Future ya CCM baada ya Lowassa kung'oka

Future ya CCM baada ya Lowassa kung'oka

uko sawa kabisa umeeleweka,lkn hawa Ukawa tatizo hawataki kujenga hoja na kuueleza ukweli,bali wao wanajua kutukana tu na kutetea waliyokaririshwa na viongozi wao!! Kuhama Lowassa wanaona washashinda uchaguzi kumbe lzm wajue kwamba wafuasi wengi wa ccm waliridhishwa na jina la Maguguli kuwa mgombea urais,hivyo kundi kubwa lililokuwa linamuunga mkono Lowassa liliweka silaha chini ila wakabaki wale waliokuwa wameahidiwa vyeo.
 
akili,majina,tabia,hisia ,hulka huwa vinabaki constant...alafu chama ni variable. cdm ikipokea wote kutoka ccm eti ni mtaji ,sidhan kama itatoa picha nzuri. screening ifanyike ili kulinda heshma ya chama

kumbuka huwezi kuonekana msafi wakati umesimama jalalani
 
Tunaweza kuudanganya umma kuwa chama kipo imara na kitashinda lakini ukweli tunaujua. Mambo si shwari. Tunajikaza kisabuni kwa kurubuni tu. Mchakato wa Dodoma umetujeruhi. Si Lowassa pekee asiyeridhika. Wapo wengi ingawa wenyewe wameamua kunyamaza.

Dodoma imetuacha vipande vipande kama kunde au kande. Dodoma hatujatoka wale. Hadi sasa,CCM imepoteza Wabunge na Madiwani kadhaa. Imepoteza focus na nafasi ya kula nanasi. Kujidai. CCM imefikia kutokwa povu la nguvu mbele ya waandishi. Ya jana ni tosha kuthibitisha.

Ingawa mapengo yatajazwa,lakiní si mwaka huu. Too late to do it now. Ninawajua makada waliojiapiza kupigia kura upinzani ili wapate amani. Walitamani upinzani uanzie chamani. Ukweli ni kwamba,CCM haiko tulivu wala kuwa na wavumilivu. Imejaa wenye nia ovu na wivu. Kumechafuka!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Kikwete alikuwa na Majina mfukoni ya wagombea wa kupitishwa by Prof Mark Mwandosya.
Nae adhibitisha lilikuwa ni Goli haramu la Mkono. Hichi ndicho alichokisema Lowassa kuwa ni unafiki kubaki ccm baada ya kushuhudia ikibaka demokrasia yaani haki za Watanzania pale Dodoma.
Mafuriko yaendelee, kila msafi wa CCM karibu Ukawa.
Zuia Utapeli wa Goli la Mkono!
 
Ilibidi iwe ivyo ili tusikabidhi chama kwa wanamtandao wezi. Nahisi tayari umeshaona shetani amekimbialia mtaa wa pili.
 
Mzee Wangu,
Hawa jamaa ni sikio la kufa,, hawasikii wala hawaambiliki. wameshauriwa sana ... wapi. sasa hakuna namna nyingine, ni kuwatupa tu kama jongoo na mti wake.
 
kikwete yupo Australia anatafutia watoto wake business partiners anajali nini yule mtu bwana
 
kumbe alikuja na majina mfukoni .prof mwandosya heko baba chukua maumizi magumu
 
Tunaweza kuudanganya umma kuwa chama kipo imara na kitashinda lakini ukweli tunaujua. Mambo si shwari. Tunajikaza kisabuni kwa kurubuni tu. Mchakato wa Dodoma umetujeruhi. Si Lowassa pekee asiyeridhika. Wapo wengi ingawa wenyewe wameamua kunyamaza.

Dodoma imetuacha vipande vipande kama kunde au kande. Dodoma hatujatoka wale. Hadi sasa,CCM imepoteza Wabunge na Madiwani kadhaa. Imepoteza focus na nafasi ya kula nanasi. Kujidai. CCM imefikia kutokwa povu la nguvu mbele ya waandishi. Ya jana ni tosha kuthibitisha.

