G55 CHADEMA Ni Wazi kuwa ni Mizizi wa Historia Toka CCM..Je kwa CDM ni Mustakabali wa Demokrasia au Ni chanzo cha Mgawanyiko Ndani ya Chama Hicho?

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
12,622
Reaction score
28,459
20250406_090809.jpg

Wiki hii, tulichangamshwa na habari juu ya kuibuka kwa kundi jipya linalojiita G55 ndani ya chama kikuu cha upinzani nchini, CHADEMA.
Kutambulishwa rasmi kwa kundi hili kulitanguliwa na kuvuja kwa mawasiliano ya kundi la WhatsApp linalojiita G55. Mawasiliano haya yalivuja wakati uongozi wa CHADEMA ukiwa umeitisha kikao na wanachama wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu—huku msimamo rasmi wa chama ukiwa ni #NoReformsNoElection, yaani kususia uchaguzi endapo sheria za uchaguzi hazitaboreshwa.

Katika mawasiliano hayo, aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, alisikika akihamasisha wenzake kutohudhuria mkutano huo. Alidai kwamba kutoenda kwao kutatoa ujumbe kuwa hawakubaliani na msimamo wa chama, na pia kuwakwepa "kufokewa".
20250406_090406.jpg

Miongoni mwa waliotajwa kuwa wanachama wa kundi hilo ni aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Boniface Jacob. Hakuna aliyejitokeza kukana kuhusika na kundi hilo, badala yake baadhi yao waliamua kujitokeza hadharani na kuthibitisha kuwepo kwao ndani ya G55, huku wakitoa msimamo wao.
20250406_090831.jpg

20250406_090954.jpg

Lakini kwa nini jina G55?

Historia Inajirudia?

Kundi hili linajifananisha na lile la mwaka 1993, ndani ya CCM, ambapo wabunge 55 walijitokeza kuunga mkono hoja ya mbunge wa Chunya, Njeru Kasaka, aliyependekeza kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano. Hoja hiyo iliwasilishwa kufuatia hatua ya Zanzibar kujaribu kujiunga na Jumuiya ya Kiislamu (OIC) bila ridhaa ya Serikali ya Muungano.

Wabunge hao 55 walichachafya serikali ya Rais Ali Hassan Mwinyi, na hoja yao ilitishia uimara wa Muungano. Miongoni mwa wabunge waliokuwa sehemu ya kundi hilo ni
  • Edward Oyombe (Rorya),
  • Lumuli Kasyupa (Kyela),
  • Phares Kabuye,
  • Sebastian Kinyondo (Bukoba), na
  • Twaha Ulimwengu maarufu kama "Jenerali Ulimwengu" (mbunge wa kuteuliwa).
Kutokana na nguvu ya hoja yao, Serikali ililazimika "kuwazima" kwa kuwateua katika nafasi mbalimbali serikalini, hatua iliyotafsiriwa kama njia ya kuwanyamazisha.
  • Edward Oyombe Ayila – Aliteuliwa kuwa Balozi, akipelekwa kuwakilisha Tanzania katika nchi za Afrika Mashariki.
  • Sebastian Rweikiza Kinyondo – Aliteuliwa kuwa Naibu Waziri katika moja ya wizara muhimu.
  • Lumuli Kasyupa – Aliteuliwa katika moja ya bodi za taasisi nyeti za serikali.
  • Twaha Ulimwengu "Jenerali" – Alishikilia nafasi ya ushauri wa kisera serikalini.
20250406_090508.jpg

Kuibuka kwa G55 mpya ndani ya CHADEMA kunaibua maswali mengi kuhusu afya ya demokrasia ya vyama vingi nchini. CHADEMA, ambacho kimekuwa kinapigania mabadiliko ya kisiasa kwa miaka mingi, sasa kinakumbwa na changamoto ya msimamo wa ndani.

Je, kundi hili ni dalili ya ukosefu wa maridhiano ya kimkakati ndani ya chama, au ni njia ya kutafuta mwelekeo mpya wa kisiasa?

