Gari la Mbunge wa Kwimba lapigwa mawe

Watakuwa ni wavivu wa kulima hao,mbunge wao angekuwa amewapelekea pesa wangepiga gari yake na mawe?mbona wabunge wa CCM huwa wanapata ubunge kwa kutoa rushwa kwa nini huwa hawapigi magari yao kwa mawe?.
 
Mgawa rushwa huwa anapigwa mawe au anapelekwa TAKUKURU?
Hao waliorusha mawe wakamatwe washughulikiwe kikamilifu bila huruma
Hii ndio Tanzania kila kitu tunachukilia poa tu maiti za kwenye viroba majibu ya waziri umeyasikia ??
 
Mbona wakipewa pilau wanakula ,leo hii kupewa majembe wafanye kazi wanaona ni vibaya....tena naombeni mchukue hayo majembe na kila mtu aingie shambani.
 
Mtoa taarifa naona umepindisha maana ya Habari. Haiwezekani mtu aje agawe majembe bila wanakijiji kutaarifiwa. Nafikiri watu walipewa taarifa kuwa Mbunge wao anakuja kugawa majembe. But hayo mawe lazima kuna Other source.
 
Kilichoripotiwa ni mbunge kupigwa mawe. Sawa kabisa, lakini sidhani ka kosa ni kugawa majembe! Hayo majembe hawakushurutishiwa, nadhani aliwaudhi kwa kitu kingine. Labda aliwasimanga nayo
 
Kwa maoni yangu ni kweli kwamba kuna kitu ambacho hakijawekwa wazi kilichochochea hasira za wananchi hao kulipopoa mawe Gari la mbunge wao hiyo kusoma kutoa rushwa ni geresha tu. Cha msingi ni kwa mbunge huyo kujitathimini wapi alipo kosea aombe msamaha ajirekebishe na maisha yasonge mbele
 
Taarifa inatia shaka,kugawiwa majembe ndiyo rushwa? Hebu fafanua vizuri kisa ni nn? Hiyo rushwa ni ya nini uchaguzi au kitu gani,wakipelekewa maji nayo ni rushwa,wakijengewa zahanati nayo ni rushwa?
 
Mgawa rushwa huwa anapigwa mawe au anapelekwa TAKUKURU?
Hao waliorusha mawe wakamatwe washughulikiwe kikamilifu bila huruma

Ni kwanini mpaka leo Ligumi hajashtakiwa.Ikiwa serekali ina ujasiri wa kufunika uovu wa Ligumu wananchi wana ubavu gani wa kupambana na Mbunge mgawa rushwa.
 
Kuna haja ya Serikali kuanzisha kampeni za makusudi juu ya kuwaeleza wananchi kufuata sheria za nchi, make siku kadri siku zinavyosonga na ndo wananchi wanazidi kuwa vinara wa kujichukulia sheria mkononi pasi kumsikiliza mtuhumiwa, nk.
Mkuu acha ulaghai... Nchi yeyote. Duniani ikitenda haki uovu hutoweka wenyewe sasa unapoizungumzia Serikali hii ya ajabu ni sawa na kujamba kwenye Maji ili ushuzi usinuke...
 
Gari La Mbunge wa Kwimba kupitia chama cha mapinduzi mh. Mansour limepigwa mawe na kutolewa vioo likiwa linagawa majembe kwa wananchi wa Lunele Jimbo la Kwimba.

Wananchi walifikia hatua hiyo baada ya kukerwa na hiyo tabia ya kuwagawia majembe,kwani walitofasiri kuwa ni Rushwa.

[HASHTAG]#Tunamtakabenakiwahai[/HASHTAG].
Kuna kitu nadhani hakiko sawa kwenye taarifa yako maana sioni support ya vyanzo zaid ya wewe mwenyewe inamana tukio hilo unalishuhudia peke yako??? Kuna walakin na habari hii.
 
Kuna haja ya Serikali kuanzisha kampeni za makusudi juu ya kuwaeleza wananchi kufuata sheria za nchi, make siku kadri siku zinavyosonga na ndo wananchi wanazidi kuwa vinara wa kujichukulia sheria mkononi pasi kumsikiliza mtuhumiwa, nk.

Ukija na kampeni yako na wewe tunakudunda vilevile
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom