanzisha gazeti la Mwananchi na Mwanaspoti mwaka 2000, nikashiriki kuanzisha gazeti la Tanzania Daima na Sayari, mwaka 2004. Hakika nilipata uzoefu wa kutosha katika taaluma hii.
Yapo mambo si msingi wa mada hii leo, kwamba kwa nini nilitoka Free Media Ltd, hapa sitayajadili lakini niliokwishazungumza nao kwa njia ya simu, hakika walinihurumia na kunipongeza kwa uamuzi niliouchukua. Kosa nililofanya mwaka 2004 la kuanzisha taasisi ya kitaaluma bila kuwa na maandishi ya kimkataba, lilikuwa fundisho kubwa na hili nimelizingatia katika kuanzisha Jamhuri Media Limited, kuwa si vyema katika biashara ya habari kama kweli una nia ya kuitumikia jamii, kushirikisha wanasiasa.
Wanasiasa kama raia wema, ni sehemu ya jamii hii. Sisi kama sisi hatuna mtaji. Wakati tunajiandaa kuanzisha na hatimaye kukopa benki, tumepata wasamaria ambao hawana masilahi ya kisiasa. Hatuko tayari kufanya kazi kwa mashinikizo ya kisiasa. Tutaitumikia jamii, kwa uadilifu mkubwa, ubunifu na kuweka mbele utaifa (kutetea rasilimali za nchi). Karibuni mtuunge mkono hata kwa kutuchangia sehemu ya mtaji (kifedha na hata kwa ushauri).
Ndugu zangu Watanzania, sisi tumefika mahala tumethubutu. Hakuna aliyezaliwa kuwa mmiliki wa vyombo vya habari, na wengine kuwa watumishi wake. Ikiwa kuna yeyote anatutilia shaka, kwa sasa tunaomba atupe nafasi. Kadri tutakavyochapisha nakala zetu, atatujuvya iwapo tupo kuchumia matumbo kama wanavyosema au la. Nawahakikishia mimi si mmoja wa wachumia tumbo.
Tuungeni mkono, tuliendeleze taifa letu kwa kukupeni habari sahihi bila mikingamo. Sisi kauli mbiu yetu ni kuwa TUNAANZIA WENGINE WANAPOISHIA.
Asanteni
Lowasa jamani anajisumbua. Uwaziri mkuu ulimshinda atawezaje uprezidaa. Anajisumbua. Hakuna wa kumchagua. Asidhani waTZ ni wajinga kiasi hicho. Aachane na kigazeti hicho. Rais wa 2015 anajulikana naye ni Dr.S......LA.
Kubwa lililonifanya nijiunge leo ni taarifa inayoendelea kujadiliwa humu ndani juu ya uanzishwaji wa gazeti la Jamhuri. Kwa kuwa siku zote mimi ni muwazi, nimeona ni vyema kwanza nisiingie humu kwa majina bandia, bali nitumie jina langu halisi. Pili, napenda kuwafahamisha wanajamii kuwa ni kweli tumeanzisha gazeti la Jamhuri. Ni kweli pia wakurugenzi wa kampuni iliyoanzisha gazeti hili; Jamhuri Media Limited ni Deodatus Balile, Manyerere Jackton, Absalom Kibanda na Mhariri mwingine ambaye jina lake nitalitaja siku za usoni.