hivi jamani ninyi mnaohangaika na hawa waislam uchwara, wa hako kagazeti, kuwafafanulia maana halisi ya kauli ya Msigwa, hivi kweli mnafikiri wao hawaielewi hiyo kauli??!! Hawa waislam uchwara wanaielewa vizuri sana kauli ya Msigwa lakini kinachofanyika hapo ni uzandiki wa kutumia hii midini ya kikoloni kuchonganisha waafrika. Kwa Mwislam kutoa tafsiri ya jinsi hii kwa waislam wenzake ni muendelezo ule ule wa kudharauliana kati ya waislam wenyewe, mintarafu maneno ya mwalimu Nyerere kuwa "Mtu akikudanganya, na yeye anajua kuwa unatambua kuwa anakudanganya, na wewe ukamkubalia, Anakudharau". Hapa hamna cha sana zaidi tu ya waislam wa hako kagazeti kuwadharau waislam wenzao. Badala ya kuwahimiza waislam wenzao wakazanie ilmu dunia kwa kwenda shule wao wanacapitalize kwenye ujinga wa waislam walio wengi kwa faida ya ccm iliyowadidimiza waislam hao kwa miaka nenda miaka rudi. Ni ujinga ulioje huu??!! Nakumbuka Nyerere alitumia maneno ambayo, baadaye, hawa wasomi uchwara, na wapumbavu, wakataka kuyapa hayo maneno mujarab ya Nyerere tafsir hizi hizi za kishenzi; mwalimu alitumia maneno kwamba "I cant let my country go to the dogs": tafsri ya moja kwa moja hapo (direct translation kama inayofanywa na haka kagazeti uchwara) itakuwa mwalimu alimaanisha "siwezi kukaa kimya niache nchi yangu itawaliwe na ma mbwa". Basi wasomi uchwara, na bila shaka walikuwepo hawa wa haka kagazeti, wakashadidia eti Nyerere kawatukana watanzania wasio wanaccm kuwa ni ma mbwa!!!!!
Ndiyo maana mimi huamini kuwa ni kweli kabisa watu wanaposema kuwa ccm imedumaza kabisa elimu ya nchi hii, kwa walio wengi, ili idumishe ujinga wa walio wengi kwa minajili ya kuiwezesha kuwapumbaza na hatimaye kutawala milele isivyo halali. Watanzania wengi, hasa waislam, wanaangamia si kwa kupenda bali kwa kukosa maarifa walionyimwa, na wanayoendelea kunyimwa, kwa miaka mingi, na serikal ya ccm. Ubaya zaidi ni pale waislam wenzao walioona mwanga kidogo wa ilmu, badala ya kuwatoa wenzao kwenye hayo maangamizi ya ccm, kwa kuwapa ilmu na kuwakazania waende shule, wao ndo kwaaaaaaaanza wanawasokomezea kabisa wenzao kwenye shimo la umauti wa ccm.
Na hili si jambo la kushangaza wala la bahkati mbaya. Dini hizi za kuja(dini za kikoloni) zimetumika sana kuchochea chuki, mapigano, vita na dhulma dhidi ya jamii mbalimbali duniani. Maisha mengi sana yameangamizwa kwa kuchochewa na dini hizi ambazo zilianzishwa huko mashariki ya kati na kuenezwa maeneo mengine duniani. wachochezi wa dini hizi za kuja, huku wakijifanya waaumini wa Mungu, wanajificha nyuma ya dini hizi wakijifanya kuubiri wema wa Mungu huku nia yao hasa ni kuubiri uzandiki, fitna na chuki wakiwa na kiu ya kuona mifarakano na kuchinjana kati ya ndugu na ndugu. Huwa napata shida sana napomuona mswahili wa kinyerezi anajinasibu sana na mwarabu, kajitwika vilemba na kanzu, kifimbo mkononi na kijastibikozi chake basi anajiona eti yeye naye ni mwaaaaaaarabu kweli kweli na anafikia hata hatua ya kuwadharau waafrika wenzie, ambao kihakika kabisa ni damu yake ya karibu kuliko hao waarabu. Ni ajabu kuwa Waafrika wanapendana zaidi kwa kujiita ndugu katika imani (za kuja/kuletewa) kuliko wanavopendana kwa kujiita ndugu wa/katika damu!!!!
