Gatho Beevans: Mkongwe wa Muziki nchini Congo

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Wakuu,

Huyu jamaa ni mmoja kati ya watu waliotoa albums zao zikafanya vema miaka ya 90, akiwa na kina Tshala Muana. Nilikuja kufuatilia habari zake nikaambiwa kwa sasa anaishi Atlanta GA kutokana na matatizo ya Congo.

Kuna vibao kama Ngoma ya Kwetu



Na Azalaki awa
Yupo hai? What does he do for living? Roulette, una taarifa za huyu jamaa?
 
Last edited by a moderator:
Sikonge, naamini nawe enzi hizi uliburudika nami; what happened to Gatho Beevans?
 
Last edited by a moderator:
Invisible,

Lazima nikiri kuwa huyu Mwana muziki alinipita kushoto sana. Tatizo kubwa ni kuwa wakati akisitesa kwenye anga za Africa, mie nilikuwa nimeondoka kidogo na kuishi ughaibuni na huko kupata miziki ilikuwa kasheshe.

Ilitokea sherehe moja ya Watanzania na nikamuomba Marehemu Jafar wa JF. MSIBA WA JAFAR WA JF (msiba wa siku nyingi) anitumie miziki kadhaa ya Kiafrica kwa sababu alikuwa amekwenda kusoma Belgium. Alinitumia kweli Cassete kadhaa na moja wapo ikiwa ni hiyo ya wimbo wa "ngoma ya kwetu." Kwenye sherehe nikampa DJ aupige na kwa shida sana akakubali. Ulipoanza tu kijana mmoja alikuja na kuanza kunieleza jinsi huo wimbo ulivyomrudisha mbali sana nyumbani. Kutoka hapo ndiyo nikawa nimeguswa na kuelewa sasa kumbe jamaa yupo juu sana.

Pana sehemu nilipata CD ya miziki ya Kiafrica na sikujali sana ndani kuna nini na akaja dada mmoja nikampa kopi. Mie ndani nilikuwa nimeupenda wimbo wa Dezo Dezo - Tshala Muana. Ila yeye ndani akaupenda wimbo wa Azalaki Awa. Akaniuliza kama ninazo nyingine na ukweli sikuwa nazo.

Kusema ukweli nimemfahamu huyu Mwana muziki juu juu tu na sikuwahi kuwa kwenye sherehe ambazo watu walicheza na kufurahia miziki yake. Kisa kingine cha kutokumpenda sana ni kule ku-Copy kwake sana Michael Jackson. Anyway, hilo ni tatizo langu mie ambaye nimeshazoea HIGH QUALITY ya Usanii kuanzia Recording, Video making, uchezaji, uvaaji nk.

Ila kwa hali ya nyumbani, nampa sifa sana kwani alijitahidi kuweka jina lake. Mara nyingi Wa-Congo wakipata visenti wanatumbua hadi vinaisha. Mwisho unaweza kumkuta kashakuwa Mbeba Box (sisemi anabeba box).

Kwa ufupi sina habari zake na labda nianze kufuatilia. Kwa Congo inaweza kuwa ngumu sana kwa Sababu Wacongo wanajali zaidi Mwanamuziki anayeimba kwa Kilingala au Kikongo tu. Ukianza kuimba lugha za watu, wanakuweka pembeni.

Nafikiri tatizo lake kubwa lilikuwa ni lilelile kama la Emeneya, Yondo Sister, Mayoni Mayaula, Defao nk kwa kutokuwa na Band yake maalumu na anabaki kuwa Mwanamuziki wa Kuunga-unga. Nafikiri hii huwa inaleta sana shida unapokwenda kwenye Concert LIVE na unakuwa huna wanamuziki waliopiga wimbo Original na mwisho hata uimbaji unakuwa mwingine kabisa utafikiri Band nyingine wanaku-copy. Watu wanakuchoka na kuanza kukimbia Concert zako na ndiyo mwisho wako kwa sababu kwa Africa huwezi kuishi kwa mauzo ya CD maana Wahindi ndiyo wanatajirika nazo, wewe utabaki na Concert na hizo sasa ukikosa, ndiyo umekwisha.


Sikonge, naamini nawe enzi hizi uliburudika nami; what happened to Gatho Beevans?
 
Mkuu, huyu jamaa was a Michael Jackson fan and wanted to demonstrate that another type of Congolese music was possible. Kuna hata a lingala version of "Bad (who's bad) that he sang, mi sikuipenda coz it wasn't so original.

Mapema in the 90's ali-retire from music and the last time I heard of him he was doing his MA in business administration in the US where he lived with his family. Umenikumbusha, I'm still to share with you my Papa Wemba collection, ila tatizo you are nowhere to be seen, you are Invisible. Sijui itakuaje hapo. lol
 
Mkuu, huyu jamaa was a Michael Jackson fan and wanted to demonstrate that another type of Congolese music was possible. Kuna hata a lingala version of "Bad (who's bad) that he sang, mi sikuipenda coz it wasn't so original. Mapema in the 90's ali-retire from music and the last time I heard of him he was doing his MA in business administration in the US where he lived with his family. Umenikumbusha, I'm still to share with you my Papa Wemba collection, ila tatizo you are nowhere to be seen, you are Invisible. Sijui itakuaje hapo. lol

Wasn't that FELIX WAZEKWA?

