Gazeti la Al-Huda lafanya uchochezi

Gazeti la Al-Huda lafanya uchochezi

Status
Not open for further replies.
Uelewa mdogo wa mwandishi juu ya matumizi ya 'analogy', 'metaphor', na 'simile' AKA figurative speech; na si ajabu hili kutokea kwenye gazeti hilo.

Wewe ndio uelewewa wako ni mdogo, mwandishi anajuwa anachokifanya na ana uelewa mkubwa tu.

Hizi dini mbili zilipaswa kupigwa marufuku miaka mingi huko nyuma, maana kuna taasisi ndani ya dini hizi kama dunia ikiwa na amani na wao watakufa njaa.

Inahitaji akili nyingi kunielewa hapa, kuna vigroup vya wakristo na waislamu vinaendesha maisha yao kwa kutumiwa pesa na wazungu na waarabu, hivi vigroup vinaishi kwa kutengeneza taarifa kwamba kila upande unaonewa na ndio maaana kuna wakati nawadharau sana wazungu huwa hata sijui malengo yao ni nini maana kama ni huruma waje watembee mikoani huko wakauone umaskini wapeleke pesa huko direct.
 
Hilo gazeti niliposoma heading tu, nikatambua ni la kidini na linabeba misimamo ya kuwagawa Watanzania kidini, kama sivyo lingeenda hatua moja mbele kumuuliza Msigwa, ana maana gani au alimaanisha nini, na kwa nini anafananisha Chadema na Kanisa.

Vv

Haina haja ya kumuuliza Msingwa anamaanisha nini (alikuwa anaongea Kiswahili sio Kichina). Ya nini kumuuliza tena? Yeye kisha sema Chadema ni kama kanisa tena kwa lugha fasaha kabisa ya Kiswahili.
 
Tatizo la watu kukariri maana ya neno Wokovu kwamba linatumiwa na wakristo mtu anapoamua kuachana na maisha yasiyo mjua Mungu.Unapokuwa ktk hali ya hatari halafu ukapata msaada wa kuepuka na kuweza kutoka ktk hali hiyo tunaita UMEOKOKA kifo au hatari .So Chadema ndicho chama pekee cha kututoa watanzania ktk hatari ya ufisadi,umaskini, nk ambayo tumefungiwa ndani na ccm
 
Gazeti limeripoti kama alivyosema Mchungaji wa Chadema Msigwa.

Kasema kweli Chadema ni kama Kanisa.

Sasa hapo unalishambulia gazeti kwa kosa gani, wewe umejuaje kama Mchungaji Msigwa alikuwa hana maana hiyo.

Nakumbuka huyu mchungaji alisimama ndani ya bunge na kuhoji kwanini mwezi wa ramadhan zanzibar migahawa inafungwa ... mchana
 
Magazeti mengi tu yameandika hii habari.

Chadema ni kanisa la wokovuAkizungumzia taarifa hizo, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa alikifananisha chama hicho na kanisa ambalo kwa kawaida halikatai mtu, bali linawapokea wenye dhambi na kuwaongoza kufanya toba.“Chadema ni kama kanisa, hakataliwi mtu, tunahubiri habari njema ya wokovu, ukija hapa unatubu unaendelea kufanya kazi,” alisema.

Mwananchi.
 
Chadema Ni kanisa kweli. Au we hutaki?

Kama kanisa maana yake kazi inayofanya niyakupambana kuwaokoa watanzania kutoka kwenye maisha magumu yaliyosababishwa na mafisadi na kuwapa Raha,Umoja na Uhuru kamili.Ukijua kweli inakuweka huru
 
Msigwa ametumia figure of Speech aina ya simile. Hivi ni vitu vya kawaida kabisa katika mazungumzo yetu ya kila siku. Vinatusaidia kutoa picha ya kile tunachomaanisha ili kieleweke kwa urahisi zaidi. Ni kama unaposema, "Mtu huyu ana kichwa kigumu kama jiwe" hapa humaanishi kuwa kichwa cha mtu huyo ni jiwe bali ni jinsi gani mtu huyo alivyo mgumu kuelewa.

Hata vivyo kwa mtu mwenye ufahamu mfinyu kama huyu mwandishi, vitu kama hivi havieleweki. Ninashangaa hata waliompa cheti cha uandishi wa habari walimpa kwa vigezo vipi. Mtu kama huyu ni wa kumpuuza tu.
 
Magazeti mengi tu yameandika hii habari.

Chadema ni kanisa la wokovuAkizungumzia taarifa hizo, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa alikifananisha chama hicho na kanisa ambalo kwa kawaida halikatai mtu, bali linawapokea wenye dhambi na kuwaongoza kufanya toba.“Chadema ni kama kanisa, hakataliwi mtu, tunahubiri habari njema ya wokovu, ukija hapa unatubu unaendelea kufanya kazi,” alisema.

Mwananchi.

