Gari ni muhimu sana katika mapenzi

Applicant

JF-Expert Member
Feb 12, 2020
1,962
1,746
Kwanza wanawake wa sasa hivi wenyewe wanaangalia cha kwanza gari, hata ukipishana nae mtaani ukiwa ndani ya gari yako unamng'oa chapu tu, na ninachowapendea wanawake hajiulizi gari ni lako au umeazima, yeye akikuona unadrive tuu umevaa shati lako safi limepigwa pasi likakubali, anajua ni lako na anaona labda wewe ni kigogo fulani au mfanyabiashara mkubwa, gari ni muhimu jamani.

Wewe hata uwe na viwanja vingapi, ukipita mtaani watoto wazuri hawatajua kama una kiwanja au nyumba.

Juzi nakatiza zangu mitaa fulani nipo ndani ya ndinga, mtoto mkali akapita nikapiga honi mara moja tuu nikapaki pembeni, mtoto huyo akaja, nikashusha kiyoo maongezi machache tuu namba hii hapa nikasave, na lifti nikampa, na mabusu motomoto kwenye gari manusura nilete ajali barabarani maana ilikua hatari sana.
 
Back
Top Bottom