Pia nijuavyo mimi, maiti za kujifunzia , cadaver, hupaswa kutoka mataifa ya mbali ya watu wasio na uwezekano wowote wa kinasaba na nchi husika, mfano Tanzania inapaswa kuletewa cadaver toka China etc ili wanafunzi wajifunze bila emotional wala remorse, hili la miili ya Dar kupelekwa Dodoma si wanafunzi watakuja kukuta ndugu zao?.
<br />
<br />
Pasco ujuavyo si sahihi. Mara zote maiti ama hutolewa humuhumu nchini au hutolewa nchi za jirani kama Kenya, Malawi n.k. Huwezi kwenda China kuchukua maiti, wakati models zipo. Tunataka miili halisia inayofanana na sisi.
Madaktari wa binadamu kokote duniani hutumia maiti kujifunzia. Katika chumba hiki cha cadaver ambacho ni darasa la Anatomy na pia pathology watu wanamheshimu maiti kama mwalimu. Unajifunza kwa kukata kiungo kimoja hadi kingine. Mwisho wa siku hatakuwa mtu tena, maana vitakuwa ni vipandepande tu ambavyo baadaye huchomwa. Baadhi ya nchi kwa kuheshimu elimu tunayoipata kupitia maiti, wameandika kwenye darasa la cadaver, "Here is the only place where the dead teaches the living".
Kutumia cadaver ni moja ya vitu vinavyomtofautisha daktari wa degree (Medical officer/MD) na madaktari wa "UPE" (Assistant Medical Officers na Clinical Officers). Hivyo hufanya wawe wana uelewa mkubwa wa anatomy, pathology na physiology ya mwili wa binadamu. Enzi zetu tulikuwa tukipewa mwili wa binadamu mmoja (first year), mwaka mzima mnakesha nao. Na mtihani unaweza ukaja wamechukua nerve ya sehemu fulani, wameifunga label wanakuuliza jina lake na vitu ifanyavyo.
Kutumia maiti kujifunzia iko kisheria. Labda tatizo ni namna ya kuzipata maiti. Mimi mwaka wangu kulikuwepo na maiti ya kimasai. Pia niliwahi sikia kuwa kuna mwanafunzi fulani aliacha chuo baada ya kumwona ndugu yake chumba cha cadaver, ni story ambazo hazijathibitishwa.
Sasa twahitaji cadaver, ili madaktari wajue miili yetu kabla hawajaanza kutugusa. Maiti hiyo yaweza ikawa mjombako, shangazi au sio ndugu. Ila lazima tukumbuke kuwa hakuna maiti ambayo haina ndugu duniani, hivyo hilo lisitusumbue. Cha muhimu ni kwamba hawa maiti wanachangia kuacha elimu kubwa kwa wale wanaobaki nyuma yao.
Kuhusu kuhamisha maiti usiku nadhani ni utaratibu mzuri. Wewe ulitaka fuso yenye maiti kumi wanaopelekwa UDOM itoe maiti hao mchana kweupe? Hujui uzito wa maiti? Au wadhani wanaenda kuaga na kuzika? Hata Muhimbili chuo pale maiti wanaingizwa usiku wa manane. Maana wanaingizwa kwenye darasa ambalo aghalabu pembeni kuna ofisi za wafanyakazi tofauti wengine wasiokuwa madaktari.
Sasa tukubaliane tuchukue maiti walioachwa kwa muda gani? Siku kumi na nne? Ukisema siku kumi na nne chache sasa cut off ya siku chache ni ipi? Una dawa za kuhifadhia hao maiti? Una fridge za kutosha? Una umeme wa kutosha? Sasa tuhifadhi miaka kumi ili kila mtu aridhike? Halafu wewe unayesema siku kumi na nne chache, ukienda hospitali ukakuta maiti ikuhusuyo imeshazikwa na mamlaka husika utasemaje? Kwamba fukueni?
Nadhani haya mambo madogo sana, alimradi twatambua kuwa hawa maiti wanastahili heshima, kwa kuwa wanaacha kitu kizuri nyuma kuliko yule anayeenda moja kwa moja kaburini na kuliwa na funza ambako wote tutaishia huko.