Gari iliyomgonga trafiki yakamatwa

Gari iliyomgonga trafiki yakamatwa

ni sheria kubandika mbele kushoto.maandishi yapo ila watu hawasomi.i wish ningekuwa na scanner nipige picha nikuwekee hapa uone.sio mazoea
mkuu sio lazima katarasi hizi uzibandike mbele kushoto, ni mazoea yetu tu.
 
serikali yetu yenyewe haieleweki, ninachoamini ilo gari lililomgonga huyo mwana mama lilikuwa kwenye msafara na hapa wanafanya kutuhadaa tuu kama ilivyo kawaida kwa serikali yetu
Mimi ninashindwa hata kujua yupi mwenye ukweli wa hii story. Kila siku inakuja story mpya.

The best way, kukaa kimya na kusikiliza.
 
bora ni gari ya MCHUNGAJI maaana ingekuwa ya shekh tungesikia ya magaidi walitaka kumuua RAIS,
 
bora ni gari ya MCHUNGAJI maaana ingekuwa ya shekh tungesikia ya magaidi walitaka kumuua RAIS,

Inakera mijitu inayowaza udini kwenye kila wakati na kila mahali'!!!!!!
 
Hiyo gari haijamgonga binadamu......gari iliyogonga mtu lazima iwe na mbonyeo au kioo kupasuka au mahali fulani kuwa tofauti na kabla ya kugonga mtu.
BARRY angalia kona hapo kwenye head lamp kushoto utaona kuna mbonyeo na kirusha maji kimechomoka. Lazima marehemu alikuwa anamkwepa ila upana wa gari ni mkubwa, likamgonga.. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema...
 
Last edited by a moderator:
Si nia yangu kuwashushia watu heshima. Lakini nataka tu kukusahihisha. Kwa kauli yako ya mwisho yenye rangi nyekundu. Kwa kauli hii una maanisha, Ponda pia ni mbwa, Lwakatare naye ni mbwa, Basil Mramba ni mbwa, na wengine wote waliowahi kuwekwa kwenye kizuizi cha polisi ni mbwa! Hivyo ndivyo ulivyomaanisha? Siyo siku zote asiyetii sheria manake hana akili timamu. Wakati mwingine mtu anaweza asitii sheria kwa nia njema.
Bado unaendela kujigongagonga. Hao wote uliowataja kesi zao ziko mahakamani na sijui hiyo ya kusema hawakufuata sheria umelitoa wapi.
 
lkn ni kwamba watu huwa sio wasomi yaani namaanisha hatusomi na kuelewa jambo.

wengi wa watanzania hata kama ni gazeti utaona anasoma akimaliza muulize habari imesemaje hiyo??
hata weza hata ku nukuu mstari mmoja akuambie.

hahahah
ngoja
nifanye
research
juu
ya
hili.
 
Mimi nimefurahishwa na uwepesi wa polisi wetu katika kushughulikia hili! ingekuwa hivi na kwa mengine amani ingetamalaki nchini.
 
Mimi ninashindwa hata kujua yupi mwenye ukweli wa hii story. Kila siku inakuja story mpya.

The best way, kukaa kimya na kusikiliza.

kweli ila ukifuatilia mtiririko wa matendo ya serikali yetu unajipatia jibu pasipokufanya research, serikali imekuwa na maneno mengi pasipokuwa na mateendo na kama ingekuwa inaimba taarabu basi mzee yusufu si lolote na si chochote
 
JF bana wakati mwingine ni umbeya tupu.

Mbona jana tuliaminishwa hapa JF kuwa gari iliyomgonga ilikuwa kwenye msafara wa Rais Kikwete na watu kwa hasira wakarusha makombora ya matusi na dharau.
La muhimu, magari ya kwenye msafara wa Rais kidogo yangekuwa yanakuwa machache ili iwe rahisi kwa traffic polisi kuongoza.

Anyway, haijarishi gari ilikuwa ni ya nani. Kuna familia kwa sasa ina omboleza.

Kwa harakaharaka kama ntu aliepost thread alikuwa kwenye eneo la tukio lazima atasema ni gari iliyokuwa kwenye msafara maana ilikuwa inafuatana sambamba na gari zilizokuwa kwenye msafara na kumbuka gari zote za kwenye msafara wa rais hazina namba maalum
 
Gari aina ya Landriver Discovery mali ya Mchungaji mmoja wa Kanisa, imekamatwa.

attachment.php


Taarifa zaidi baadae.

Na mimi ngoja nikasomea uchungaji sasa maana kama hiki chombo ni cha mchungaji shida gani ya kuhangaika na pay as you earn
 
Mbona hii gari haina stika hata moja kwenye kioo,au zimebandikwa kwenye kioo kidogo cha nyuma
 
Back
Top Bottom