Gambia's public sector to have 4-day working week!

Gambia's public sector to have 4-day working week!

Nikawaida ya WaTanzania kusubiri waone wengine wamefanya kitu ndipo wao waanze Kushangaa shangaa, utasikia maneno kama;
”Wenzetu bwanaa!! WaKenya bwana !!! WaZungu bwana!!!! Sasa WaGambia bwana!!

Kuanzia tarehe 01/Feb/13 Serikali ya Gambia Imeamua siku ya Ijumaa kuwa ya mapumziko kuwapa waislam nafasi ya kujiandaa na kuabudu kama walivyopewa wakiristo siku za Jumamosi na Jumapili

Wa-Gambia watafanya kazi siku nne kwa wiki, kuanzia J’T
atu hadi Alhamisi, saa za kazi zitaanza sa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni, ambapo mfanya kazi atakuwa amefanya masaa 40 kwa wiki sawa na kufanya kazi (J’tatu-Ijumaa) siku tano zakaida

Raisi wa Gambia na wataalamu wa uchumi wamesema:Kitendo cha kufanya kazi siku nne kwa wiki, kitawafanya WaGambia kupata nafasi zaidi ya shughuli zao za kilimo ambazo ni tegemeo kubwa kwa nchi na pia kutawapa nguvu mpya ya utendaji kutokana na mapumziko marefu


Je Uongozi wa Tanzania unauwezo wa kufanya Maamuzi magumu ?

Source: BBC News - Yahya Jammeh gives Gambians an extra day off
 
ahh wapi hata kwa nchi tajiri hawafanyi hivo
bila kazi uchumi utakuwa?
kama kuabudu mchana watu wanaruhusiwa maofisini
lakini sio kusema ijumaa yote iwe mapunziko.jms na j2 ni wekends
 
Tena afadhali tufanye kazi wiki nzima, huu upuuzi wa kupumzika ndiyo maana hatuendelei.Mleta mada amenikumbusha kipindi cha mzee Mwinyi, sikukuu ikiangukia w/end, J'3 ni mapumziko.Eti kwa mtindo huu tuendelee!!!!!
 
Au hayo mapumziko ndio itakuwa ya kufanya maandamano,huyo raisi wa Gambia si ndie mganga wa jadi eti anatibu ukimwi,ndio matatizo ya vibarakashia,hukandamiza ubongo kiasi cha kushindwa kufikiri
 
Hata uarabuni ambako ndiko chimbuko la uislamu wanafanya kazi siku tano na kupumzika jumamosi na jumapili. Sasa utajiuliza nyie wagambia mnautoa wapi huo wa kwenu, ka-nchi kenyewe maskini vile.

Mkuu uarabuni Ijumaa ni mapumziko.
 
kwahiyo na kwenyewe wanafanya kazi siku nne tu katika juma? Au kwao jumamosi na jumapili ni siku za kazi?


Mkuu, soma source ya habari ktk linki niliyoiweka itakusaidia kushiriki vizuri mjada usijeonekana wa ajabu
 
ahh wapi hata kwa nchi tajiri hawafanyi hivo
bila kazi uchumi utakuwa?
kama kuabudu mchana watu wanaruhusiwa maofisini
lakini sio kusema ijumaa yote iwe mapunziko.jms na j2 ni wekends

Weekends maana yake ni mwisho wa wiki, vipi jumamosi iwe wikiendi wakati ni 1st day kama inavojisoma wenyewe "mosi" vipi juma pili iwe mwisho wa wiki wakati ni "pili" second day?
 
kwahiyo na kwenyewe wanafanya kazi siku nne tu katika juma? Au kwao jumamosi na jumapili ni siku za kazi?

Ndo manake, ijumaa ni siku ya mapunziko kwao, jmosi na j2 kazini kama kawa. Wao weekend ni ijumaa na ndivyo ilivyo asa
 
Kusema ukweli kabisa productivity yetu na hasa watumishi wa serikali yaweza average ya siku mbili tu....

Na haijalishi how many day watafanya kazi cha maana ni kubana zaidi wafanyakazi kuleta results
 
watu wanawaza kupumzika tu,wakati nchi yao ni pili toka chini kwa umaskini..!
 
Natamani ungeletwa na huku

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
waislamu tunaonewa...ijumaa iwe siku ya mapumziko kama jumapili......katiba mpya
 
Kwa hili nakubaliana na Waislamu 100 Percent.

Bora Ijumaa ifanywe siku ya mapumziko kisheria sawa na Jumapili kwa Wakristo.
 
Back
Top Bottom