Katika demokrasia, tofauti za kimtazamo ni sehemu ya ukuaji. Lakini pale tofauti hizo zinapozua migawanyiko mikubwa na kuvuja kwa taarifa za ndani, huashiria kasoro kubwa ya mawasiliano na maelewano ya ndani ya chama. Kama CHADEMA haitadhibiti mvutano huu kwa njia ya kidemokrasia, kuna hatari ya kudhoofika zaidi kuelekea uchaguzi mkuu.

Lakini pia, kama ilivyokuwa kwa G55 ya mwaka 1993, kundi hili linaweza kuwa chachu ya mageuzi ya kweli—kwa chama chenyewe na kwa siasa ya Tanzania kwa ujumla.

Historia imetuonyesha kuwa pale hoja yenye msingi inapowasilishwa kwa nguvu na msimamo wa pamoja, inaweza kuibadilisha nchi. Swali linabaki: Je, G55 ya CHADEMA ni sauti ya mabadiliko au ishara ya mgawanyiko?

Wakati ndio utakaotoa majibu.
 
View attachment 3294627

View attachment 3294628
Miongoni mwa waliotajwa kuwa wanachama wa kundi hilo ni aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Boniface Jacob. Hakuna aliyejitokeza kukana kuhusika na kundi hilo, badala yake baadhi yao waliamua kujitokeza hadharani na kuthibitisha kuwepo kwao ndani ya G55, huku wakitoa msimamo wao.
View attachment 3294630
View attachment 3294631

  • Phares Kabuye – Baada ya mchakato wa G55, aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa (Mara)

View attachment 3294635

Hata wewe nikufundishe kitu, katika maisha ukitaka kufanya jambo anza na watu wachache wenye uelewa wa haraka hao wengine watajoin baadae muda wao wa kuelewa ukifika
 
Shida Ni kwamba Wale G55 wameanza Kuenguliwa Kwenye Nafasi zao Tofauti na G55 ya CCM ambayo.Ilipewa Nafasi za Juu ili kuzima Msala..
Ila hawa Wanakula Demotion angalia Mifano Utaielewa
 
Hata wewe nikufundishe kitu, katika maisha ukitaka kufanya jambo anza na watu wachache wenye uelewa wa haraka hao wengine watajoin baadae muda wao wa kuelewa ukifika
Point. Pia usipende kujibizana na wasio kundini. Wape nafasi waliokuelewa wawajibu.
 
Kwahiyo MTU anaweza kuwa anacheza Simba Ila analipwa na Yanga Mshahara .

Maana kwa akili ya haraka haraka haiwezekani uende Kugombea huku unajua hautafanyiwa haki.

Madhara ya Mchezaji wa Yanga kulipwa na Simba ndo haya.
 
G55 hawana nguvu huku Chini kwa Watu wa Kawaida ni watu walizoea aidha kubebwa na chama au mtu Fulani Mkubwa
Ila Ile one to one wengi wao uwezo wao upo k average.

Nafikiri CCM watawatumia kuigawa CHADEMA na kuikosesha nguvu lakini kikosi cha G55 Hakina makali kwa wananchi.

Naweza Kusaidiwa kwenye hiyo G55 ni Nani hasa mwenye Ile nguvu ya ushawishi kwa Umma ambaye CHADEMA wanaweza kumhofia au CCM wanaweza kujivunia kumtumia kuivuruga CHADEMA.
Nani hasa?
 
Hiyo G55 nahitaji kumjua hata mtu Mmoja ambaye anaushawishi. Mmoja tuu.
 
View attachment 3294627

Wiki hii, tulichangamshwa na habari juu ya kuibuka kwa kundi jipya linalojiita G55 ndani ya chama kikuu cha upinzani nchini, CHADEMA.
Kutambulishwa rasmi kwa kundi hili kulitanguliwa na kuvuja kwa mawasiliano ya kundi la WhatsApp linalojiita G55. Mawasiliano haya yalivuja wakati uongozi wa CHADEMA ukiwa umeitisha kikao na wanachama wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu—huku msimamo rasmi wa chama ukiwa ni #NoReformsNoElection, yaani kususia uchaguzi endapo sheria za uchaguzi hazitaboreshwa.

Katika mawasiliano hayo, aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, alisikika akihamasisha wenzake kutohudhuria mkutano huo. Alidai kwamba kutoenda kwao kutatoa ujumbe kuwa hawakubaliani na msimamo wa chama, na pia kuwakwepa "kufokewa".
View attachment 3294628
Miongoni mwa waliotajwa kuwa wanachama wa kundi hilo ni aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Boniface Jacob. Hakuna aliyejitokeza kukana kuhusika na kundi hilo, badala yake baadhi yao waliamua kujitokeza hadharani na kuthibitisha kuwepo kwao ndani ya G55, huku wakitoa msimamo wao.
View attachment 3294630
View attachment 3294631

Lakini kwa nini jina G55?

Historia Inajirudia?

Kundi hili linajifananisha na lile la mwaka 1993, ndani ya CCM, ambapo wabunge 55 walijitokeza kuunga mkono hoja ya mbunge wa Chunya, Njeru Kasaka, aliyependekeza kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano. Hoja hiyo iliwasilishwa kufuatia hatua ya Zanzibar kujaribu kujiunga na Jumuiya ya Kiislamu (OIC) bila ridhaa ya Serikali ya Muungano.

Wabunge hao 55 walichachafya serikali ya Rais Ali Hassan Mwinyi, na hoja yao ilitishia uimara wa Muungano. Miongoni mwa wabunge waliokuwa sehemu ya kundi hilo ni
  • Edward Oyombe (Rorya),
  • Lumuli Kasyupa (Kyela),
  • Phares Kabuye,
  • Sebastian Kinyondo (Bukoba), na
  • Twaha Ulimwengu maarufu kama "Jenerali Ulimwengu" (mbunge wa kuteuliwa).
Kutokana na nguvu ya hoja yao, Serikali ililazimika "kuwazima" kwa kuwateua katika nafasi mbalimbali serikalini, hatua iliyotafsiriwa kama njia ya kuwanyamazisha.

  • Phares Kabuye – Baada ya mchakato wa G55, aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa (Mara)
  • Edward Oyombe Ayila – Aliteuliwa kuwa Balozi, akipelekwa kuwakilisha Tanzania katika nchi za Afrika Mashariki.
  • Sebastian Rweikiza Kinyondo – Aliteuliwa kuwa Naibu Waziri katika moja ya wizara muhimu.
  • Lumuli Kasyupa – Aliteuliwa katika moja ya bodi za taasisi nyeti za serikali.
  • Twaha Ulimwengu "Jenerali" – Alishikilia nafasi ya ushauri wa kisera serikalini.
View attachment 3294635

Kuibuka kwa G55 mpya ndani ya CHADEMA kunaibua maswali mengi kuhusu afya ya demokrasia ya vyama vingi nchini. CHADEMA, ambacho kimekuwa kinapigania mabadiliko ya kisiasa kwa miaka mingi, sasa kinakumbwa na changamoto ya msimamo wa ndani.

Je, kundi hili ni dalili ya ukosefu wa maridhiano ya kimkakati ndani ya chama, au ni njia ya kutafuta mwelekeo mpya wa kisiasa?

Katika demokrasia, tofauti za kimtazamo ni sehemu ya ukuaji. Lakini pale tofauti hizo zinapozua migawanyiko mikubwa na kuvuja kwa taarifa za ndani, huashiria kasoro kubwa ya mawasiliano na maelewano ya ndani ya chama. Kama CHADEMA haitadhibiti mvutano huu kwa njia ya kidemokrasia, kuna hatari ya kudhoofika zaidi kuelekea uchaguzi mkuu.

Lakini pia, kama ilivyokuwa kwa G55 ya mwaka 1993, kundi hili linaweza kuwa chachu ya mageuzi ya kweli—kwa chama chenyewe na kwa siasa ya Tanzania kwa ujumla.

Historia imetuonyesha kuwa pale hoja yenye msingi inapowasilishwa kwa nguvu na msimamo wa pamoja, inaweza kuibadilisha nchi. Swali linabaki: Je, G55 ya CHADEMA ni sauti ya mabadiliko au ishara ya mgawanyiko?

Wakati ndio utakaotoa majibu.
Hakuna sauti ya mabadiliko wala mgawanyiko.

Hayo ni Mapandikizi ya CCM yanayofanya kazi maalum ya CCM kutaka kubadilisha mwelekeo wa wananchi bada ya kuona agenda ya No Reform No Election imepokewa vyema na Wananchi.

Hao ni madalali wa kisiasa wanaofanya siasa kwa faida zao binafsi na sio faida ya Wananchi.

Hao ni watumwa wa Rushwa na Tamaa za madaraka ambao hata kwenye biblia wamezungumziwa.

Kwa kifupi No matter mtawapa airtime kiasi gani ila Wananchi Wameshawajua kuwa hao ni maadui wa demokrasia ya kweli kwa Watanzania ambao kila siku wamekuwa kwenye lindi la umaskini kutokana na siasa hizi za kilaghai za CCM.
 
Hiyo copy and paste ni ujinga G55 ukifuatilia kwa undani ilikuwa inaundwa na watu 55 na siyo watu 7 kwahiyo kimetumbuliwa .
Yeah na Wanaiga Vibaya kuna watu wanaponza mfano Catherine Ruge wamemponza Maaba Yeye alikuwa Mguu nje mguu ndani sasa amechomolewa ndani kabisa
 
Amejiponza mwenyewe .

Hiyo CPA yake haimsaidii katika kuchanganua mambo
 
Kwa sasa hivi MTU mwenye ushawishi ni TAL tu kwa siasa za Tanzania.

Ila hawa akina wenje , Yericko n.k nahisi ndo wale wachezaji wa Yanga wanaocheza Yanga Ila wanalipwa na Simba
Anhaaa!

Bahati nzuri wale wahujumu wa upinzani round hii watakuwa dhahiri.
CCM walisingiziwa mambo mengi kumbe kuna ambao wapo CHADEMA wanahusika na ubaya uliokuwa unajitokeza.

Watu walikuwa wanasema wanaibiwa Kura na kuna dosari nyingi katika Sheria za tume ya uchaguzi na watendaji Kazi wake.
Wakataka mabadiliko.

Lakini sasa watu haohao hawataki. Huo si ndio unafiki huo.
 
Nafikiri haya ni makundi tofauti. Hii G55 sasa ukitazama malengo yake ni maslahi binafsi; kwamba tuchaguliwe ili tuingie bungeni, ili tukadai mabadiliko hata kama kwa kufanya hivyo umesababisha vifo vya wafuasi wako!

Tuwe wakweli, kati ya hao walioiitokeza katika hilo kjndi ni yupi ukimtazama unasema, huyu anaweza kupata ubunge nje ya chama? Au wanataka kupewa huo ubunge? Na nani? Kwa maslahi gani?

Ile G55 ya akina Ulimwengu, ilikuwa imelenga maslahi mapana ya Tanganyika na hivyo uliona ilivyoungwa mkono.

Hawa wa sasa ni maslahi binafsi. Na katika hilo ndio huoni wakiungwa mkono na wenzao au wananchi wengi, zaidi utashangaa kwamba sasa CCM inawashawishi kugombea na eti watawaunga mkono!
 
G55 hawana nguvu huku Chini kwa Watu wa Kawaida ni watu walizoea aidha kubebwa na chama au mtu Fulani Mkubwa
Ila Ile one to one wengi wao uwezo wao upo k average.

Nafikiri CCM watawatumia kuigawa CHADEMA na kuikosesha nguvu lakini kikosi cha G55 Hakina makali kwa wananchi.

Naweza Kusaidiwa kwenye hiyo G55 ni Nani hasa mwenye Ile nguvu ya ushawishi kwa Umma ambaye CHADEMA wanaweza kumhofia au CCM wanaweza kujivunia kumtumia kuivuruga CHADEMA.
Nani hasa?
Ntobi,Boniface na Mrema Maana Hata maranja Kawakana Kabaki na "No reform no election"..

Unajua Kuna Tatizo Kubwa Sana Ukiangalia kwa Jicho la Tatu tatizo kubwa ninaona ni Mrema Na ni Tangu Mrema siku Lissu anashinda alikuwa anaanzisha mikwaruzano
 
Yeah na Wanaiga Vibaya kuna watu wanaponza mfano Catherine Ruge wamemponza Maaba Yeye alikuwa Mguu nje mguu ndani sasa amechomolewa ndani kabisa
Wacha apumzike , siasa inahitaji watu wenye nia ya dhati .
 
Inafikirisha Sana Mkuu.

Back
Top Bottom