Gaddafi Ataka Uswizi Ifutwe Kwenye Ramani ya Dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gaddafi Ataka Uswizi Ifutwe Kwenye Ramani ya Dunia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Sep 8, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi Saturday, September 05, 2009 2:58 AM
  Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi anajiandaa kuliomba baraza la umoja wa mataifa liifute kwenye ramani ya dunia nchi ya Uswizi na ardhi yake igawanywe na kupewa majirani zake. Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi amesisitiza msimamo wake wa kulitaka baraza la Umoja wa mataifa liifute kwenye ramani ya dunia nchi ya Uswizi na kisha ardhi yake igawanywe na kupewa majirani zake nchi za Italia, Ufaransa na Ujerumani.

  Gaddafi anajiandaa kuwakilisha wazo lake hilo wakati Libya itakapoanza zamu yake ya urais wa baraza la umoja wa mataifa kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia septemba 15 mwaka huu, liliripoti gazeti la Daily Mail la Uingereza.

  Gaddafi aliwahi kuliwakilisha wazo lake hilo kwenye kikao cha mataifa manane makubwa G8 kilichofanyika nchini Italia mwezi julai mwaka huu.

  "Uswizi ni mafia wa dunia na haiwezi kuhesabika kama nchi" alisema Gaddafi kwenye kikao hicho.

  "Uswizi inaundwa na jumuiya ya kiitaliano ambayo inabidi irudi Italia, jumuiya nyingine ya kijerumani inabidi irudi Ujerumani na jumuiya ya tatu inatoka Ufaransa inabidi irudi Ufaransa" alisema Gaddafi.

  Waziri wa mambo ya nje wa Uswizi alisema kwamba mawazo hayo ya Gaddafi ni mawazo yake binafsi katika kampeni yake ya kupingana na Uswizi.

  Uhusiano wa Uswizi na Libya ulitetereka baada ya mtoto wa kiume wa Gaddafi, Hannibal, 33, na mke wake mjazito walipokamatwa na kushikiliwa kwa muda na polisi wa Uswizi mwaka jana baada ya kumshambulia mfanyakazi wa hoteli waliyokuwa wamefikia.

  Waliachiwa baada ya siku mbili baada ya kesi yao kufutwa lakini Gaddafi aliamua kulipa kisasi kwa kuondoa kiasi cha dola bilioni tano kutoka kwenye benki za Uswizi pamoja na kuvunja mikataba ya biashara na Uswizi.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3000934&&Cat=2
   
 2. S

  Shamu JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapa ndipo anapojiharibia jina kwa kuvifanya vitu vidogo vidog viwe big deal. Mandela inabidi amwambie rafiki yake Gaddaf, to calm down, and relax.
   
 3. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  huyu jamaa atakuwa hana advisors nini? au wanamwogopa. Anadhani yeye ni nani hadi aombe taifa kuondolewa. Na Libya nayo pia ifutwe maana imechanganya raia wa misri, algeria, tunisia, chad, niger na sudan.
   
 4. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Lunacy at its apex!
   
 5. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Huwezi kuchanganya personal issues na business. Sasa kama mtoto wake alimpiga mhudumu wa Hotel alitakiwa afikishwe kwenye vyombo vya sheria. Waafrika tunapenda kujikuza sana pale tunapokuwa tuna madaraka. Huyo mhudumu naye ana haki zake ambazo zinatakiwa zilindwe. Kama hizo bilioni 5 alizoondoa kwenye akaunti Uswizi zilikuwa ni zake na familia yake siwezi kumlaumu, lakini kama zilikuwa ni za serikali yake nitamuona mpumbavu tu.
   
 6. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Yani mpaka leo ulikuwa hujaona kuwa Gaddafi ni mpumbavu? Anazungumza pumba sana! Sijui viongozi wengine wanamwonaje?!
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Sep 8, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Huyu baba juzijuzi alitaka nchi zote za Afrika ziondoe uhusiano wa kidiplomasia na Israel eti kwa sababu Israel imesababisha migogoro mingi ya Afrika. Aliitaja bila aibu Uganda wakati wa Iddi Amin huku akijua kuwa Libya ilikuwa mshirika mkuu wa Uganda wakati wa Iddi Amin na misaada yake ya silaha na wanajeshi imesababisha mauaji ya kutisha Uganda miaka ya sabini. Hili wazo la kufuta nchi kupitia UN sijui amelitoa wapi kwa sababu UN huwa hazianzishi nchi, kazi yake ni kuzitambua tu (recognition) na kuzisajili kuwa mwanachama. Sasa kama nchi haijaanzishwa na UN itakuwaje UN iifute? Kama UN haiitaki nchi fulani kwa sababu ya ku-violate UN Charter au human rights violations itaifutia uanachama au kuiwekea vikwazo! Na hili wazo la kuifuta nchi kwa sababu ina mchanganyiko wa watu watu wa asili ya nchi nyingine ni pumba tupu! Tuseme kwa kuwa Tanzania ina watu wenye asili ya Afrika Kusini (wangoni), Uarabuni, Somalia, India na siku hizi China ndio tuseme nchi ifutwe ili Waafrika Kusini, Wasomali, Wahindi, Wachina, nk waichukue? Huyu mzee akikaa kimya atapoteza nini? Vitu vya kibinafsi vinaingiliaje mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi na nchi? Kweli Walibya wameliwa kwa kuwa na rais mwenye thinking capacity ndogo! Poor Gaddafi!
   
  Last edited: Sep 8, 2009
 8. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  inasemekana kwamba gaddafi kapata jeuri baada
  ya serikali ya uswiss "kumuangukia" mwezi agosti
  na kumuomba suala la mgogoro uliotokana na kukamatwa
  kwa mwanae limalizwe kidiplomasia.
   
 9. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Jamani naona hapa ni kwa sababu tu amezungumza Ghadafi ambaye baadhi yetu hatumpendi kwa sababu fulani fulani, lakini kwa kifupi Uswis ni nchi ambayo imekuwa chaka la mafisadi duniani kwa miaka mingi sasa. Mafisadi wa dunia wanaishi maisha bora sana wanapokuwa huko. Wengine wanaishi milimani wakipata ulinzi bora kabisa wa serikali ya Uswisi. Nchi hiyo imepata utajiri na itaendelea kutajirika kwa mitaji ya fedha zetu kutoka nchi masikini. Hawawezi kubadilika, maana wanahubiri demokrasia na utawala bora kwetu huku wao wakikumbatia wahalifu kutoka kwetu. Jamani kama wakigawanywa itakuwa afadhali maana kuna afadhali kubwa sana kati ya Uswisi na nchi jirani kama Ujerumani na Ufaransa ambako mhalifu anajishauri mara mbilimbili kwenda huko. Jiulizeni Vithlani yuko wapi, ziko wapi fedha zetu za rada na kadhalika
   
 10. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  wewe, wacha hizo. shida zenu mnataka kumsingizia jirani? Kwani Uswiss haitoi account za mafisadi wakikamatwa? itabidi uondoe hadi visiwa vya Cayman Island, nk basi kama ni hivyo!! Kila nchi ina uhuru wa kutafuta ulaji wake kwa njia zake za kubuni. Kama anakamua mafisadi wenu, basi nyie pambaneni na mafisadi, sio mmsingizie yeye.
   
 11. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #11
  Sep 8, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Gaddafi hajasema nchi ifutwe kwa sababu ya ufisadi maana kama ni hivyo itabidi Libya nako ifutwe! Sababu yake ni kwa kuwa mtoto wake kafanyiwa mabaya, wala sio Libya iliyofanyiwa mabaya!
   
 12. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #12
  Sep 8, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Una akili sana we mtoto kuliko hata wakubwa. Hongera sana.Ndio maana huwa wezi na majambazi wakifanikiwa wanaitwa "wajanja" kwa kuwa na wao "wanatafuta njia zao za ulaji za kubuni" na ule usemi wenu wa "kila mtu atakula kwenye meza yake".

  Tutaendelea hivyo hivyo Watanzania kwa Wajanja kama kina..... kuendelea kupeta. Na wengine tutaambiwa hivyo hivyo "muna wivu wa kike", "mumepata wapi mitaji" "ni ugomvi wa kibiashara" na kadhalika na kadhalika lakini nchi inaendelea kuwa omba omba na kutegemea fadhila za hao hao Waswisi.
   
 13. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #13
  Sep 8, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Nashukuru kwa ufafanuzi, ile nimeongeza hisia zangu za hivi karibuni, hasa kuhusu kesi ya rada.
   
 14. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #14
  Sep 8, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  pamoja na ubovu/mfumo wizi wa waswisi, nadhani hoja ya gaddafi inamatatizo. kama dunia itakubali waswisi kumezwa na majirani zao
  nini kitazuia mtu mwengine kutaka nchi fulani imezwe na jirani yake/zake
  kwa sababu ya lugha au kihistoria?

  hata hivyo nakubaliana nawe sana tuu kuhusu jamaa (waswisi) wanavyoshamiri kwa pesa za mafisadi. halafu hata wakibanwa
  kuzirudisha hizo pesa shurti kwa mbinde.
   
 15. s

  saikon nokoren Member

  #15
  Sep 8, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Can He start with Somali land?
   
 16. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #16
  Sep 8, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hatumii akili kama anataka ifutwe why alimpeleka mwanae huko akatibiwe?ujue waarrabu hupenda ubabe na kunyenyekewa especialy wanapokuwa na hela nyingi,nimeishi Libya ni washenzi sana na kupenda kupiga watakapo watu wa chini yao
   
 17. M

  Magezi JF-Expert Member

  #17
  Sep 8, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  hata hivyo Gadaffi anajeuri ya kusema lolote kwa baadhi ya vinchi ambavyo anajua havina uwezo wa kumfanya chochote. Yeye anawaheshimu USA, UK, Canada, France, Germany, Russia, Italy na wengine ambao anajua wanaweza kumbana lakini kanchi kama uswisi kwake haoni kama kana effect yoyote.
   
 18. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #18
  Sep 8, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Mbona wapambe anao kibao tu. Hukuna sherehe yake ya 40 years ya kutawala akina nani walikuwepo??? hata jamaa yetu alikuwepo pia!!!
   
 19. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #19
  Sep 9, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kina nani si omba omba na wajipendekezaji. Hivi huyu jamaa kweli ana akili ya kuongoza nchi? Viongozi wengi Africa ni mananga tu. Uongozi ni wamepewa tu kutokana na vyama vyao kuwa na support kubwa ya walala hoi.
   
 20. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #20
  Sep 9, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  hahaha...ukweli ni kwamba tusisingizie ufisadi wetu kwa watu wengine. Yeye hana kosa maana hela zimekuja kwake kihalali. Sisi wenyewe ndo tupambane na waizi! Hii ndo solution pekee. Nakupata katika wao kushikilia pesa zetu. Lakini siwapi blame wao. Wao ni sawa na mbwa wa mitaani. Watakusanyika mahali panapomwagwa chakula. Hivyo basi solution sio kuwaua mbwa, bali kuzuia umwagaji wa chakula, au sio?
   
Loading...