Gazeti la Al-Huda lafanya uchochezi

Gazeti la Al-Huda lafanya uchochezi

Status
Not open for further replies.
Credible Viewer

Wewe ndio mchochez,kwani ulijuaje kama Msigwa hakukusudia unacho kikataa wewe? Al huda "wame quote" direct kutoka kwa source,je wewe hio hoja yko kuwa Msigwa hajakusudia "uchochez" ume qoute kwa nani?

Msigwa amekanusha kauli yake au wewe ndo msemaji wake? Hio falsafa kwanini aitumie ya "symbol" ya kanisa?wakat tayar kuna vugu vugu la udini na mivutano ya kidin isio kwisha?

Tena tuhuma nyengine zinaelekezwa hko hko chadema?Kwani Msigwa hakuona falsafa nyengine ya kusema?

Mfano,kwanini msigwa asiseme "Chadema ni kama maji ya kunywa,kila mtu atayahitaji" n.k,Falsafa ya udini haikubaliki hata kama yeye ni mchungaji?

Msigwa ndio mchochozi pamoja na wewe.Al huda ni wasafi,wao wamefanya direct quote from the source.

Njia ni moja,mafikio tofauti.

mkuu ku-quote ni sawa ila ile kusema wanachama waislamu matatani ndo inaonekana kama uchochezi coz msigwa hakuzungumzia udini hapo
 
Last edited by a moderator:
Msigwa yeye ni mchungaji
na anajua tuhuma zipo za CHADEMA kuwa chama cha wakristo
hata kama hizo tuhuma si za kweli na za kutunga
hakupaswa kuwa reckless na kuanza kuita CHADEMA kanisa

Mifano ipo mingi ya kufikisha ujumbe

Kutumia mifano ya aina hiyo ni ama uzembe au kiburi na kutokujali kina nani hawatapendezwa

mkuu huyo msigwa wala sio mara ya kwanza kafanya hivyo. hata alivyoshinda 2010 alisema wazi kuwa kanisa limeshinda atafanya kazi ya kulitumikia kanisa la bwana. huyo mleta mada anaweweseka tu. na kwa sababu watanzania ni wasahaulifu tayari miaka 4.5 iliyopita imeshasahaulika. kwa kifupi hakuna jipya hapo bali ni muendelezo tu wa kile alichokisema miaka 4.5 iliyopita.
 
Hawa viumbe wa ajabu sana mchungaji wao kasema Chadema ni kama Kanisa kakiri mweyewe halafu analalamikia gazeti.

"Lowassa ni kama Mohammed"
Ulielewa vp kauli hii ya shekhe wenu
 
kanisa gani hilo! Wewe acha ubabaishaji waislamu walongoza kutangaza kwenye miskiti chadema ni wakristo msiwape kura Mpeni mwenzetu kikwete mwislamu ndio ule ushindi wa kishindo!

Ila JK kawageuka vibaya mpaka wanajuuta kumchagua,madai yao yote kayatia kapuni
 
Mi naona tatizo ni kutaka kila chama cha siasa kikubaliwe na jamii zote nchini. Hii kitu ni ngumu sana kwasababu kila chama huwa na misingi yake. CCM wamepata bahati ya kukubaliwa na jamii karibu zote kwakuwa kilikuwa chama dola na kwa kiasi fulani bado ni chama dola. Hakuna siku watu wa Pwani wataikubali chadema na vilevile hakuna siku middle class itaikubali CUF. Ni kama USA ambako kuna democrats na republicans na kila mtu ana msimamo wake.

Kwahiyo, ni kweli Msigwa hakuwa makini, lakini sioni namna au kitu chadema inaweza kufanya ili ikubalike Pwani. Kuweka viongozi wa juu wanaotokea Pwani ni kama kupaka poda, unalala ukiamka haipo-inabidi upake tena. Ndiyo maana hata UKAWA inakubalika na viongozi kwasababu wanaona kwamba bila umoja hawawezi, lakini tofauti kati ya wafuasi wao ni kubwa kiasi kwamba UKAWA imebaki kuwa ya wenyeviti tu.
 
Nimefadhaishwa sana na gazeti la Al-Huda litokalo kila wiki toleo na.523 SHAWWAL1436 la tar23-29, Julai 2015 Uk wa mbele limepambwa na maneno.

Msigwa: CHADEMA kama kanisa
*Asema wanahubiri habari ya wokovu
*Wanachama waislamu sasa mashakani

Kimsingi kauli hizo ni za kichochezi dhidi ya waislam na wakristo! Ifahamike kuwa Mchungaji Msigwa(Mbunge wa Iringa) alitoa kauli hiyo kifalsafa kumkaribisha Lowassa ndani ya Chadema! Msigwa alisema "...CHADEMA ni kama kanisa, hakataliwi mtu, tunahubiri habari njema ya wokovu, unatubu unafanyakazi!"

Mimi siyo msemaji wa Msigwa lakini nimekerwa na gazeti hilo kwa sababu kauli ya Msigwa haikulenga kutugawa Wanachama wa CHADEMA kwa misingi ya kidini! Ni kama kauli ya Tundu Lissu alipotamka kuwa "...John Pombe Magufuli na kabila lake la MaCCM..." hakulenga kuwa kuna kabila la MaCCM!

Kwahiyo siyo kweli kuwa msigwa alimaanisha CHADEMA ina wafuasi wa kikristo pekee!

Naomba mamlaka husika iingilie kati! Mungu Ibariki Tanzania!

Hizo lawama zako ziende kwa Mch, Msigwa ambaye alishindwa kujitambua na hivyo kutoa kauli bila ya kujali mazingira aliyopo.
 
Credible Viewer

Wewe ndio mchochez,kwani ulijuaje kama Msigwa hakukusudia unacho kikataa wewe? Al huda "wame quote" direct kutoka kwa source,je wewe hio hoja yko kuwa Msigwa hajakusudia "uchochez" ume qoute kwa nani?

Msigwa amekanusha kauli yake au wewe ndo msemaji wake? Hio falsafa kwanini aitumie ya "symbol" ya kanisa?wakat tayar kuna vugu vugu la udini na mivutano ya kidin isio kwisha?

Tena tuhuma nyengine zinaelekezwa hko hko chadema?Kwani Msigwa hakuona falsafa nyengine ya kusema?

Mfano,kwanini msigwa asiseme "Chadema ni kama maji ya kunywa,kila mtu atayahitaji" n.k,Falsafa ya udini haikubaliki hata kama yeye ni mchungaji?

Msigwa ndio mchochozi pamoja na wewe.Al huda ni wasafi,wao wamefanya direct quote from the source.

Njia ni moja,mafikio tofauti.

Ww pia unaweza ukawa walewale, kwanza huo mfano wako wa maji usinge kidhi haja, pia hulazimishwi kuelewa hutaki unapiga chini, tumechoka na uchochezi wenu.
 
Last edited by a moderator:
Siku sio nyingi watataka watu wasiwe wananukuu Biblia, Msigwa alikuwa sahhih kabs nimeshangaa sana kuona uchochezi wa aina hii, hata na hvy mshaanza kuelewa mpaka october mtakuwa mmeshaiva
 
Uelewa mdogo wa mwandishi juu ya matumizi ya 'analogy', 'metaphor', na 'simile' AKA figurative speech; na si ajabu hili kutokea kwenye gazeti hilo.

Waandishi wa gazeti hilo ni wasomi wakubwa tu, wamesoma hadi vyuo vikubwa (madrasa)! Sishangai ufahamu wao ulivyo wa chini.
 
Waandishi wa gazeti hilo ni wasomi wakubwa tu, wamesoma hadi vyuo vikubwa (madrasa)! Sishangai ufahamu wao ulivyo wa chini.

Kusoma ndio wangeandika uharo huo? Hivi mtu akisema Tanzania ni jehannum watu wanakufa kwa shida. Je ni kweli jehannum = Tanzania? Ndio usomi huo?
 
Gazeti limeripoti kama alivyosema Mchungaji wa Chadema Msigwa.
Kasema kweli Chadema ni kama Kanisa.
Sasa hapo unalishambulia gazeti kwa kosa gani, wewe umejuaje kama Mchungaji Msigwa alikuwa hana maana hiyo.
Shuleni ulifundishwa kuhusu "tamathali za usemi"? Kweli ujinga ni hasara. Hivi mtu akitumia tamathali kwamba wewe ni mfupi kama nyundo; mweusi kama chungu;mwekundu kama papai n.k bado unakumbuka hizi tamathali zina maana gani kweli? Au ndio shule ilikupita kushoto? Kweli shule muhimu!
 
Siyo kweli mdau. Nenda tena kaisome kauli ya Msigwa. Kwenye siasa huwezi kutegemea hadhira ndo iamue ulimaanisha nini. You have to be as clear as possible. Na kwa vile kauli hii imeleta utata, Msigwa inabidi afafanue alimaanisha nini. Hii ni Politics 101 hasa kwenye ishu ya crisis/scandal management and containment. Kuna ugumu gani kufanya hivyo na kuwakata ngebe hawa wapenda udini? Mtatoa povu tu eti tamathali. Tamathali si tamathali haijalishi kwa hali ikivyofikia sasa na msipoangalia inaweza kuwacost kura kibao.
 
Watanzania hebu tuwe na hekima sasa huu udini umevuka mipaka.Sikutegemea kama kauli hii italeta mjadala mkubwa hivi!Huu ni mfano unaohusisha jambo lililopo.Tanzania kuna nyumba za ibada,kanisa mojawapo na linajulikana,hata uwe si mkristo.Hoja ya Msigwa imejikita kwenye mstari unaofuatia baada ya kulitaja kanisa,ile kazi ya kuhubiri wokovu kwa kila mtu na kumkaribisha anayeupokea wokovu huo na kutubu halafu na yeye akajiunga kufanya kazi ya kuokoa wengine,hii ni ishu ambayo iko unique kwa kanisa zaidi ya nyumba nyingine za ibada.Sasa nani amewahi kusikia habari za kuokoka zikihubiriwa misikitini au kwenye temple za budha?

Hiyo kazi ya kanisa ndio hasa Msigwa anaifananisha na kazi ya CHADEMA kwenye siasa za Tanzania,kuikomboa (wokovu) nchi toka mikononi mwa viongozi wabovu,katika kazi hiyo mtu yeyote hata kama katoka huko kwa wabovu alimradi ameelewa na kukubaliana na sera ya CHADEMA,basi anasamehewa na kujiunga na ukombozi!Ukitazama hapo utagundua,kazi ya wokovu ya kanisa ni the best,simple and very familiar example kwake yeye Msigwa na kwa watz kumwelewa kutokana na umaarufu wa kanisa kwenye mambo ya "wokovu".Ni sawa na jinsi tunavyoambizana huku mitaani,eti "unavua viatu kwani uko masjid hapa?"why?kwa sababu katika mazingira ya jamii yetu ambamo majority ni wafuasi wa dini hizi,ukizungumza habari ya kuvua viatu masjid utaeleweka haraka,maana hilo ni popular na waislam ni popular na nyumba ya ibada inayoitwa msikiti ni very popular,na utaratibu wao wa kuvua viatu msikitini ni jambo linajulikana na kueleweka sana kwa mtz yeyote kukuelewa vizuri zaidi.Hata kwenye semi zetu kuna ule unasema "ukicheza na mbwa atakufuata hadi msikitini".

Mbona hatuhangaiki kujiuliza ni kwa nini umetajwa msikiti hapo badala ya kingine chochote?mimi sihitaji kujiuliza maana nishaulewa usemi haraka tu pamoja na kuwa si muislamu lakini ninaishi na uislam katika jamii yangu,nimeishi nao bongo tangu mdogo nasikia adhana alfajiri,alasiri na jioni,sawa tu na kengele za makanisa za saa sita mchana,na ndio maana nimemuelewa Msigwa bila shida,sasa inaleta mantiki kweli tukianza kulalamikiana masuala kama haya?halafu mchungaji kataja kanisa imekuwa tabu,tunasahau uanasiasa wake,mbona hatuoni tabu kwa Al huda kuipa mtazamo mmoja tu wa hasi habari hii?kwa nini imekuwa rahisi kuibeba tafsiri ya Al huda badala ya kuchukua mfano wa Msigwa kiurahisi ulivyo?kwa hiyo hata akina Kikwete wazuiwe kutolea mifano misikiti kisa wao waislam?mnaenda wapi watz?

kuna watu humu ni watu wazima,wana elimu na exposure ya kutosha,ila nashangaa wanavyoweka tunu zao kando na kujivunjia heshima kwa sababu tu ya politiki.Mnawagawa watz kwa sababu ya maslahi ya kisiasa.Kauli ya Msigwa ni rahisi sana ila angalia watu wanavyoifanyia kazi ya "kitengo" humu kisa tu imetoka CHADEMA.kwani Tz hakuna makanisa?hayastahili kuzungumziwa mifano?kwa nini iwe chaos likitajwa kanisa na CHADEMA?Kuna sheria inawapiga marufuku CHADEMA kutaja kanisa? au mmewatengenezea mazingira tu?@ritz and co mnanisikitisha sana.Waoneeni huruma watoto wenu,muwarithishe nchi ile ile ya amani mliyopokea toka kwa baba zenu.Huo ni uislam wenu nyinyi wala sio wa Allah.Mwenyezi Mungu hafundishi watu kuwa wachonganishi.
 
kumbe ni kweli alisema,sasa uchochezi wake upo wapi ikiwa ww mwenyewe unakiri kwamba alisema?
 
Siyo kweli mdau. Nenda tena kaisome kauli ya Msigwa. Kwenye siasa huwezi kutegemea hadhira ndo iamue ulimaanisha nini. You have to be as clear as possible. Na kwa vile kauli hii imeleta utata, Msigwa inabidi afafanue alimaanisha nini. Hii ni Politics 101 hasa kwenye ishu ya crisis/scandal management and containment. Kuna ugumu gani kufanya hivyo na kuwakata ngebe hawa wapenda udini? Mtatoa povu tu eti tamathali. Tamathali si tamathali haijalishi kwa hali ikivyofikia sasa na msipoangalia inaweza kuwacost kura kibao.

hivi ungetajwa msikiti,kungekuwa na mada hii saa hizi hapa?why kanisa mkuu?njia ya kuwakata ngebe si kushauri watu waache kutaja mifano ya kanisa,bali waichukulie mifano hiyo katika usahihi wake sawa tu na kama ungetajwa msikiti.Likitajwa kanisa au msikiti halafu minung'uno ikaanza kama hivi,hatuko salama.Ni lazima kanisa na misikiti itajwe na watu wawe na amani bila kustuka.Ndio uhuru wenyewe.Msigwa ni mtanzania huru.Ila baadhi ya watz waliomsikia hawako huru,ndio maana manung'uniko.Tuwaweke huru,siku nyingine wakisikia kanisa waendelee na kazi zao bila shida.
 
Nadhani uelewa mdogo na ushabiki wa kidini ndio unasumbua watu hapa, kama tungechukua mda na kutafakari hata kama msigwa alimaanisha kanisa basi watu wote walitakiwa kufurahi kwa sababu kanisa tunaamini ni mahali pa ibaada na mahali panapo fundisha maadili mema! Waislam hampendi maadili mema? Utakuta wote wanaoshabikia huu mtangamano msimamo yao na vitabu vya dini haiko sawa! Kanisa ni mahali pa ibaada, msikiti ni mahali pa ibaada, tofauti ni lugha tu, na mafundisho karibu yote ni yaleyale yakiwa na chembe chembe ndogo sana, nashangaa watu kucapitalize katika hizo tofauti ndogo kuliko kutafuta umoja katka mambo mengi yanayo fanana ndani ya ukristo na uislam.
Msigwa kama former pastor maneno yaliyomjaa niya kikanisa kanisa, sidhani kama ni vizuri kujaribu kumuelewa kichochezi wakati kuna alternative ya kumuelewa positively.
Nadhani wenzetu waislam mpunguze munkari, muwe objective, down to your hearts mutaona logic na connection ya kile alicholenga.
Vinginevyo kama una preconceived ideas, siku zote utapata sababu halisi ya kudhihirisha kile unacho kidhania, kila msemo waweza kuwa na maana za pande mbili
 
Nimefadhaishwa sana na gazeti la Al-Huda litokalo kila wiki toleo na.523 SHAWWAL1436 la tar23-29, Julai 2015 Uk wa mbele limepambwa na maneno.

Msigwa: CHADEMA kama kanisa
*Asema wanahubiri habari ya wokovu
*Wanachama waislamu sasa mashakani

Kimsingi kauli hizo ni za kichochezi dhidi ya waislam na wakristo! Ifahamike kuwa Mchungaji Msigwa(Mbunge wa Iringa) alitoa kauli hiyo kifalsafa kumkaribisha Lowassa ndani ya Chadema! Msigwa alisema "...CHADEMA ni kama kanisa, hakataliwi mtu, tunahubiri habari njema ya wokovu, unatubu unafanyakazi!"

Mimi siyo msemaji wa Msigwa lakini nimekerwa na gazeti hilo kwa sababu kauli ya Msigwa haikulenga kutugawa Wanachama wa CHADEMA kwa misingi ya kidini! Ni kama kauli ya Tundu Lissu alipotamka kuwa "...John Pombe Magufuli na kabila lake la MaCCM..." hakulenga kuwa kuna kabila la MaCCM!

Kwahiyo siyo kweli kuwa msigwa alimaanisha CHADEMA ina wafuasi wa kikristo pekee!

Naomba mamlaka husika iingilie kati! Mungu Ibariki Tanzania!

unakubali nini unakataa nini chungeni ndi zenu
 
Kwa nini unahangaika kitu kinajieleza chenyewe? Msigwa kasema Chadema no Kanisani kila mtu anaruhusiwa akitibu. Kwa nini asisema ni kama Msikiti kila mtu huja kupmba dua? Hivi samahani kuuluza ' Msigwa anachunga nini khasa? Tundu Lissu ana akili timamu anajua CCM siyo kabila lakini CHADEMA ni kabila fulani sasa anataka kujibaraguza. Basdaye si alisema Makufuli si Msukuma ni Mzinza? Where do we get these cheapies? WM
 
Gazeti la Mwananchi, Nipashe, Tanzania Daima yote yameandika hii habari yeye kalichagua Al-Huda tu.

Hawa jamaa wana chuki sana

Hayo magazeti ya Mwananchi, Nipashe, Tanzania Daima hayakulenga ujinga ulioandikwa kwenye gazeti la Al-Huda! Al-Huda wanaonekana wameichukulia kwa mtazamo hasi kauli ya msigwa! Ni mambo haya ndiyo yanatuchelewesha ya kujadili upuuzi kama huu, isijekuwa hii ni mbinu ya CCM kuhamisha mjadala tuchelewe kuparurana wenyewe kwa wenyewe kujadili ujinga kama huu wa udini! Mbinu hii chafu haikubaliki, na hatuikubali vinginevyo labda Gazeti husika waje na majibu ya kina watuambie lengo lao lilikuwa ni nini kutuchonganisha wakristo na waislamu!? Kwani ndani ya CCM, CUF, NCCR-Mageuzi, ACT-Wazalendo hakuna wakristo huko!?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom