Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare (Chadema) kustaafu Siasa, aaga bunge

digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
7,901
14,365
Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare (Chadema) leo Jumanne Aprili 14 ameaga bungeni kuwa hatagombea ubunge katika uchaguzi Mkuu wa mwaka huu

Hadi uchaguzi mkuu,chama kitabaki na mwenyekiti na katibu tu.

===

Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare (CHADEMA) amekuwa Mbunge wa tatu na wa kwanza kwa wabunge wa upinzani, kutangaza kutogombea nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Wabunge wengine wawili ambao ni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka na Mbunge wa Kuteuliwa, Abdallah Bulembo walitumia Mkutano wa 19 wa Bunge la 11 unaoendelea jijini hapa kuaga, kwa kusema hawatagombea tena.

Akichangia jana Bajeti ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa mwaka 2020/21, Lwakatare alisema, “Leo na mimi natangaza kufuata nyayo za Mama Tibaijuka na Bulembo wote wa kulekule ukanda wa Kagera, napumzika katika siasa, ambayo nimeitumikia kwa miaka mingi na kutumikia nafasi nyingi.”

Alisema akiwa Tamisemi, amekuwa mtumishi kwa muda wa miaka 13 akiwa Ofisa wa Utumishi na Utawala.

“Nikaingia kwenye siasa na nikailipa serikali mishahara ya miezi mitatu, nikabahatika kuwa Mbunge mwaka 2000 na kuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, lakini nikatumikia vyama vya CUF kama Naibu Katibu Mkuu na nikaenda Chadema kama Mkurugenzi wa Ulinzi na Intelijensia.”

Alisema aligombea tena ubunge na kushindwa, lakini alirudi tena mwaka mwaka 2015 na kumuondoa Mbunge wa wakati huo, Balozi Khamis Kagasheki wa CCM.

“Sina deni na niliogombea nao, sina deni lolote na waliowahi kunishinda na niliowashinda, sina deni lolote. Naamini nimejenga upinzani makini na naacha upinzani makini ambao wanaweza kuongoza Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba,” alisema Lwakatare na kuishukuru halmashauri hiyo kwa kufanya kazi bila mgogoro.

“Nishukuru kabisa madiwani wa Bukoba wa vyama vyote kwa kuwa tumeendesha halmashauri tukiwa tunaheshimiana na viongozi wa serikali akiwemo mkuu wa mkoa, nashukuru Mungu kwa kufika hatua hii,” alisema.

Aliongeza “Dk Bashiru (Katibu Mkuu wa CCM) aliwahi kusema kinachokosekana nchi hii ni upinzani credible (wa uhakika), mimi nategemea upinzani credible unategemea na mpanga mipango awe credible kama hayupo credible upinzani hauwezi kuwa credible.”

Lwakatare alimtaka Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo kujipima katika uchaguzi anaosimamia, kama ni halali na kama haupo halali, hata upinzani hauwezi kuwa halali.

“Chama Cha Mapinduzi mmepata fursa ya kuongoza mabadiliko ya vyama vingi, tulitegemea ni upambanishaji wa fikra, tumeona nchi zingine wanapata faida kubwa, uchaguzi wa serikali za mitaa tuna viongozi ambao hawakubaliki kwa wananchi,” alisema mwanasiasa huyo mkongwe

Zaidi, soma;

Lwakatare kustaafu Siasa: Kutoka Bukoba Manispaa Ofisi ya Mbunge 2015-2020 - JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
you-my-friend-are-an-idiot.jpeg
 
Back
Top Bottom