Kwanini viongozi wa CHADEMA wanakiua chama?

TAMKO

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
1,090
762
Nduguzangu wanachadema, Mkumbuke kila mtu amewekeza Nguvu ya namna yoyote kuunda CDM. Na wengine mmeenda mbali na Kuuimarisha Upinzani, Lazima Tuongelee Chama.

Viongozi Wetu Wamekuwa na Maamuzi ya kiuwendawazimu yanayo Dhoofisha Chama, Mawazo yasiyo na Mbadala, Mawazo ya Kukurupuka yasiyo na macho. Wanaamua kwa Jazba na munkari bila kutafakari Madhara yake.

wote Mnakumbuka Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019. Chama Kilisusia. Si kwamba walisusia bila sababu, kulikuwepo na Sababu ambazo Chama kiliona uchaguzi hauta kuwa Huru na Haki. Wanachama Tulitarajia Chama Kimesusia Lazima Viongozi wetu waje na mpango kabambe kujibu mapigo ya susio lao, Tukashangaa kimya.. Kususia Kijinga kabisa, Unakataa jambo na huna njia nyingine mbadala. ni kama mtu anasusia kula, kisha kesho yake anakubali kuendelea kula, simoly ni chizi! Mtu ukiamua Jambo Unalipangila kisawasawa hadi kieleweke!

Leo Watanzania Tutathimini, Je! kususia kwa Chama Uchaguzi Ule Nini chama kimefaidika Hadi leo. Ni Hatua Gani ya Kibabe ambayo Chama Kimechukua kama Karata ya Kususia chaguzi ila - HAMNA. ni kimya, ni Ujinga tu. Na mwisho wa siku Wanaingiza timu kwenye Uchaguzi 2020. Ilikuwa akili za Matope kabisa. Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mtaa ni Kete Muhimu sana kuelekea Uchaguzi wowote mkubwa utakao Fuata.

Chama kwa sasa Kiko bize na Kuimarisha Ugomvi wa Ubabe ndani kwa ndani, CCM iko bize na Kuimarisha Chaguzi, wameanza za shina , sasa Matawi na wanaendelea. mpaka kufika uchaguzi wa serikali za mtaa 2024 watakuwa na Mfumo imara sana. Utashangaa Chadema wanaibuka baadae na kuanza kampeni za mtandaoni. wanabamizwa utaskia uchaguzi haukuwa huru na Haki.

Siamimi kwamba wanafanya mambo haya kama misukule, naamini wanajua wanacho kifanya na wanafanya Maksudi ili Chama kiwe kinashika mkia kila Chaguzi. Viongozi Wanafanya maksudi Kuua chama.

Leo Vijana wa Chadema wanazunguruka mitaani kufanya Elimu ya Umuhimu wa katiba mpya. . Then Mwananchi ndio Chombo cha Maamuzi? Chadema wanajua kale kamsemo kwamba "Mwananchi ndio mwenye Mamlaka ya mwisho ya Maamuzi katika Taifa.." Hakafanyi kazi kwenye Siasa sio Africa tu hata Ulaya. ni Mameno ya Hadaa wajinga wanaamini wakifundishwa Darasani. Hata kama Ikiundwa Katiba bora kiasi Gani kama Mamlaka za Usimamizi hazina meno Itafanyaje Kazi? marekani wenyewe wanasumbuka? mwenye njaa hana maamuzi wala msimamo..

Kabla ya Kubadili Katiba Mila za Nchi husika lazima zibadilike kwanza, na Mila Hubadilika kwa Ushawishi wenye Akili.

Chadema ya Leo Inafanya Siasa mzungu (ambaye sijui yupi wao ndio wanajua) aone wanaonewa labda, Wanakandamizwa, Wanabinywa, .. HATAKAMA, sasa Mzungu mnamjua nyie kweli, Anatetea penye maslahi Yake. Chama chochote Ambacho Hakitafuti kuungwa mkono na Nguvu za wananchi ndani ya nchi yake, kinatafuta Huruma ya Nje hicho chama ni Mfu.

Tukiongea hivi kuna misukule inakuja juu kwamba tunawashambulia viongozi wao waondoke ila Mamluki waingie kuongoza chama, Nduguzangu Fikra kama hiZo zikienea basi Hakuna kiongozi atakaye achia madaraka kwa kuhofia "mamluki" haya kwani hao hamluki watakipeleka chama Chini zaidi ya wapi, mbona chama chenyewe sasa kimekaa matopeni, hakuna mwensekiti wa serijali ya mtaa, hakuna wabunge (waliopo ndio wanatunguliwa) hakuna Lolote kwa chama. chama Kimakaa chini kwenye medani za siasa za Nchi. viongozi wamekirudisha Chama 1992.

Uongozi mpya una Jukumu la Kukiamsha Tena.. kukirudisha Juu.. kushindwa ni kushindwa , hakuna aliye shindwa ambaye hana sababu, anazo tena za maana sana ila KASHINDWA! Basi Waje wengine Wakiinue.

lakini Endapo Chadema, Itaendelea na siasa Hizi za kususia, na jazba na Visasi na visirani 2024 tutakosa serikali za mitaa, 2025 tutakosa Wabunge na Tutaendelea na Visirani hadi 2030.. kama mziki utaendela hivi hadi 2050 huko chama kitajifia Chenyewe.

ukiona wenye akili za kuona mbali wanakishauri chama Namna hii ujue hawapendi Upinzani Upotee. Upinzani wa kweli Ukipotea CCM Itatawala kwa kunyea watu sana. Unaona mbunge CCM anayekula Kodi za wananchi anatumia muda kusema Wanaume wasinyonye maziwa ya wake Zao? jamani, kwani wanaume wanakunywaga maziwa ya kinamama? mambo ya ajabu kabisa.. ni kiwango cha juu cha kukosa challenge!

ukiwepo upinzani imara hawezi kuchezea bunge that way, anabwatuliwa moja hadi atakosa ladha ya kuja bungeni!!
 
Back
Top Bottom