Gari ya Kipanya iwe usafiri rasmi wa Rais Samia

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,488
20,444
Heri ya idd ndugu zangu.

Tanzania ni moja ya nchi chache Sana duniani ambazo tunatengeneza Magari halafu official state car bado tunatumia gari za nchi nyingine.

Viongozi wakuu wa nchi za Marekani, ujerumani, Japan na Uingereza viongozi wao wanatumia kampuni za nyumbani.
images (20).jpeg


Bibi la Bibi Elizabeth akipush Land Rover.
download (2).jpeg

Gari yakansela wa Ujerumani
菅内閣総理大臣警護車列_内閣総理大臣専用車_60系センチュリー.jpg


Gari ya kijapani kwa ajili ya waziri mkuu. Kuna faida zaidi ya moja kwa mama Samia kutumia Gari ya Kipanya.
images (22).jpeg
images (21).jpeg

1. Kutoa ajira kwa vijana wa Kitanzania na kulinda fedha zetu za kigeni

2. Kuepuka njama ovu za mabeberu- huwezi kupima marinda Watanzania halafu kesho unaenda Marekani kununua gari ya rais Detroit . Hii inaweza kuwanya mabeberu- kukupa gari inayotumia nusu saa kufunga breki na hivyo kuhatarisha usalama wa mama.

3. Kupunguza gharama. Gari ya Kipanya Mwanza Dar inatumia luku ya elfu 20.

4. Kuendana na viwanda vingine-baada ya mama kumsaini mkataba wa uchimbaji Cobalt kwa ajili ya utengenezaji betri za gari, hii itasaidia upatikanaji kwa urahisi malighafi nchini pia kukamilika kwa bwawa la Nyrere kutahakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika.

5. Kusupport royal tour kwa njia ya indirect.
6. Rangi ya Gari kuendana na rangi ya ushungi wa mama. Kama utani lkn rangi ya Gari kufanana na mavazi ya mama inaongeza usalama. Gari ikiwa nyekundu na mama akavaa ushungi mwekundu inam camouflage, pia inaongeza unadhifu.

Mama anakuwa ana Gari la tano standby.
 
wanakuambia eti kipanya anaunga unga gari na hajabuni.

kitu ambacho hawajui ni kuwa kuna kampuni nyungi za utengenezaji magari ambazo hununua spare parts kutoka viwanda nguli vya vyuma

mfano. Volkswagen- wananunua engine spare parts kutoka kwa Dutch machines

Kama unaona anachofanya masudi ni simple kwanini usifanye wewe?

Nchii imejaa watu wenye sumu wasiojua kuwa ni ngumu kuanzisha kitu ila ni rahisi kubomoa
 
Hivi huyo Masoud alitengeneza hii gari kwa kuzalisha (manufacture) vifaa au alinunua injini na vitu vingine kisha kuviungamanisha (assembling)? Nauliza hivyo kwa sababu sidhani kama tunavyo viwanda vya kuzalisha chuma mbali na vifaa vya ujenzi. Kama alifanya assembling basi hakuna uvumbuzi wowote hapo.
 
Tatizo la kutaka onekana wewe ndo waweza kila kitu.
Kuanzia jina etc kataka aonekane yeye ila lile dude ni baya sana.

Arudi darasani awekeze nguvu kwenye research and development ili kuweza fanya design ya body, interiors, suspension, chasis, electronics, aerodynamics etc
 
kuna kiongozi mmoja alisikika akisema hilo ni kanyaboyaaa .... anatafta upigaji wa hela
 
wanakuambia eti kipanya anaunga unga gari na hajabuni.

kitu ambacho hawajui ni kuwa kuna kampuni nyungi za utengenezaji magari ambazo hununua spare parts kutoka viwanda nguli vya vyuma

mfano. Volkswagen- wananunua engine spare parts kutoka kwa Dutch machines

Kama unaona anachofanya masudi ni simple kwanini usifanye wewe?

Nchii imejaa watu wenye sumu wasiojua kuwa ni ngumu kuanzisha kitu ila ni rahisi kubomoa
Tanzania tunakuwa kama kichekesho cha dunia. Mtu anaungaunga mabati anaweka na motor yenye kuzungusha matairi na inakuwa habari ya nchi nzima kuwa fulani katengeneza gari!
 
Na hakika hata kipanya mwenyew hawezi Tumia hilo Gari for his daily use
 
Back
Top Bottom