Dini inapofikia kiwango cha kutumika kueneza ubaya na uovu kwa kiwango hiki, tena uovu dhidi ya ndugu wa damu moja, basi dini hiyo inapoteza kabisa u maana wake na inabakia kuwa ushenzi tu sawa na uchawi na ushirikina.
Ni wajibu wa waislam wanaoijua vizuri dini yao kukataa dini yao kugeuzwa ushenzi kama wafanyavyo waandishi kama hawa wa gazeti hili la Al-Huda. Ni wajbu wa waislam waliobahatika kupata ilmu dunia kuhangaika kuona kuwa, jamii yao ya kiislam, ambao wengi wao hawajabahatika kupata ilmu kama wao, nayo inapata ilmu kwa kuweka miundombinu na kuwahimiza waislam kuitafuta ilmu. Mtume (saw) amesema itafuteni elimu ijapokua iko ktk miji ya china, kwani kutafuta ilimu ni wajibu wa kila islamu (Ibnu Abdul-Bar). Mtume (saw) akaongeza sadaka iliyo bora ni islamu kujifunza ilimu, kisha akamfunza mwenzie......sasa cha ajabu hawa kina ritz, aL-hUDA, faiza foxy na wenzao wengine wa kaliba yao, badala ya kuwafunza waislam wenzao ilmu wao wanawajaza ujinga na upumbavu mtupu, nia ikiwa ni kuisaidia ccm iendelee kuwatawala, kuwanyonya na kuwakandamiza waislam, na jamii nyingine za watanzania, daima.
Mwalimu alionya - Nanukuu;
Wale wenye bahati ya kupata elimu, wanao wajibu wa kulipa jasho ambalo wengine wamejitolea. Ni sawa na mtu aliyepewa chakula chote katika kijiji chenye njaa, ili apate nguvu za kwenda kuhemea katika sehemu zilizo mbali. Mtu huyu akipokea chakula hicho na halafu asiwaletee ndugu zake, basi yeye ni msaliti
.
Hapa, Mwalimu alikuwa akiwakumbusha vijana wasomi, tena wa dini zote wakiwemo waislam, wanaopata elimu kwa jasho la Watanzania kutumia elimu yao kwa maendeleo ya wananchi badala ya maendeleo binafsi, au kwa manufaa ya kikundi (chao) cha kitabaka nchini. Kufanya hivyo ni usaliti kwa umma. Waandishi uchwara wa kagazeti ka Al Huda wanausaliti na kuudhalilisha umma wa Kiislam, wanawadhihaki na kuwang'ong'a kuwa hawana ilmu kwa kuwapa tafsir za kidhalilishaji, kijinga na kipumbavu kesha wanakaa pembeni wakiwacheka kwa jino pembe, wakiwaangalia waislam wenzao wakivurugana kwenye tope la ujinga, huku wenzao wasio waislamu, na ni wakristo to be precise, wakichanja mbuga kujiwekea miundo mbinu ya ilmu kila kona, kukwea vidato na vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi. Matokeo ya muda mrefu ya haya ni waislam kuzidi kuachwa nyuma kielimu na kimaendeleo na mwishoni kuishia malalamishi yasiyoisha
Waislam wema kote nchini tunawakumbusha tena na tena, na ni kwa nia njema tu na kama hutaki unaacha....shtukeni sasa dhidi ya huu upumbavu mnaojazwa, Vuteni shuka sasa kabla hakujacha kabisa, la msivute shuka milele.