Ritz maana ya hayo uliyonukuu ni kwamba wale walioko ccm wakihama na kuwa wanachama wa chadema wanakuwa wanachama wapya na wanaachana na maisha Yale ya uccm
 
Tatizo la watu kukariri maana ya neno Wokovu kwamba linatumiwa na wakristo mtu anapoamua kuachana na maisha yasiyo mjua Mungu.Unapokuwa ktk hali ya hatari halafu ukapata msaada wa kuepuka na kuweza kutoka ktk hali hiyo tunaita UMEOKOKA kifo au hatari .So Chadema ndicho chama pekee cha kututoa watanzania ktk hatari ya ufisadi,umaskini, nk ambayo tumefungiwa ndani na ccm

Mkuu wanaelewa ila wanajifanya hamnazo kwa sababu ya mahaba!
 
Muulize ilo swali Mchungaji wenu Msigwa siyo mimi.

Nimekupa maana yake kanisa ni sehemu ya kuwapokea watu wanaoacha matendo machafu au ushirika na mambo ya aibu
 
Wewe ndio mchochez,kwani ulijuaje kama Msigwa hakukusudia unacho kikataa wewe? Al huda "wame quote" direct kutoka kwa source,je wewe hio hoja yko kuwa Msigwa hajakusudia "uchochez" ume qoute kwa nani? Msigwa amekanusha kauli yake au wewe ndo msemaji wake? Hio falsafa kwanini aitumie ya "symbol" ya kanisa?wakat tayar kuna vugu vugu la udini na mivutano ya kidin isio kwisha?Tena tuhuma nyengine zinaelekezwa hko hko chadema?Kwani Msigwa hakuona falsafa nyengine ya kusema?Mfano,kwanini msigwa asiseme "Chadema ni kama maji ya kunywa,kila mtu atayahitaji" n.k,Falsafa ya udini haikubaliki hata kama yeye ni mchungaji?Msigwa ndio mchochozi pamoja na wewe.Al huda ni wasafi,wao wamefanya direct quote from the source.

Njia ni moja,mafikio tofauti.

Wewe ndo umepotea kabisa na pengine wewe ni miongoni mwa waandishi wa gazeti hili!!

Unauliza amejuaje kama Msigwa alimaanisha hicho alichokisema mleta mada!?

Wewe hujui kusoma au kusikia na kisha ukapata mantiki (logic) ya kilichosemwa au kilichosikika?

Kama wana natatizo ya tafsiri ya mantiki kama uliyonayo wewe, hata km wangemsikia kasema "CHADEMA ni kama maji....,...................." wasingeelewa na wangekuja na tafsiri potofu tu ili mradi tu nia na lengo lao ovu litimie!!

Kubali tu ndugu yangu, gazeti hili limechemka na kujishushia hadhi na nadhani wana malengo ovu/baya nyuma yake especially kwa Msigwa mwenyewe na chama chake!

Hakuna namna nyingine unavyoweza kusema dhidi ya hili gazeti zaidi ya alichokiona mleta mada, and I agree with him/her!
 
Wewe ndo umepotea kabisa na pengine wewe ni miongoni mwa waandishi wa gazeti hili!!

Unauliza amejuaje kama Msigwa alimaanisha hicho alichokusema mleta mada!?

Wewe hujui kusoma au kusikia na kisha ukapata mantiki (logic) ya kilichosemwa au kilichosikika?

Kubali tu ndugu yangu, gazeti hili limechemka na kujishushia hadhi na nadhani wana malengo ovu/baya nyuma yake especially kwa Msigwa mwenyewe na chama chake!

Hakuna namna nyingine unavyoweza kusema dhidi ya hili gazeti zaidi ya alichokiona mleta mada, and I agree with him/her!
Magazeti zaidi ya kumi yameandika hii habari au nikuwekee?
 
Gazeti la Mwananchi, Nipashe, Tanzania Daima yote yameandika hii habari yeye kalichagua Al-Huda tu.

Hawa jamaa wana chuki sana na Waislam

Kwahiyo unataka kuniambia ndani ya CUF hakuna wakristo!? Kwahiyo UKAWA imekuwa ni ya wakristo kwasababu ya Chadema!? Shame on you!
 
mbona mnataka kumsemea msigwa?

Mwenyewe kasha sema chadema ni kanisa, wanahubiri wokovu. kitu gani kisicho eleweka hapo? mbona kiswahili chepesi kabisa hicho au hamjui maana ya kanisa???
 
Bahatimbaya sana na hatari sana ni mtu kutojijua type yake.Kuna watu humu wanajifanya wanakemea uchochezi kumbe wao ndio wanachochea,wengine wajifanya waerevu na kuwakashifu pamoja na kuwatukana wenzao kumbe wao ndio wapumbavu kabisa na bahati mbaya hawajijui.Ushauri wa bure "Watu wajitahidi kutafakari sana kabla ya kusema lolote na ikibidi kunyamaza ni bora zaidi kuliko kuongea au kuandika upuuzi.Naomba kuwasilisha.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom