Kazi za Kanisa zinafana na kazi za Chadema?
Wewe ndo umepotea kabisa na pengine wewe ni miongoni mwa waandishi wa gazeti hili!!
Unauliza amejuaje kama Msigwa alimaanisha hicho alichokisema mleta mada!?
Wewe hujui kusoma au kusikia na kisha ukapata mantiki (logic) ya kilichosemwa au kilichosikika?
Kama wana natatizo ya tafsiri ya mantiki kama uliyonayo wewe, hata km wangemsikia kasema "CHADEMA ni kama maji....,...................." wasingeelewa na wangekuja na tafsiri potofu tu ili mradi tu nia na lengo lao ovu litimie!!
Kubali tu ndugu yangu, gazeti hili limechemka na kujishushia hadhi na nadhani wana malengo ovu/baya nyuma yake especially kwa Msigwa mwenyewe na chama chake!
Hakuna namna nyingine unavyoweza kusema dhidi ya hili gazeti zaidi ya alichokiona mleta mada, and I agree with him/her!
Fisadi dawa yake jela kama kina Yona kauli ya Mchungaji Msigwa ipo wazi wala haitaji maelezo period.Mojawapo ya kazi za kanisa ni kuwafundisha watu wawe huru na utumwa wa dhambi ni sawa na chadema inavyofanya
inawaambia mafisadi ukweli na wanaojitambua wanahama chama.Ndicho alichokuwa anamaanisha Msigwa
Gazeti la Mwananchi ili hapa soma.Hili gazeti linatoka nchi gani...msaada tafadhali
Hajakukera Mchungaji Msigwa kufananisha Chadema na Kanisa likukere gazeti.Hata mm hiyo kauli imenikera...
Magazeti zaidi ya kumi yameandika hii habari au nikuwekee?
mbona mnataka kumsemea msigwa?
Mwenyewe kasha sema chadema ni kanisa, wanahubiri wokovu. kitu gani kisicho eleweka hapo? mbona kiswahili chepesi kabisa hicho au hamjui maana ya kanisa???
Mafisadi na majambazi wamejaa huko ccm akina Chenge,Ngeleja,Tibaijuka ,Lowasa n.k mmeshindwa kuwapeleka mahakamani?Fisadi dawa yake jela kama kina Yona kauli ya Mchungaji Msigwa ipo wazi wala haitaji maelezo period.
hayo magazeti nikawaida sana kuchochea waumini wa dini mbalimbali...
The Boss
Rais Kikwete ni Muislamu amewasaidia nini waislamu hadi anaondoka madarakani!? Hilo gazeti linaonekana linatumia plan B baada ya ile plan A ya Mizengo Pinda kuwatumia waislam kwa kuwahadaa na Mahakama ya kadhi kufanikisha ushindi wa CCM!
Tunajua waandishi wengi wa habari wanakadi za CCM si vibaya, lakini hii style inayotumika kuchafua Chadema hapo maana yake wanajichanganya wenyewe, kwakuwa bahati mbaya sana CCM mgombea wao ni mkristo anaitwa John Pombe Magufuli kwahiyo mnatuambia nini!?
Hii ni nchi yetu sote hampaswi kuturudisha nyuma tuchelewe kujadili upuuzi wenu huu wa udini baadaye mtahamia kwenye ukabila mwisho ukanda! Shame on you!
Gazeti limeripoti kama alivyosema Mchungaji wa Chadema Msigwa.
Kasema kweli Chadema ni kama Kanisa.
Sasa hapo unalishambulia gazeti kwa kosa gani, wewe umejuaje kama Mchungaji Msigwa alikuwa hana maana hiyo.
Gazeti la Mwananchi ili hapa soma.
Chadema ni kanisa la wokovuAkizungumzia taarifa hizo, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa alikifananisha chama hicho na kanisa ambalo kwa kawaida halikatai mtu, bali linawapokea wenye dhambi na kuwaongoza kufanya toba."Chadema ni kama kanisa, hakataliwi mtu, tunahubiri habari njema ya wokovu, ukija hapa unatubu unaendelea kufanya kazi," alisema Mchungaji Msigwa.