Ingawa mapengo yatajazwa,lakiní si mwaka huu. Too late to do it now. Ninawajua makada waliojiapiza kupigia kura upinzani ili wapate amani. Walitamani upinzani uanzie chamani. Ukweli ni kwamba,CCM haiko tulivu wala kuwa na wavumilivu. Imejaa wenye nia ovu na wivu. Kumechafuka!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Huu ndio ukweli ingawa najua fika kuwa kuna watu watakuja kukupinga maana wanatamani kuendelea kutudanganya kuwa bado hali ni tulivu,wakati hali siyo tulivu tena.
 
Hali si shwari watu bado wana machungu ya kukatwa tangia mgombea anatangazwa watu hawakua Sawa. Na CCM mwaka uu MNA wakati mgumu sana kwa wananchi kwanza hamjafanya mambo mengi, wananchi wamewachoka bado na ndani hamko Sawa. Mwaka huu ngoma inogile sana tu
 
Mwaka huu ndo mwisho Wa ccm Sijawai kupiga kura ila lazima mwaka huu nipige kura ili tuiondoe ccm madarakani
 
Ilibidi iwe ivyo ili tusikabidhi chama kwa wanamtandao wezi. Nahisi tayari umeshaona shetani amekimbialia mtaa wa pili.

Nikujidanganya kuficha pembe la ng'ombe
 
Ilibidi iwe ivyo ili tusikabidhi chama kwa wanamtandao wezi. Nahisi tayari umeshaona shetani amekimbialia mtaa wa pili.

Wanamtandao waliotuwekea kiongozi upande wa pili ndio hao hao watakao tuwekea kiongozi upande wa tatu,hakuna jambo geni hapo!
 
Kutojiamini kwa kamati hii ya maadili ndiyo imesababisha sasa wana CCM tujione dhaifu na ninavyoona tutashindwa. Kamati hii haikusimama katika haki iliyumbishwa na ikayumba, Mzee Man'gula angekataa kupelekwa pelekwa, sasa kazi ni kubwa, sijui tukishindwa tutarudi lini kwenye siasa.

Hhuku mitaani tumekuwa tukizomewa na ghafla tumejiona kama watu dhaifu, kibaya sana wale viongozi waliokuwa wanatoa matamshi ya kuvuruga chama wapo majimboni kusaka ubunge wameacha chama kama hakina mwenyewe.

Kwa kweli wazee hawa wametuua wametufanya kitu mbaya, hii ni kutokana na ukweli kuwa hawa wazee bado wanadhani siasa za miaka 10 iliyopita ndiyo inaendelea, wametuangusha, Nape umetuangusha, wazee mmetuangusha, sijui kwa dakika hizi bao hili tutalirudishaje?
 
Wanamtandao waliotuwekea kiongozi upande wa pili ndio hao hao watakao tuwekea kiongozi upande wa tatu,hakuna jambo geni hapo!

Geni hakuna ila kuna jipya ambalo ni kuhamia kwa kubwa la maadui katika nyumba yenu. Hicho ni kitorondo jiulizeni katika nyumba yenu shetani kaingiaje?
 
Geni hakuna ila kuna jipya ambalo ni kuhamia kwa kubwa la maadui katika nyumba yenu. Hicho ni kitorondo jiulizeni katika nyumba yenu shetani kaingiaje?

Baada ya kuhama ndio unamuona ni adui?ccm jiandaeni kuwa kambi rasmi ya upinzani
 
Baada ya kuhama ndio unamuona ni adui?ccm jiandaeni kuwa kambi rasmi ya upinzani

Ccm haijawahi kusema el ni msafi refer op magamba. Mkuu labda nikuulize na wewe sasa na huyo mwenyekiti wako leo ndio mnaona lowassa sio fisadi?
 
Back
Top Bottom