Gambia's public sector to have 4-day working week!

Gambia's public sector to have 4-day working week!

kwahiyo na kwenyewe wanafanya kazi siku nne tu katika juma? Au kwao jumamosi na jumapili ni siku za kazi?

Sawa kabisa, jumapili ni siku ya kazi kama kawa. Nilona Dubai na wakristo huenda kanisan ijumaai
 
Weekends maana yake ni mwisho wa wiki, vipi jumamosi iwe wikiendi wakati ni 1st day kama inavojisoma wenyewe "mosi" vipi juma pili iwe mwisho wa wiki wakati ni "pili" second day?

Jumamosi ni siku ya kwanza kwa kiswahili lakini kwa kingereza ni siku ya sita kwa hiyo inategemea waongea jumamosi kwa perception ipi
 
Hata kulala tunalala mapema mno!Haiwezekani sehemu kama Kariakoo eti saa 12 jioni watu wanfunga biashara.Kuna wakati rais alizungumzia hilo lakini utekelezaji sijui unamngoja nani!Tunatakiwa tufanye kazi 24/7.Mabasi yasafiri usiku,mabenki yafunguliwe siku zote.Hongera meneja Saed wa CRDB Kahama kufanya maamuzi ya kufanya kazi hadi jumapili na siku za siku kuu
 
mi nashauri sisi twende mbali kidogo,tupige kazi 24/7 ila tuwe tunapishana tu,mfano ijumaa wakristo waendelee na kazi kama kawaida wakati waislam watakua mapumzikoni kwa ajili ya ibada,jumapili waislam nao waingie mzigoni kama kawa wakiwaacha wakristo wakienda makanisani,jumamosi wasabato tu wapate day off wengine wote kazini.
 
Kwa hoja ya mtoa mada n.k NI KAMA KUONA ALIYEPATA ZERO ANAJIFUNZA KWA ALIYEKOSA FURSA YA KUIJUA SHULE MAMBO YAHUSUYO ELIMU. Naona baadhi ya Watanzania wajilinganisha na hohehahe. Hatari kweli kweli!
 
Nchi hiyo imewatendea haki wazee wa kanzu na makobasi
 
Nchi hii wenye pesa ni wafanya biashara, kwasababu tu, wanafanya kazi siku 365, lini umeskia Kilimanjaro Hotel imefungwa eti kesho ni jumamosi au jumapili?

Kwanini upumbafu mwingi unatokea wakati wa Mrisho?
 
waislamu tunaonewa...ijumaa iwe siku ya mapumziko kama jumapili......katiba mpya


... Umwinyi wenu utawapeleka pabaya! Acheni uvivu, fanyeni kazi, someni kwa bidii' kama mnataka kuendelea.
Mtaishia kulalama lalama kuwa mnaonewa.
 
mi nashauri sisi twende mbali kidogo,tupige kazi 24/7 ila tuwe tunapishana tu,mfano ijumaa wakristo waendelee na kazi kama kawaida wakati waislam watakua mapumzikoni kwa ajili ya ibada,jumapili waislam nao waingie mzigoni kama kawa wakiwaacha wakristo wakienda makanisani,jumamosi wasabato tu wapate day off wengine wote kazini.

Point nzuri boss
 
Kwa hili nakubaliana na Waislamu 100 Percent.

Bora Ijumaa ifanywe siku ya mapumziko kisheria sawa na Jumapili kwa Wakristo.

Kwani Waislamu wanataka siku ya ijumaa kuwa ya mapumziko kwakuwa dini yao inawataka kupumzika siku hiyo takatifu kwao au kwa sababu Wakristo wao siku zao za ibada ni za mapumziko?Jinsi ilivyo,Wakristo wameagizwa kupumzika ktk siku zao za ibada ndio maana lazima wapate mapumziko, kwa Waislamu Kuruani inawataka waende kuswali unapofika muda wa ibada, yaani kitabu chao kimewaruhusu watafute ridhiki kama kawaida siku ya ijumaa na kwenda ibadani unapotimu muda.Tunawaona waarabu ambao wengi wao ni Waislamu katika miji mikubwa hapa Tanzania kama Mwanza,Dar-es-salaam na Arusha jinsi wanovyoendelea na shughuli zao za kibiashara alafu baadae wanaenda kwenye ibada. Kufanya siku ya ijumaa kuwa ya mapumziko ni kuendekeza uvivu na kamwe Afrika yetu haitajitoa kwenye hili dimbwi la umaskini kwa mtindo huu.
 
Tena afadhali tufanye kazi wiki nzima, huu upuuzi wa kupumzika ndiyo maana hatuendelei.Mleta mada amenikumbusha kipindi cha mzee Mwinyi, sikukuu ikiangukia w/end, J'3 ni mapumziko.Eti kwa mtindo huu tuendelee!!!!!

... Mkuu umenena' hawa jamaa sijui kwa nini wanapenda kutofanyakazi. Kazi kulalamika tu! kuwa wanaonewa- wanaendekeza umwinyi umwinyi tu.
 
... Kuna Wakristu wanafanyakazi mpaka siku za jumapili' hawa lalamiki!
Mpaka siku hizi hata Wasabato wanafanyakazi J'mosi. Inakuwaje awa ndugu zetu wameshikie bango' vitu vidogo vidogo visivyo kuwa na tija kwa taifa. "kweli kukosa Elimu ni kitu kibaya"
 
Nikawaida ya WaTanzania kusubiri waone wengine wamefanya kitu ndipo wao waanze Kushangaa shangaa, utasikia maneno kama;
”Wenzetu bwanaa!! WaKenya bwana !!! WaZungu bwana!!!! Sasa WaGambia bwana!!

Kuanzia tarehe 01/Feb/13 Serikali ya Gambia Imeamua siku ya Ijumaa kuwa ya mapumziko kuwapa waislam nafasi ya kujiandaa na kuabudu kama walivyopewa wakiristo siku za Jumamosi na Jumapili

Wa-Gambia watafanya kazi siku nne kwa wiki, kuanzia J’T
atu hadi Alhamisi, saa za kazi zitaanza sa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni, ambapo mfanya kazi atakuwa amefanya masaa 40 kwa wiki sawa na kufanya kazi (J’tatu-Ijumaa) siku tano zakaida

Raisi wa Gambia na wataalamu wa uchumi wamesema:Kitendo cha kufanya kazi siku nne kwa wiki,
kitawafanya WaGambia kupata nafasi zaidi ya shughuli zao za kilimo ambazo ni tegemeo kubwa kwa nchi na pia kutawapa nguvu mpya ya utendaji kutokana na mapumziko marefu


Je Uongozi wa Tanzania unauwezo wa kufanya Maamuzi magumu ?

Source: BBC News - Yahya Jammeh gives Gambians an extra day off

Hayo ni ya Wagambia, hii ni Tanzania. Naamini wamefanya hivyo kama ambavyo inaonekana hapo kwenye RED. Nasema hivyo kwa sababu hakuna sehemu yeyote kwenye Quran yenye kusema kuwa Waislam wasifanye kazi Ijumaa (kama ipo iweke hapa)

Halafu nadhani ni upuuzi kusema kuwa siku imetolewa ili WAISILAMU ....... kama walivyopewa WAKRISTO, kwani Gambia haina watu wa dini nyingine zaidi ya Wakristo na Waisilamu?
 
Huyu jamaa kaja na mawazo ya aina yake, wakati tanzania inataka kujikwamua kwenye dimbwi ka umaskini, hasa elimu inayoonekana kushuka kwa kasi ya kutisha, eti anataka tupumzike siku tatu, kwa maana hiyo wanafunzi watasoma siku 4 kwa wiki badala ya 5.

Anyway ni mawazo yake.
 
Hivi maana ya kazi ni nini? Ufanye kazi ya ofisi j3 mpaka alh halafu ij uende shamba mpaka j2 sasa utapumzika lini? Hii ipo kiimani zaidi.
 
swala sio siku ngapi za kufanya kazi,bali saa ngapi za kufanya kazi kwamahesabu ya mjomba angu(mtoto wa dada angu, wa darasa la 3)12x4=48, sasa sisi wa masaa 40,na hao wa masaa48 wap wanafanya kaz mda mwingi,waachen wa gambia wafanye yao,natuwapongeze kwa kuheshimu uhuru wa watu kuabudu.
 
ikija bongo watoto yatima na wezi watakuwa wengi zaidi ya ilivo sasa..
 
Unapofanya maamuzi kama haya, lazina uangalie aina ya watu ulionao, aina ya usimamizi pia! Vinginevyo nchi inayumba!

Hapa kwetu kutokana na usimamizi mbovu watu wanafanya kazi masaa 25-30 tu kwa wiki!
 
Back
Top Bottom