Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,886
- 6,883
Hali Tete Uchaguzi Mdogo Igunga; Magari Ya CCM Yapigwa Mawe
Mbuge wa Mtera, Livingstone Lusinde, akiwaonesha maafisa wa polisi sehemu ya kioo cha gari lake kilichopasuka baada ya kurushiwa mawe na watu waiojulikana wakati masfara wa magari ya kampeni ya CCM, kurushiwa mawe katika kijiji cha Nkinga.
Picha na Victor Makinda
[h=2]Haya yalitokea baada ya Mbunge Livingstone Lusinde kuongea yafuatayo kwenye mkutano wa hadhara.[/h]
KAMPENI za uchaguzi mdogo katika jimbo la Igunga, zimezidi kupamba moto baada ya Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), kujiapiza mbele ya wananchi kuwa atakunywa sumu iwapo chama hicho kitashindwa kwenye uchaguzi huo.
Akizungumza na wanakijiji wa Ugaka kwenye kata ya Nkinga wilayani hapa wakati akimwombea kura mgombea wa CCM, Dk. Peter Kafumu, Lusinde alisema kutokana na mwenendo mzuri wa kampeni za CCM na jinsi wanavyowafikia wananchi, haoni sababu za kushindwa kwenye uchaguzi huo.
"Hapa nimewaona waandishi wa gazeti la Mbowe (Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA); nataka mkaandike kwa namna ambavyo tumezunguka, CCM tukishindwa nakunywa sumu," alisema na kuongeza:
"Nataka tuwaambie, tutawapiga bao la mbali kabisa na huyo Dk. Slaa sisi tunammudu ndiyo maana tukamwambia Mzee Kikwete, endelea kuongoza nchi atuache vijana tumkabe koo maana yule mzee ni mnafiki mkubwa," alisema Lusinde.
"Kale kazee kagonjwa kale, ndiyo maana nimekuja kuwaambia inawezekana viongozi wa CHADEMA wanavuta bangi, zile bangi zile, haiwezekani unatembea nchi nzima unahamasisha vurugu, unatangaza vita," alisema Lusinde Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM.
Tanzania Daima