Gari la Mbunge wa Mtera lapigwa jiwe; aapa kuwapiga bao CHADEMA!

Chama kinapoamua kutumia vyombo vya dola kukandamiza umma na vilevile sanduku la kura linaposhindwa kutimiza matarajio ya jamii fulani basi jamii hiyo huamua kutafuta alternative means ya kuleta mabadiliko.
 
Huyu Mbunge alisema jimboni kwake hakuna umeme lakini Bwawa la kuzalishia umeme lipo hapo Jimboni kwake,akahaidi kwenda kung'oa nguzo za umeme,huyu jamaa atakuwa Kichaa usikute katoroka Mirembe.
 
Chama kinapoamua kutumia vyombo vya dola kukandamiza umma na vilevile sanduku la kura linaposhindwa kutimiza matarajio ya jamii fulani basi jamii hiyo huamua kutafuta alternative means ya kuleta mabadiliko.
Hiyo altenative means wanayoitumia CDM ni ya kipuuzi!
 
Fujo, hujuma, hasira, matusi, kejeli sio vitu vizuri katika siasa. Uvumilivu, hoja, mifano hai, mipango mahususi na pia mapendekezo ya wengi ni mambo ya maana sana katiika siasa. Pole sana Mbunge wa Mtera. Ila pia ni wakati wako wa kuvumilia na siamini kuwa hayo maneno kama kazee kagonjwa, bangi, yametolewa na mheshimiwa. Ukiingia kwenye siasa kubali kuwa jalala Mheshimiwa MBUNGE. POLE SANA

UVUMILIVU NDIO SIASA NJEMA.
 
Mimi nadhani kuionyeshea Chadema mkono ni uvivu wa kufikiria kwa kweli .Na pia ni siasa za maji taka .Waliopiga mawe ni watanzania wa igunga na wamepiga mawe kwa matokeo ya matusi na kejeli za huyu kilaza wa CCM .Leo Chadema wamefanya nini ? Haya mambo CCM walikuwa wanayafanya siku za nyuma now yanawarudia wanalia lia .
 
IMG_1637.JPG


Hali Tete Uchaguzi Mdogo Igunga; Magari Ya CCM Yapigwa Mawe


Mbuge wa Mtera, Livingstone Lusinde, akiwaonesha maafisa wa polisi sehemu ya kioo cha gari lake kilichopasuka baada ya kurushiwa mawe na watu waiojulikana wakati masfara wa magari ya kampeni ya CCM, kurushiwa mawe katika kijiji cha Nkinga.
Picha na Victor Makinda




Haya yalitokea baada ya Mbunge Livingstone Lusinde kuongea yafuatayo kwenye mkutano wa hadhara.


KAMPENI za uchaguzi mdogo katika jimbo la Igunga, zimezidi kupamba moto baada ya Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), kujiapiza mbele ya wananchi kuwa atakunywa sumu iwapo chama hicho kitashindwa kwenye uchaguzi huo.

Akizungumza na wanakijiji wa Ugaka kwenye kata ya Nkinga wilayani hapa wakati akimwombea kura mgombea wa CCM, Dk. Peter Kafumu, Lusinde alisema kutokana na mwenendo mzuri wa kampeni za CCM na jinsi wanavyowafikia wananchi, haoni sababu za kushindwa kwenye uchaguzi huo.

“Hapa nimewaona waandishi wa gazeti la Mbowe (Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA); nataka mkaandike kwa namna ambavyo tumezunguka, CCM tukishindwa nakunywa sumu,” alisema na kuongeza:

“Nataka tuwaambie, tutawapiga bao la mbali kabisa na huyo Dk. Slaa sisi tunammudu ndiyo maana tukamwambia Mzee Kikwete, endelea kuongoza nchi atuache vijana tumkabe koo maana yule mzee ni mnafiki mkubwa,” alisema Lusinde.

“Kale kazee kagonjwa kale, ndiyo maana nimekuja kuwaambia inawezekana viongozi wa CHADEMA wanavuta bangi, zile bangi zile, haiwezekani unatembea nchi nzima unahamasisha vurugu, unatangaza vita,” alisema Lusinde Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM.

Tanzania Daima


Siasa uchwara na za matusi tumeshazichoka (in red)
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom