Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,329
- 33,139
Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi Saturday, September 05, 2009 2:58 AM
Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi anajiandaa kuliomba baraza la umoja wa mataifa liifute kwenye ramani ya dunia nchi ya Uswizi na ardhi yake igawanywe na kupewa majirani zake. Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi amesisitiza msimamo wake wa kulitaka baraza la Umoja wa mataifa liifute kwenye ramani ya dunia nchi ya Uswizi na kisha ardhi yake igawanywe na kupewa majirani zake nchi za Italia, Ufaransa na Ujerumani.
Gaddafi anajiandaa kuwakilisha wazo lake hilo wakati Libya itakapoanza zamu yake ya urais wa baraza la umoja wa mataifa kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia septemba 15 mwaka huu, liliripoti gazeti la Daily Mail la Uingereza.
Gaddafi aliwahi kuliwakilisha wazo lake hilo kwenye kikao cha mataifa manane makubwa G8 kilichofanyika nchini Italia mwezi julai mwaka huu.
"Uswizi ni mafia wa dunia na haiwezi kuhesabika kama nchi" alisema Gaddafi kwenye kikao hicho.
"Uswizi inaundwa na jumuiya ya kiitaliano ambayo inabidi irudi Italia, jumuiya nyingine ya kijerumani inabidi irudi Ujerumani na jumuiya ya tatu inatoka Ufaransa inabidi irudi Ufaransa" alisema Gaddafi.
Waziri wa mambo ya nje wa Uswizi alisema kwamba mawazo hayo ya Gaddafi ni mawazo yake binafsi katika kampeni yake ya kupingana na Uswizi.
Uhusiano wa Uswizi na Libya ulitetereka baada ya mtoto wa kiume wa Gaddafi, Hannibal, 33, na mke wake mjazito walipokamatwa na kushikiliwa kwa muda na polisi wa Uswizi mwaka jana baada ya kumshambulia mfanyakazi wa hoteli waliyokuwa wamefikia.
Waliachiwa baada ya siku mbili baada ya kesi yao kufutwa lakini Gaddafi aliamua kulipa kisasi kwa kuondoa kiasi cha dola bilioni tano kutoka kwenye benki za Uswizi pamoja na kuvunja mikataba ya biashara na Uswizi.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3000934&&Cat=2