Gari la Mbunge wa Mtera lapigwa jiwe; aapa kuwapiga bao CHADEMA!

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,886
6,883
IMG_1637.JPG

Hali Tete Uchaguzi Mdogo Igunga; Magari Ya CCM Yapigwa Mawe

Mbuge wa Mtera, Livingstone Lusinde, akiwaonesha maafisa wa polisi sehemu ya kioo cha gari lake kilichopasuka baada ya kurushiwa mawe na watu waiojulikana wakati masfara wa magari ya kampeni ya CCM, kurushiwa mawe katika kijiji cha Nkinga.
Picha na Victor Makinda

[h=2]Haya yalitokea baada ya Mbunge Livingstone Lusinde kuongea yafuatayo kwenye mkutano wa hadhara.[/h]

KAMPENI za uchaguzi mdogo katika jimbo la Igunga, zimezidi kupamba moto baada ya Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), kujiapiza mbele ya wananchi kuwa atakunywa sumu iwapo chama hicho kitashindwa kwenye uchaguzi huo.

Akizungumza na wanakijiji wa Ugaka kwenye kata ya Nkinga wilayani hapa wakati akimwombea kura mgombea wa CCM, Dk. Peter Kafumu, Lusinde alisema kutokana na mwenendo mzuri wa kampeni za CCM na jinsi wanavyowafikia wananchi, haoni sababu za kushindwa kwenye uchaguzi huo.

"Hapa nimewaona waandishi wa gazeti la Mbowe (Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA); nataka mkaandike kwa namna ambavyo tumezunguka, CCM tukishindwa nakunywa sumu," alisema na kuongeza:

"Nataka tuwaambie, tutawapiga bao la mbali kabisa na huyo Dk. Slaa sisi tunammudu ndiyo maana tukamwambia Mzee Kikwete, endelea kuongoza nchi atuache vijana tumkabe koo maana yule mzee ni mnafiki mkubwa," alisema Lusinde.

"Kale kazee kagonjwa kale, ndiyo maana nimekuja kuwaambia inawezekana viongozi wa CHADEMA wanavuta bangi, zile bangi zile, haiwezekani unatembea nchi nzima unahamasisha vurugu, unatangaza vita," alisema Lusinde Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM.

Tanzania Daima

Nasikitikia kitendo cha msafara wa CCM kwenye kampeni kurushiwa mawe kijijini Nkinga huko Igunga, maana ni dalili za kukosa uvumilivu, maana tunaishi watu wa itikadi tofauti na mwenye mvuto zaidi wa itikadi kukubalika na wengi avumilike. Lakini jeuri inapozidi kulazimisha kuungwa mkono taratibu zilizokubaliwa kisheria zitumike badala ya njia ya mkato kama ilivyotumika.

Na kwa hatua hii vyombo vya usalama vinabeba uzito wote kwa hoja ya kuelemea upande wa chama kimoja kukipa upendeleo kinyume cha wajibu wao. Hali hiyo inasabisha kutia hasira wananchi kwa vile hawana njia nyingine ya kutetea demokrasia yao inayobakwa ila kujichukulia sheria mkononi.
 
CHADEMA haijawahi kuunga mkono fujo kama hizi, na watu waliofanya uhalifu huo n wahalifu kama wahalifu wengine; ni kazi ya Polisi kuwasaka wahalifu na kuwawajibisha wao kama wao, na si kutumia kama mtaji kisiasa kwani hatujui watu hao wana kadi za vyama gani!
 
Ukandamizaji wa wazi unapozidi tegemea matuakio ya watu kukosa uvumilivu sasa CCM inabidi kukaa na vyama vingine wakubaliane siasa za ustarabu na waache kutumia polisi na usalama wa taifa kuakandamiza haki za wanachi na wapiga kura
 
Na Yule Fisadi Kikwete aliyepopolewa Mawe kule Mbeya ilikuwaje? Kweli sasa Watanzania wamechoka wanaonyesha kwa vitendo wakisema hawasikilizwi inaweza hii ikwa ni ujumbe kwa Magamba kuwa sasa mwisho wao unakaribia.
 
Nasikitikia kitendo cha msafara wa CCM kwenye kampeni kurushiwa mawe kijijini Nkinga huko Igunga, maana ni dalili za kukosa uvumilivu, maana tunaishi watu wa itikadi tofauti na mwenye mvuto zaidi wa itikadi kukubalika na wengi avumilike. Lakini jeuri inapozidi kulazimisha kuungwa mkono taratibu zilizokubaliwa kisheria zitumike badala ya njia ya mkato kama ilivyotumika.

Na kwa hatua hii vyombo vya usalama vinabeba uzito wote kwa hoja ya kuelemea upande wa chama kimoja kukipa upendeleo kinyume cha wajibu wao. Hali hiyo inasabisha kutia hasira wananchi kwa vile hawana njia nyingine ya kutetea demokrasia yao inayobakwa ila kujichukulia sheria mkononi.

Hakuna neno lolote la ku-justify uhalifu huu wa Chadema. Hawa jamaa wanahitaji kushughulikiwa kwa nguvu zote!
 
dah! yamekuwa haya tena!
natumaini vyombo vya dola vitafanya uchunguzi
wa kina na wa haki ili kuwafikisha wahusika kunakohusika.
 
IMG_1637.JPG

Hali Tete Uchaguzi Mdogo Igunga; Magari Ya CCM Yapigwa Mawe

Mbuge wa Mtera, Livingstone Lusinde, akiwaonesha maafisa wa polisi sehemu ya kioo cha gari lake kilichopasuka baada ya kurushiwa mawe na watu waiojulikana wakati masfara wa magari ya kampeni ya CCM, kurushiwa mawe katika kijiji cha Nkinga.

Picha na Victor Makinda
Pole sana mheshimiwa Lusinde.Lakini huko na wewe umefuata nini maana siyo mtu wa tabora na kamati kuu ccm iliteua ccm mkoa Tabora ,wilaya,tarafa,vijiji zake kusimamia kampeni zote?siasa zenu bwana zinafika wakati tunashindwa kuwaelewa.Faida ya kimbelembele ndo hizo.Watu wote hawawezi kuwa ccm hata kama mtafanyaje wapo tu walio namatumaini na upinzani
 
Sijaona mahala katika thread ya mtoa mada ikithibisha kuwa wahusika ni wana-CDM. Ni hisia zake tu.
 
Na Yule Fisadi Kikwete aliyepopolewa Mawe kule Mbeya ilikuwaje? Kweli sasa Watanzania wamechoka wanaonyesha kwa vitendo wakisema hawasikilizwi inaweza hii ikwa ni ujumbe kwa Magamba kuwa sasa mwisho wao unakaribia.

Hapo umenena mkuu watu wamechoka wakisema hawasikilizwi dawa ni kufikisha ujumbe kwa namna mbali wajione kuwa cheo ni dhamana
 
Hakuna neno lolote la ku-justify uhalifu huu wa Chadema. Hawa jamaa wanahitaji kushughulikiwa kwa nguvu zote!
<br />
<br />
Utaongea sana mwaka huu,Nape kakuongeza posho nini?mwambie chama kimeangalia kibla soon tutakizika.
 
Sijaona mahala katika thread ya mtoa mada ikithibisha kuwa wahusika ni wana-CDM. Ni hisia zake tu.
Hawajamaa wa ccm kila kitu kikifanyika Igunga ni chadema wakati wao kwa wao wanaiba wake za watu ya wezekana ni dhambi zao zinawatafuna maana hata posho wanadhulumiana
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom