Gazeti la Al-Huda lafanya uchochezi

Gazeti la Al-Huda lafanya uchochezi

Status
Not open for further replies.

Credible Viewer

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2015
Posts
444
Reaction score
118
Nimefadhaishwa sana na gazeti la Al-Huda litokalo kila wiki toleo na.523 SHAWWAL1436 la tar23-29, Julai 2015 Uk wa mbele limepambwa na maneno.

Msigwa: CHADEMA kama kanisa
*Asema wanahubiri habari ya wokovu
*Wanachama waislamu sasa mashakani

Kimsingi kauli hizo ni za kichochezi dhidi ya waislam na wakristo! Ifahamike kuwa Mchungaji Msigwa(Mbunge wa Iringa) alitoa kauli hiyo kifalsafa kumkaribisha Lowassa ndani ya Chadema! Msigwa alisema "...CHADEMA ni kama kanisa, hakataliwi mtu, tunahubiri habari njema ya wokovu, unatubu unafanya kazi!"

Mimi siyo msemaji wa Msigwa, lakini nimekerwa na gazeti hilo kwa sababu kauli ya Msigwa haikulenga kutugawa Wanachama wa CHADEMA kwa misingi ya kidini! Ni kama kauli ya Tundu Lissu alipotamka kuwa "...John Pombe Magufuli na kabila lake la MaCCM..." hakulenga kuwa kuna kabila la MaCCM!

Kwahiyo siyo kweli kuwa Msigwa alimaanisha CHADEMA ina wafuasi wa Kikristo pekee!

Naomba mamlaka husika iingilie kati! Mungu Ibariki Tanzania!
DSC09959.jpg
 
Msigwa yeye ni mchungaji
na anajua tuhuma zipo za CHADEMA kuwa chama cha wakristo
hata kama hizo tuhuma si za kweli na za kutunga
hakupaswa kuwa reckless na kuanza kuita CHADEMA kanisa

Mifano ipo mingi ya kufikisha ujumbe

Kutumia mifano ya aina hiyo ni ama uzembe au kiburi na kutokujali kina nani hawatapendezwa
 
The Boss

Rais Kikwete ni Muislamu amewasaidia nini waislamu hadi anaondoka madarakani!? Hilo gazeti linaonekana linatumia plan B baada ya ile plan A ya Mizengo Pinda kuwatumia waislam kwa kuwahadaa na Mahakama ya kadhi kufanikisha ushindi wa CCM!

Tunajua waandishi wengi wa habari wanakadi za CCM si vibaya, lakini hii style inayotumika kuchafua Chadema hapo maana yake wanajichanganya wenyewe, kwakuwa bahati mbaya sana CCM mgombea wao ni mkristo anaitwa John Pombe Magufuli kwahiyo mnatuambia nini!?

Hii ni nchi yetu sote hampaswi kuturudisha nyuma tuchelewe kujadili upuuzi wenu huu wa udini baadaye mtahamia kwenye ukabila mwisho ukanda! Shame on you!
 
Last edited by a moderator:
Usijeshangaa lile jukwaa likaja na tamko la kuwazuia waumini wake wasiipigie kura UKAWA!
 
Credible Viewer

Wewe ndio mchochez,kwani ulijuaje kama Msigwa hakukusudia unacho kikataa wewe? Al huda "wame quote" direct kutoka kwa source,je wewe hio hoja yko kuwa Msigwa hajakusudia "uchochez" ume qoute kwa nani?

Msigwa amekanusha kauli yake au wewe ndo msemaji wake? Hio falsafa kwanini aitumie ya "symbol" ya kanisa?wakat tayar kuna vugu vugu la udini na mivutano ya kidin isio kwisha?

Tena tuhuma nyengine zinaelekezwa hko hko chadema?Kwani Msigwa hakuona falsafa nyengine ya kusema?

Mfano,kwanini msigwa asiseme "Chadema ni kama maji ya kunywa,kila mtu atayahitaji" n.k,Falsafa ya udini haikubaliki hata kama yeye ni mchungaji?

Msigwa ndio mchochozi pamoja na wewe.Al huda ni wasafi,wao wamefanya direct quote from the source.

Njia ni moja,mafikio tofauti.
 
Last edited by a moderator:
Usijeshangaa lile jukwaa likaja na tamko la kuwazuia waumini wake wasiipigie kura UKAWA!

Ndiyo wasivyo na haya wanaweza kufanyahivyo, bado tunakumbuka michezo ya kitoto ya BAKWATA ya Wilaya ya Igunga walipokuja na igizo la hijabu ya Fatma Kimario!
 
Gazeti limeripoti kama alivyosema Mchungaji wa Chadema Msigwa.

Kasema kweli Chadema ni kama Kanisa.

Sasa hapo unalishambulia gazeti kwa kosa gani, wewe umejuaje kama Mchungaji Msigwa alikuwa hana maana hiyo.
 
Msigwa yeye ni mchungaji
na anajua tuhuma zipo za CHADEMA kuwa chama cha wakristo
hata kama hizo tuhuma si za kweli na za kutunga
hakupaswa kuwa reckless na kuanza kuita CHADEMA kanisa

Mifano ipo mingi ya kufikisha ujumbe

Kutumia mifano ya aina hiyo ni ama uzembe au kiburi na kutokujali kina nani hawatapendezwa

Alitoa mfano tu kwani si ndio profession yake? Hiyo ni metaphor na sio simile, hao Al-huda watakua kibiashara tupu kucatch attention za watu
 
Msigwa yeye ni mchungaji
na anajua tuhuma zipo za CHADEMA kuwa chama cha wakristo
hata kama hizo tuhuma si za kweli na za kutunga
hakupaswa kuwa reckless na kuanza kuita CHADEMA kanisa

Mifano ipo mingi ya kufikisha ujumbe

Kutumia mifano ya aina hiyo ni ama uzembe au kiburi na kutokujali kina nani hawatapendezwa
Mkuu The Boss, nimeipenda objectivity yako kwenye hili!.

Pasco
 
Credible Viewer

Ndio maana hua tunaseema waandishi wengi nchini ni makanjanja hawana sifa! Kama ana sifa basi amefanya makusudi kutengeneza uchochezi, na kama haelewi basi sio mwandishi huyo.

Naona hapa kamtazama Msigwa kama Mchungaji na kuangalia mdomo wake unatamka nini na yeye bila kufikiri kahamisha hivyo hivyo. Huu ni ulimbukeni uliopitiliza, hamna mtu ambaye hakumwelewa Msigwa!

Alimaanisha CHADEMA ni kama kanisa kwa maana ya kupokea kila mtu ambapo hata wengine hutubu dhambi zao na kuendelea kupiga kazi ya kumtukuza Mungu basi.
 
Last edited by a moderator:
Credible Viewer

Ni kweli, wakati mwingine, tena kwa makusudi, tunasahau mtu kaongea katika muktadha gani. Kuna aliyemwita au kumfananisha Lowassa na Mtume Mohammed. Inaeleweka kwa kuwa ni muislamu. Angekuwa mkristo pengine angemfananisha na Yesu. Lazima tuangalie context!

All said, lazima kuwa wangalifu na kauli hasa wakati huu kila neno linachunguzwa kwa umakini zaidi!
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom