Gambia's public sector to have 4-day working week!

Gambia's public sector to have 4-day working week!

siku ya Ijumaah inawezekana kuwa ya mapumziko,sio kwamba watu watalala tu bali itakuwa fursa kwa Waislamu kufanya ibada zao kwa utulifu na sio kwa huruma ya boss au muda wa Ijumaah ukifika boss au idara ndiyo inaanzisha vikaa ili tu kukwaza watu wengi wanaopaswa kuabudu siku hiyo.hivyo kama waislamu watapumzika ijumaah wengine ni fursa nzuri sasa ya kumalizia kazi zao ambazo hazikukamilika vizuri wakiwa hima makwao au hata ofisini kwani hakuna anayezuiliwa kuingia ofisini siku ya mapumziko kumalizia viporo vya siku zilizopita kwa utulivu kabisa.pia kunashughuli nyingine huitaji maandalizi mazuri kama vile ufundishaji mashuleni unakuta mwalimu bussy na mwanafunzi bussy hivyo mwalimu huingia darasani bila maandalizi yakutosha lakini ikipatikana fursa zaidi lazima atajiandaa vizuri kisha siku za kazi nikutekeleza aliyoyatayarisha siku za mapumziko.pia kwa wanafunzi ni fursa ya kurejea masomo yao kwa ufasaha zaidi.ebu tutizame uwajibikaji wa sasa wa baadhi ya idara na taasisi za serikali zetu bado uko chini humuona mtumishi akipoteza muda kwa simu na mazungumzo badala ya kufanya kazi,masaa aliyofanya kazi ni masaa 4 ndani ya masaa 8 na nusu.huu si ufisadi wa muda.
nikimalizia watu wachangie kwa uzalendo na kuwapendea wenzao mazuri,kwani kama huyo tusemaye aje afanye kazi muda wote kama hapati muda wa kupewa maneno ya Mungu vizuri,ndiye tukimwendea hatakuwa tayari kutusikiliza na kuwajikika lakini kama tumempa fursa ya kuabudu vizuri na viongozi wa dini wakautumia muda huo kuwajenga waumini tutapata watendaji wazuri,lakini tukiacha tukaongozwa na theories za watu na mataifa ya magharibi tumekwisha.kwani wao mali kwanza au hata wako radhi kutuingiza mikataba mibovu.mambo mengi tumerithi sasa andaa ya kwako mtanzania,yenye kuendana na fursa za nchi na wahitaji ya watu,hivyo kila kundi lisikilizwe.
 
Mh! Huyo rais atakuwa kashauriwa vibaya. Na umaskini wa nchi zetu hizi bado unapumzika siku 3 kwa wiki?
 
Mkuu mbona kama hujielewi unaandika kitu gani?Nani kasema anataka kupumzika ijumaa?Mimi nimesema kuwa nchi nyingi za kiarabu na za kiislamu ijumaa kwao wanapumzika, je hiyo inamaana kuwa nimesema nataka kupumzika? Halafu japokuwa ijumaa siyo siku ya mapumziko lakini kiuhalisia wafanyakazi wa serikali wengi wetu ijumaa tunakwenda kusign tu daftari la mahudhurio then tunatambaa kwenye mishe zetu kila mtu anajivika uislamu kuwa anakwenda msikitini.
Mkubwa, hujielewi wewe au mimi? Formula yangu yeyote anaeunga mkono ubaya na kutoa kigezo hata x naye anafanya najua kabisa naye anaupenda ubaya huo! Ila hajapata fursa tu!
 
Waislamu (baadhi, sio wote) ni kupingana na lolote la western Europe and USA. Kwa vile wazungu wanapumzika Jpili na siku hiyo inahusishwa na kusali kwa wakristo, basi ni kuiga tu. Haya mambo yanakwenda na maagizo ya "Mungu"/"mtume"/"Nabii" unayemwamini. Ninavyojua ni kuwa koran inasema kuwa nenda kaswali baadaye endelea na kazi. Haijasema upumzike!!!!Sasa huyu wa gambia kupumzika amekutoa koran gani. Wakristo wanasema ishike kitakatifu siku ya Mungu usifanye kazi-ndio maana hakuna kazi kwa wakristo jumapili. Ni maagizo kama wanavyoamini.
 
mm nauliza swali hivi kwan masaa ambayo ni ya kazi huku kwetu ni nane kwa siku so kwa siku 5 ni masaa 40 kwa wiki, sion shda kama serikali yao imetafuta namna ya kukompaseti kwa watu kufanya 12 hrs ili kufidia siku ya ijumaa. to me ni bora tukafanya kazi 12 hrs kwa siku, kisha ijumaa tukapumika kuliko kufanya kazi masaa 38 ya wiki ambapo ijumaa ofc nyingi ni nusu siku ili watu waende wakasali misikitini.

ni kiasi cha kufikiri zaid na zaid. swala la msingi apa ni je watu wataweza kudeliver inavyotakiwa kw kufanya kzi 12 hrs consecutively? kwani haya 8 tu nanga inapaa
 
Mkubwa, hujielewi wewe au mimi? Formula yangu yeyote anaeunga mkono ubaya na kutoa kigezo hata x naye anafanya najua kabisa naye anaupenda ubaya huo! Ila hajapata fursa tu!


Bado sikuelewi kiongozi wangu! Hivi mimi nimeungamkono au nimemsahihisha Bwana Lukolo aliposema kuwa hata uarabuni Ijumaa siyo siku ya mapumziko? Hivi hata mtu akipotosha ukimrekebisha unakuwa mfuasi? Hebua fuatilia comment yangu ya kwanza niliyom-quote ndugu Lukolo.
 
Itakuwa vema kama wale wanaoabudu jua na miti nao wakipewa siku zao kati ya wiki
 
waadventist hawawezi kukubali.kwao kupumzika jumamosi ni lazima sio ombi.

Mkuu kijana wangu yupo SAUT Mwanza, hao waadventist unaowasema kuwa jumamosi hawafanyi kazi, pale chuo hiyo jumamosi hawajali huo upuuzi, mpaka mitihani wanafanya siku za jumamosi.

Tubadilike jamani, dini zisiwe mizigo ya kutuzuia kuyafikia maendeleo tunayoyahitaji!
 
Back
Top Bottom