Gari kubwa na ndogo hutafautiana speed?

Lukansola

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
5,435
1,597
Habari zenu wana sayansi na teknologia,
najua wengi wetu baada ya kuona hiyo headline kama kawaida mawazo moja kwa moja yameenda kwenye yaleeeeee... mambo yetu yale!!!!! ha ha ha teh teh teh,

Anyways tuyaache hayo, mimi nina swali langu hapa,

Bila shaka wote tunakifahamu kifaa kiitwacho Speedometre ambacho hufungwa kwenye vyombo vya usafiri kwa ajili ya kupimia mwendo kasi wa chombo husika, yaani kwa mfano kama gari inasafiri katika kasi ya km 80 kwa saa mshale kwenye kifaa hicho utatulia kwenye namba 80.

Tunajua pia kwamba magurudumu ya gari ndogo mfano toyota duet ni madogo ukilinganisha na ya gari kubwa kama scania,

Tunajua pia kwamba mzunguko (circumference) wa tairi ya gari kubwa ni mkubwa kuliko wa gari ndogo, sasa swali langu ni kwamba kama gari zote kubwa na ndogo zikiendeshwa katika kasi sawa, yaani km 80 kwa saa (kwenye mshale), zitakuwa zikienda kwa kasi sawa ya barabarani? ukizingatia tofauti ya ukubwa wa magurudumu.

Ni matumaini yangu kuwa swali langu limeeleweka?
 
Haziwezi kuwa sawa kaka, kumbuka Newtons second law inasema F=mass*velocity and speed=velocity which is measured as km/h.

kumbuka pia Momentum=Force as Momentum refers to moving things. It is a product of the mass of an object and its velocity. Momentum is why the driver of a car applies the brake to stop the car rather than just taking his foot off the accelerator. The car has gathered momentum and will continue to move forward after the driver stops accelerating it.

so hizi gari mbili hazina Mass sawa i mean uzito wa lori na Vitz ni tofauti,

hope nimejaribu.
 
Speedometer inapima speed sio mzunguko wa matairi hivyo hizo gari zote ni speed sawa. 80km/h ni ile ile kwa kila gari.

Btw Sungusia speed sio sawa na velocity.
 
Ndio zitaenda sawa, haijalishi matairi makubwa au engine kubwa or watsoever, cha muhimu ni kwamba zote zinatembea in 80 km/h. Speedometer ipo kupima speed/velocity per hour, tire circumference ikiwa included in calculations.
Mfano, inaweza kuwa tairi ya gari kubwa inazunguka mara X in one minute to maintain 80 km/h na tairi ya gari ndogo inazunguka mara Y to maintain speed ya 80 km/h.
Kwa hiyo, gari zitaenda sawa na hazitaachana if zote zitamaintain 80 km/h, lakin tofauti itakuwa kwenye Number of rounds of their tires per given time. Tairi za gari ndogo zitazunguka mara nyingi zaidi ukilinganisha na zile za gari kubwa.
 
Hii thread kama hii iliwahi kuja hapa majibu yaliletwa ningeomba watafiti watoe link for save bandwidth.100,km/phr ya Scania ya Dar express na 100,km/phr ya Duet nisawa ila matairi yatakuwa yanapishana ktk mzunguko!!Duet itakuwa inakimbia zaidi!!
 
Lukansola lazima tunafahamiana maana hili swali hadi tumetaka shikana mashati na watoto wa kitaa. 80km/h za corola na 80km/h za bus zinatofauti gani jamani?
Huyo hapo wa laws za newton ndio kaniacha hoi kabisa.
 
Umekwisha sema mwendo km 80 kwa saa sasa kisichoeleweka ni nini? Awe mnyama duma au treni au pikipiki haijalishi.
 
Ndio zitaenda sawa, haijalishi matairi makubwa au engine kubwa or watsoever, cha muhimu ni kwamba zote zinatembea in 80 km/h. Speedometer ipo kupima speed/velocity per hour, tire circumference ikiwa included in calculations.
Mfano, inaweza kuwa tairi ya gari kubwa inazunguka mara X in one minute to maintain 80 km/h na tairi ya gari ndogo inazunguka mara Y to maintain speed ya 80 km/h.
Kwa hiyo, gari zitaenda sawa na hazitaachana if zote zitamaintain 80 km/h, lakin tofauti itakuwa kwenye Number of rounds of their tires per given time. Tairi za gari ndogo zitazunguka mara nyingi zaidi ukilinganisha na zile za gari kubwa.

I think that is the right answer.
Cha umuhimu hapa ni kujua kuwa speedmeter ya duet na ya scania ni tofuti ktk kukalkuleti speed, mzunguko mmoja wa tairi la scania ni sawa na mzunguko mmoja na robo tatu ya tairi la duet. kwa mantiki hiyo inabidi duet tairi yake izunguke mzunguko mmoja na robo tatu ili iwe sawa na mzunguko mmoja wa scania ili speed ziwe sawa.
Mfano rahisi ni kuwa ukichukua duet uifunge katika scani zianze kuvutana speed meter zitasoma sawa sawa isipokuwa mizunguko ya tairi itatofautiana
 
asanteni sana waungwana, nimeelewa jibu vizuri sana
 
Lukansola lazima tunafahamiana maana hili swali hadi tumetaka shikana mashati na watoto wa kitaa. 80km/h za corola na 80km/h za bus zinatofauti gani jamani?
Huyo hapo wa laws za newton ndio kaniacha hoi kabisa.

ndugu yangu Nyamgluu, you never know huenda ikawa tunafahamiana au ni coincedence time will tell. huyo wa laws za newton tusimlaumu nadhani hakuwa ameelewa swali.
 
habari zenu. sijui kama nitakuwa nimewaelewa. gari mbili,tatu,nne,tano, iwe ndege ya angani au kitu chochote kile duniani vikiwa vinaenda kasi kwa mfano 80kph na kupimwa na speedometer basi vyote vitakuwa na mwedo sawa na hakuna kitakachompita mwenzie kama vitashindanishwa na vyote vikaenda na mwendo huo.

watu wengi wanachanganya bila wao kujua hasa madereva wa magari makubwa kwani magari hayo makubwa hasa mascania utakuta yameandikwa kwenye speedometer speed mwisho 120 na yale madogo yana approx 180 mwisho. lakini utakuta gari kubwa ikiwa 100 ile ndogo hata ikiwa 120 haiwezi kumpita kwa sababu:- ukichunguza ile speedometer kwenye gari kubwa inapima speed kwa mph(miles per hour) na gari ndogo nyingi zinapima kwa kph(kilometeres per hour) now 1mile = 1.6km kwa hiyo ukifanya conversion 120mph = 192kph. kwa hiyo gari kubwa ikienda kwa mwendo wa 120mph ile ndogo inabidi iende 192kph ili ziwe sawa. therefore mi naona hizo units ndo zinazochanganya watu ila speed za aina moja haziwezi kutofautiana.
 
katika link hiyo topic inasema eti starlet ikisoma speedometer 100 inapitwa na scania ikisoma speedometer 80 which is not true, unless zimechakachuliwa. kiukweli ukichukua starlet uifunge sambamba na scania kitaalamu inatakiwa speedometer isome sawa.
kalkulation ya speedmeter ya starlet ni tofauti na ya scania, kuna mambo mengi zaidi ya ukubwa wa tairi kama ukubwa wa injini pia na mambo mengine. na ndio maana ukichukua speedmeter ya scania ufunge ktk starlet na vaisi vesa utapata vitu vya ajabu
 
Haziwezi kuwa sawa kaka, kumbuka Newtons second law inasema F=mass*velocity and speed=velocity which is measured as km/h.

kumbuka pia Momentum=Force as Momentum refers to moving things. It is a product of the mass of an object and its velocity. Momentum is why the driver of a car applies the brake to stop the car rather than just taking his foot off the accelerator. The car has gathered momentum and will continue to move forward after the driver stops accelerating it.
so hizi gari mbili hazina Mass sawa i mean uzito wa lori na Vitz ni tofauti,
hope nimejaribu.

Kwenye nyekundu hapo, F= MXacceleration na wala sio velocity, SI unit ya acceleration ni m/s^2 au N/kg. SI unit ya M ni Kg

Penye blue hapo Veleocty sio sawa na velocity. Speed ni scalar quantity wakati velocity ni vector quantity.
 
Jamani, njia rahisi kabisa pasipo kushusha formula wala nini. Maana ya hiyo 80Km/h ni speed au mwendo unaotumika ambao utakifanya hicho chombo(gari) liwe limefika umbali wa kilometer 80 baada ya saa moja. Sasa kama hiyo gari ndogo itatembea kwa speed ambayo baada ya saa moja itakuwa imefikia umbali wa kilometer 80, kutakuwa na tofauti gani na gari kubwa ambayo nayo dereva wake ataamua atembee speed ambayo baada ya hiyo saa moja awe amefika umbali wa kilometer 80. Kwahiyo kama magari hayo mawili yataanza safari hiyo kwa pamoja kwa lengo hilohilo la kufika umbali wa kilometer 80 baada ya saa moja, basi yatafika pamoja na yataenda sambamba muda wote wa safari.
 
Back
Top Bottom