Felix-Wazekwa_HautLesMains.jpg
 
Mkuu Safari,

Nafikiri aliyekuwa akijifananisha zaidi na Michael Jackson na hata kuimba "Who's Bad Whos Bad" alikuwa Stino wa Viva La Musica, band iliyoanzishwa na Papa Wemba na baadaye akamwachia Reddy Amisi na huyo Stino.

Band hii ni kama Zaiko Langalanga B kwa sababu imezalisha pia wanamuziki wengi wazuri kama Koffi Olomide aliyepita hapo kwa muda mfupi.



Koffi Olomide akiwa Yanki na Papa Wemba:

 
Mkuu Safari,

Nafikiri aliyekuwa akijifananisha zaidi na Michael Jackson na hata kuimba "Who's Bad Whos Bad" alikuwa Stino wa Viva La Musica, band iliyoanzishwa na Papa Wemba na baadaye akamwachia Reddy Amisi na huyo Stino.

Band hii ni kama Zaiko Langalanga B kwa sababu imezalisha pia wanamuziki wengi wazuri kama Koffi Olomide aliyepita hapo kwa muda mfupi.

Basi kaka.....na iwe bisonyoso ya mobali te?
 
Last edited by a moderator:
mimi sikumfagilia kihivyo huyu jamaa kwani haiba yake ilikuwa ya kike kike hivi,hata hivyo siwezi kuacha kukumbuka kibao chake cha azalaki se awa kwa sababu kilikuwa kinapigwa mno!
 
Beevans Gatho kama alivyorambulika alitamba sana hapa kwetu katika medani ya muziki ulotoka Congo mwanzoni mwa miaka ya 90.

Gatho alikuwa haendani na mtindo uliokuwa unatamba miaka hiyo huko Congo wa Soukous, lakini alijidhihirisha ubora wake na kufanya vizuri katika Soko la hapa kwetu Tanzania.

Sina uhakika kama alipenya vyema katika nchi nyingine za Africa lakini kwa hapa kwetu Gatho alifanya Vizuri sana.

Miongoni mwa nyimbo ambazo Gatho alipata kutamba nazo ni:..
Azalaki awa
coupe de foudre
Limbisa nga
Ngoma ya kwetu
Na nyimbo yake ya Ambiance agogo ambayo ilikuwa imebamba sana kipindi Corner Bar pale Africa sana ilipokuwa inafunguliwa mpaka kupelekea Bar hiyo mpaka sasa inafahamika pia kwa jina la Ambiance.

Nakumbuka siku hiyo ya ufunguzi nilikuwa nimeutwika mtungi yaani nililimong'onyoa uno wimbo huo ulipokuwa unapigwa mpaka kishtobe niliekuwa nae akaja kunitunza.

dah leo hii nikikaa kwenye mkeka lazima nijifikirie mara mbili mbili kuinuka.
Ama Kweli uzee wa Sokwe ni tofauti na ujana wa Nyani.
 
Kama Gatho ni mkongwe akina Kabasele Yampanya, Franco, Nyboma, Aurlus Mabele, Theo Blaise Kounkou, Wuta Mayi, Yondo Sister, Simaro Lutumba Massiya, Carlyto Lassa, Alain Kounkou, na Papa Wemba kutaja kwa uchache watakuwa nani?
 
Kama Gatho ni mkongwe akina Kabasele Yampanya, Franco, Nyboma, Aurlus Mabele, Theo Blaise Kounkou, Wuta Mayi, Yondo Sister, Simaro Lutumba Massiya, Carlyto Lassa, Alain Kounkou, na Papa Wemba kutaja kwa uchache watakuwa nani?
Mkuu hukunisoma vema, mpaka nimesema miaka ya 90 manake si mkongwe kivile lkn ukongwe wake nimeulinganisha na vijana wa sasa katika Muziki wa ki-Congo.

Otherwise, kina François Luambo Makiadi na Madilu System huwezi kulinganisha na kinda huyu :)
 
Nakubalina nawe ingawa hiyo miaka ya 90 unayosema ilitawaliwa na baadhi ya niliowataja kama Aurlus Mabele, Pepe Kalle, Nyboma na Papa Wemba Jules Wembadio Shungu le grand Contoumier du la Village Morokai.
Mkuu hukunisoma vema, mpaka nimesema miaka ya 90 manake si mkongwe kivile lkn ukongwe wake nimeulinganisha na vijana wa sasa katika Muziki wa ki-Congo.

Otherwise, kina François Luambo Makiadi na Madilu System huwezi kulinganisha na kinda huyu :)
 
Waungwana thread imenikuna manake haya ni mambo yangu sana ila technology inanichenga kidogo, nashare vipi youtube video na ionekane video hapa (kama hizo za Invisible) na sio link? Nina multi-quote vipi? Aaaaghhhh!
 
nilimpenda sana Gatho na nilifuatilia habari zake kwa karibu, nakumbuka habari ya mwisho kumhusu yeye na ya kusikitisha ni kukamatwa kwake nchini Ufaransa na madawa ya kulevya ndani ya ,gitaa akahukumiwa kifungo kirefu
 
Back
Top Bottom