Gari la mkopo laibiwa

Gari la mkopo laibiwa

Jamani kuna rafiki yangu alichukua mkopo wa gari aina ya NOAH kutoka bank ya CRDB na aliweka nyumba yake kama dhamana, lakini kwa bahati mbaya gari lenyewe limeibiwa jana maeneo ya Kongowe na mbaya zaidi gari lenyewe lina muda wa miezi miwili tu tangu aanze kulitumia.

Yaani mshikaji kadata balaa hajui afanye nini? na bank kama kawaida wanataka chao tu. Wakuu tusaidiane kumshauri huyu mwenzetu.

Kwanza nataka kujua alikopa Noah kwa ajili ya biashara au kutanulia? Kwa vyovyote imeshakwenda, basi na nyumba hawezi kuuza manake ipo kama dhamana, hivyo akope tena kwa rafiki arudishe Noah ya watu kama anataka kusevu nyumba.

Asiumize kichwa kumkopa mtu mmoja milioni 10 ni vigumu, anapaswa kukopa watu hata 10 kila mmoja M1 au 2 na arudishe hela hizo polepole ndani ya miaka 2 hivi matatizo yatakuwa yamekwisha.

Akope hasa kwa marafiki wa kweli au kwa ndugu wajomba, shangazi, n.k. hawa hawa watamwonea aibu kuchukua nyumba yake.

Ningemkopesha lakini lazima aweke nyumba yake mikononi mwangu na nyumba hiyo tayari benki imeshaiweka kibindoni.
 
Hiyo ni genuine case ambayo inaeleweka pia kama gari na mkopo vilikuwa na bima kubwa wala asihofu cha muhimu ni kutoa ripoti haraka polisi, bima na benki alikokopea
 
Gari ina BIMA. Afanye process tu. Ila, issue yakuweka dhamana ya Nyumba nayo sijaikubali sana.
 
Wabongo wanavyopenda magari, yaani wangekuwa wanaruhusu kuweka mke rehani wangemuweka ili tu wapate mkopo wa kununulia gari
 
akili nyingine za ajabu kabisa.unachukuaje mkopo wa gari kwa kuweka dhamana nyumba? hii nyumba itakuwa ya uridhi na sio jasho lake.hapo ndo alichemka.
 
Umeongea vizuri sana........ila nina wasiwasi na mtoa thread...........kama sio zogo anapiga.........basi huyo rafiki yake ni mbulula nambari one........kuweka rehani nyumba kukopa gari............

If this profile picture is your real picture (let's hope so), then your comment is as beuatiful as you are!!!
 
Back
Top Bottom