stephot
JF-Expert Member
- Mar 1, 2012
- 18,114
- 28,015
Nimekuwa nikiendesha magari ya automatic (sijui kwa manual gear) kwa muda mrefu,nimepata tatizo na hii ni mara ya pili kunitokea kwa gari tofauti,mafuta(Petrol) inapokuishia gari likiwa kwenye mwendo brake zinakataa kabisa kushika,bahati yangu ni kuwa huwa inanikuta mahali pasipo na mteremko mkali na mbele yangu hakuna gari hivyo inakwenda na kusimama yenyewe ndipo ninaiweka gear kwenye P na kufunga handbrake.Sasa kwa wenye ufahamu naombe tupeane maujuzi nini kifanyike unapokutwa na tukio kama hilo!