Msaada wa Garage nzuri ya Mercedes

Msaada wa Garage nzuri ya Mercedes

crayvt

Member
Joined
Dec 11, 2015
Posts
34
Reaction score
88
Wadau habari zenu,
Naomba kuulizia garage nzuri kwa gari ya Mercedes benz ukiachana na akina CFAO and co.
Gari yangu C class w204 ilikua free of problems nikawa namtumia fundi mmoja kwaajili ya services na vitu vidogo. Recently gari ilikua ina knock baada ya kuikagua hata mwenyewe niliona ball joints zimekufa. Fundi huyu akaja kunisaidia kuzibadili, lakini pia akagundua brake pads zimekaribia kuisha nikasema tuzibadili tu zote as a preventive measure.
Kuanzia hapo shida ya kwanza alipokua anafunga brake kwa maelezo yake ilikua hai-bleed ya upande mmoja mbele na baada ya kuhangaika nayo kwa siku 3(sikuwepo) akaniambia master cylinder imekufa hivyo tubadili. Ikabadilishwa brake zikawa vizuri lakini taa ya abs ikabaki licha ya jitihada za kufanyiwa calibration mara kadhaa mwisho akasema inawezekana module imekufa maana hats cruise control, run flat tyre na features zingine zilikua hazifanyi kazi tena sababu ya abs.
Few days tu baada ya kuitumia licha ya taa ya abs kuwaka ghafla ikazima na kukataa kuwaka akaja kuichukua maana nilikua nawahi kazini, baada ya kuiangalia wakaniambia ni SAM ya mbele kulia, tukaibadili kwa gharama kubwa. Ikapona kwa masaa ikawa inatembea lakini check engine ikawaka, na gari ikawa ina crank kwa muda kidogo ili kuwaka. Nikasema wacha nitafute garage nzuri maana hii ishakua shubiri. Niliporudi baada ya wiki kuwasha gari haiwaki kabisa ina crank tu, nikamuita aje aicheki ili ikiwaka ndo nitafute pa kuipeleka. Alipokua akasema fuel pump imekufa na this time alikuja na fundi mmoja maarufu tu😃. Ikabadilishwa, gari ikawaka na kutembea kama km 3 hivi kisha kuzima tena. Baada ya kuicheki na kufungua top cover now naambiwa gear zimelika sijui zinarusha chain, sababu ilikua ina leak oil pasipo kujua hivyo hiyo ndo shida na sio fuel pump nliyonunua almost 350k. Nimewambia wairudishe waipaki.
Sasa msaada wa garage nzuri tukaanze.

Nawasilisha.
 
Mercedes-Benz 204 unaita fundi nyumbani mkuu wa spana mkononi, lazima akuharibie gari. Ilitakiwa aje afanye computer diagnosis, gari ingemwambia matatizo yote kabla ya kuanza kuichokonoa.
Anyway Autotronic Bamaga, waje waicheki kwa vifaa, wakiendelea mafundi Mangungu kuichokonoa hiyo gari unapaki mkuu.
 
Nikilisolve nitakuleteeni mrejesho.
Huwa naona landrover, benz na bmw nyingi pale Keko / kurasini nafikiri ni mafundi wazoefu.

Kimara stop over ile service road ya upande wa kuja mjini baada ya kuvuka kituo cha mafuta na kabla ya kufika kimara mwisho, mkono wa kushoto huwa kuna jamaa anatengeneza benz na bmw, nazionaga nyinginyingi pale.

Mikocheni, kuna yule jamaa anaitwa Jesse (Automax garage) nae huwa nasikilia yuko poa.
 
Back
Top Bottom